Taji Liundi avunja ukimya kuhusu COVID-19

Bandiko halijazungumzia kuhusu mshahara bandiko linazungumzia kuhusu hali ya sasa, namna gan watu wanaathirika na hili Cod19, maswala ya mshahara hapa yanatoka wapi! unafurahi hali za watu kupata madhara we unazungumzia mshahara hapa, wenzako wako na masikitiko we unacheka! utu ndo jambo la kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Uwezo wako wa kufikiria mambo na kuyachakata ni mdogo sana, Soma bandiko uelewe content sio maandishi kisha soma jibu langu.

ina maana watu woooote waliosoma hawajaona hili unalolisema wewe??
 
Unadhani Serikali itatoa wapi fedha za kuwalipa watumishi wa umma kama sekta binafsi zinakufa?! Usijione uko salama kuliko usalama wenyewe ndugu. Hili ni janga kwetu sote haijalishi upo sekta gani.
Mkuu, sijaombea liendelee kwa kumaanisha, ni vile naonesha hassira zangu kwa dharau za hawa watu kwetu sisi
 
Anaandika Taji Liundi

AKIBA INAISHA.
Tunaingia mwezi wa pili sasa baadhi yetu kwenye sekta binafsi/wajasiriamali hatujafanya kazi.
Mimi ni Mshereheshaji.
Djs wangu hawajafanya kazi
Kumbi zimefungwa zote
Watengeneza cake
Wapambaji wengi wanalalamika sana.
Event Planners wanakosa kazi.
Hadi caterers wakubwa wanalia.

Nikipima mbele, napatwa hofu kwamba May na June pia zitapita tupu. Labda July na August pia. Kiufupi 2020 imeharibika kabisa.
Sikujiandaa.
Nisingeweza kujiandaa kabisa na janga hili.

*Mahitaji ya maisha hayakomi, yanaendelea. Kodi. Chakula. Matibabu.
*Najitahidi sana, mpaka sio kawaida kubana matumizi. Lakini bidhaa nyingi zimeongezeka sana bei.

Najiuliza nitafanya nini nikibaki na tuseme 300.000/ May katikati.
Nitamkopa nani?
Nitakopa wapi?

Na marafiki wengi ambao tayari wananiomba hata 30.000/ wadundulize?
Natoaje ikiwa na mimi sina mfuko mrefu?

Wewe ungefanya nini?
Nasoma nje kuhusu stimulus package ya $400/600 kwa mwezi kwa miezi 6 na jinsi waMarekani wanahaha kuipata!

Tunaona kote duniani watu wanapinga kufungwa kwa biashara. Watu wanakaidi. Wanaasi.
Hapa Dar, ukipanda Boda na Bajaj na Uber ndo utasikia malalamiko.
Ukienda sokoni au dukani. Ukienda Mlimani na kujikuta peke yako corridor nzima.

Tufanyeje?
Tutoke turisk?
Tukae bila ajira tufilisike?

Ndio maana nataka kuona takwimu za kweli.
Kila siku.

Ni namna moja ya kupima tulipo. Mafanikio ya kupunguza maambukizi. Inajenga moyo wa kwamba kuna siku maisha yatarejea kama kawaida.

Nimeshabana mkanda mpaka sipumui.
Tupeane ushauri.

Ufumbuzi wa ugonjwa huu kwanza iliyokuwa kuwa kipaumbele.

Sekta zote za uchumi ni hohehah, maambukizi yanazidi, vifo vinazidi haieleweki nini ni nini?

Sidhani kama ni sahihi kudhani kuna umoja popote ikiwamo serikalini katika suala hili.
 
Ufumbuzi wa ugonjwa huu kwanza iliyokuwa kuwa kipaumbele.

Sekta zote za uchumi ni hohehah, maambukizi yanazidi, vifo vinazidi haieleweki nini ni nini?

Sidhani kama ni sahihi kudhani kuna umoja popote ikiwamo serikalini katika suala hili.
Kweli kabisa hata Dada ya Corona imeingia mitini haisikiki tena!!
 
Utaingizaje pesa km walipa kodi wakisimamisha shughuli zao?

Unajua kwamba mshahara inatokana na kodi ?
Haelewi mkuu anafikiriserikali kuna sehemu unatoa mahela na kuwalipa watumishi, hajui kodi za kila mwezi ndio hizo billion mia 6 zinatumika kulipa mishahara, hajui kwamba asilimia zaid ya sabini ya kodi hizo zinatokana na kodi toka sector binafsi ndio yeye analipwa. Tatzo likiendelea hamna mtu atalipwa mshahara mkuu, tuombe Mungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio ujue nani anarun JF, waguse wao uone hiyo ban yake, news zote za Selasini kuhama chadema wameblock ila matusi, dhihaka, kejeli dhidi ya Raisi wa JMTZ ruksa, kwa kuwa siyo wa kwao, unajua ninachomaanisha, ...
Acha bangi ndugu, mwezi mtukufu huu.
 
Kwa sasa wewe hakikisha tu kwamba una mahitaji yale ya msingi kabisa, chakula na malazi. Usihangaike kuwa na kila kitu kama ilivyokuwa siku za kawaida.

Ukishaweza kuwa na chakula na familia yako basi, kaa kimya na kuchukua tahadhari kubwa mno dhidi ya ugonjwa. La sivyo utapata ugonjwa na ndani ya wiki 2 utakuwa umekufa.

Usiangalie eti biashara imeyumba, nakwambia bado hakijayumba kitu subiri utaona kuanzia mwezi wa 6 utatafuta ugali tu na ukipata utashukuru Mungu.

Hivyo usilalamike hili ni janga fanya ya msingi tu na kujilinda usipate ugonjwa manake ukipata ndio mbaya kuliko chochote kwa sasa.
Amina mkuuu Imani yetu wa sita patakua pametulia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom