blackstarline
JF-Expert Member
- Sep 19, 2016
- 3,095
- 7,468
Si kwenye biblia tu hata katika quran na hadith za mtume inasema kafate elimu mpaka uchinaNi sehemu gani ya mithali imeizungumzia China? Na ilizungumziwa kwa jina gani? Msaada hapo Mkuu kuna kitu nataka nikajifunze
hi
hilo jina tanzania tu ni la miungu ya kigeni sina uhakika na tanzania ni muhindi mmoja ndo alishinda hilo shindano la kutafuta jina.
hivyo mwisho wa siku tuendelee kukubali MUNGU wao wanayemtegemea wayahudi ni wakweli nasi tumekubali kumpokea na kufuata kwa kuwa ziko shuhuda mbalimbali kwao na mifano iko mingi daniel 6:16, 2wafalme6:18 na nyingine nyingi.
ila hii haiondoi uhalali wa kutetea yaliyo mazuri yetu ikiwa ni pamoja na historia zetu.
Si kwenye biblia tu hata katika quran na hadith za mtume inasema kafate elimu mpaka uchina
Mkuu, Waafrika ni watu wakuburuzwa tu, kwasababu hatutaki kuzituma akili zetu,.Wazungua wanatumia dini hasa hii ya Kikiristo kwa manufaa yao,ukweli wanaujua,wao wenyewe wazungu huwakuti Makanisani,Uingereza makanisa kibao hivi sasa yanavungwa kwa sababu yanakosa waumini..Swadakta kwa asilimia 100% na hili halina shaka...na watu wengi wamekuwa wagumu sana kulielewa hili hasa huku Africa..
HeeDaah! Yaani upendeleo kumbe umeanzia mbinguni kabisa.
Israel wako favoured kweli...what about us God?
Ushaidi mwingi wa ujanja ujanja mtandaoni kuhus maisha kuanzia mashariki ya kati then baadae fuvu la mtu wa kale kabisa kupata kuishi Duniani linapatikana Tanzania Olduvai gorge..hii ikimaanisha afrika, Tanzania ndio sehemu ambapo maisha yalianzia hivyo technically bustani ya Eden inaweza kuwa ilikuwa Arusha au Mbeya for that case...then baadae middle East wanaiba show na kusema kwao ndio maisha yalianzia tena...C'moooon!
Ubarikiwe mkuu intro maridadi kabisa ukipata fursa uje unimalizie maana hii topic ya uteule wa Israel huwa inanipa maswali mengi sana.... Ukirudi pia utanitoa tongotongo kuna mahala nilisikia ''mtu'' anasema waisraeli hawatokanyaga jehanum hata kama walikuwa dhambini na wamepotea!!! Nilishtuka sana nikabaki na maswali mengi mno naomba ukirudi usisahau na hiloZitto jr hapo#84.
Nitaenda hatua kwa hatua kwa maana haya maswali uliyo ya uliza yana hitaji ufafanuzi wa kina. Ita ni chukua muda, na wakati mwengine nitatumia mtazamo wangu baada ya kusoma maandiko matakatifu (exegesis - hapa uta tathimini mwenyewe ujiridhishe).
Ni kweli kwa kupitia Bwana Yesu Kristo, dunia yote, maadamu umempokea Bwana Yesu, ukatubu dhambi zako, ukabatizwa kwa maji na Roho Mtakatifu na ukaendelea kuyaishi Mapenzi ya Mungu basi umekuwa mteule, kwa maana umeunganishwa na Yakobo, Isack na Abraham kwa kupitia Bwana Yesu.
Hii Abraham, Isack, Yakobo na hatimaye Bwana Yesu ni mchakato/njia tu, wa/ya Mungu aliomua kuipitia ili kumrudishia mwanadamu uzima wa milele. Huu uzima wa milele mwanadamu alipewa na Mungu pale alipo muumba na kumuweka bustani ya Eden. Shetani akaja aka hujumu mpango wa Mungu pale Eden. Mwanadamu akawa ametenda dhambi na matokea yake ni adhabu ya kifo cha mwili na Roho. Mwili una rudi mavumbini uliko toka na Roho/Nafsi inaenda motoni katika jehanamu ya milele maana ilikuwa na dhambi. Roho/nafsi isiyo na dhambi inaenda kuishi katika ule uzima wa milele mbinguni kwa Mungu.(Tumeandaliwa nchi mpya na mbingu mpya)
Ni muhimu kujua kuwa Adam(na Hawa) walipewa kutawala na kumiliki ile bustani na hatimaye kuutiisha ulimwengu wote na vyote vilivyo ujaza. Lazima tukubali kuwa shetani kwa kuwa danganya Adam na Hawa maana yake kachukua zile baraka za kutawawla na kuirithi nchi (kwa maneno mengine). Haya maelezo yako katika Biblia ( Mwanzo 1,2 na 3). Hapa utaona uumbaji na mambo yaliyo tokea mara ya uumbaji.
Sasa tutakavyo endelea mbele utaja ona kuwa huu utaratibu wa Abraham kubarikiwa na kizazi chake ni katika haja ya Mungu kumrudishia mwanadamu kile kilicho hujumiwa na Shetani pale Eden. (Kwenye Biblia utakuta maneno, Adam wa kwanza, Adam wa pili)
Hata baraka za Abraham ziko kiutawala na ziko ki- Ardhi (Kaanani-Eden sina shaka ilikuwa hapa). Soma kuhusu mito iliyo kuwa inatiririsha maji kunyweshea bustani ya Eden na linganisha na mipaka ya nchi ya kaanani, utaona huu ukweli (exegenis). Mwanzo 2:20-25 na 15:18.
Itaendelee ...maana hii itakuwa ndefu sana na ina hitaji muda na subira. Na kijua ninachotaka kukielezea lakini jinsi ya kukiweka ina hitaji umakini. Hopeful uzi huu utaendelea kuwepo.
Muendelezo lodding...
Huu mstari nimeutafuta nashukuru umenipa.Sasa angalia hapo Daniel 3:16-18 ujue jinsi hawa Waisrael walivyo Muamini Mungu wao wa kweli dhidi ya mungu wa mfalme ambaye kiuhalisia ni shetani. Walithubutu kumpa mfalme makavu kuwa hatakama tutateketea katika moto which means watakufa lakini jua kuwa hatuta mtumikia huyu mungu shetani wako. Hivi unafikiri wakati Hawa jamaa wana pelekwa kwenye tanuru la moto nafsi na akili zao hazikupata mahangaiko na mateso, watesi wao wakuwacheka kuwakejeli na kufurahia kuwa wame wa angamiza, lakini walijua kwamba Mungu waliye mtumainia ni wa thamani kuliko uhai wao madaraka yao na maisha haya ya dunia ya kupita tu.
Lakini mfalme, madui zao na hata wale wengine walio jiingiza katika mkumbo wa kuwa kejeli mwisho wa siku waliaibika. Mfalme na miguvu yake yote ya kiutawala, uwezo wake wote wa mali na wale wote alio watawala walilazimika kumuabudu na kumtumika Mungu wa Israel.
Haikuwa hiari ya mfalme wala watu wake kumtumikia Mungu wa Israel bali walilazimika. Hata sisi wengine hatuna budi maana ndiye Mungu wa kweli na yako mambo yaliyo jidhihirisha kwetu kuwa ni wakweli. Hayo mambo ni ya kimwili na kiroho pia kwa pamoja bila shaka yeyote nime amini Mungu wa Abraham, Isack na Yakobo/Israel/Bwana Yesu ndiye Mungu wa Kweli, kwa hili hakuna wa kunitoa hapo.
Kwa wale wanaoamini Yesu ni Mungu,katika kusoma kwangu leo nimeona kisa chengine kwenye Biblia ambacho Yesu kasema kwa mdomo wake kuwa yeye ni Binaadamu aliuetumwa na Mungu kuja kuwakoa wana waisrael walioptea..
Kisa Yesu alikuwa akielekea Jerico,mji mmoja pale Palestina akiwa amezungukwa na watu wengi sana wakimshangilia,Njiani alikutana na mtu mmoja Tajiri sana analieitwa Zakayo,Zakayo alimkaribisha Yesu kwake,wafuasi wa Yesu walikuwa wakimfuata na kumshangilia walikasirika sana kuona Yesu amekuwa mgeni wa mtenda dhambi..
Siku ile Zakayo alimuahidi Yesu kuwa atagawa nusu ya mali yake kwa maskini,nae Yesu akasema kamainavyosema Luka 19:9-10
Luka 19:9-10 Neno: Bibilia Takatifu
” 9 Yesu akamwambia, “Leo, uwokovu umeingia nyumba hii, kwa sababu huyu naye ni mtoto wa Ibrahimu. 10 Kwa maana mimi ni Mwana wa Adamu nimekuja kutafuta na kuokoa waliopotea.”..
Kumbuka kuwa Yesu amesema vile vile kwa wafuasi wake kuwa katumwa na Mungu kwa wana wa Israel tu kama isemavyo biblia Matthew 15:24,pale alipomfukuza na kukataa kumtibu binti wa yule mama ambae alikuwa sio Myahudi…
Matayo 15:24 Neno: Bibilia Takatifu
24 Akajibu, “Nimetumwa kwa ajili ya kondoo wa Israeli(Wayahudi) waliopotea tu.”
Hii inaonyesha vipi Yesu(Isa) yeye mwenyewe hakujipa cheo cha uungu,,,kuna mistari mingi kwenye biblia inayothibitisha hayo,vile vile kuna mistari inayoongea vipi atakuja kuwa kuwapinga wale waliosingia maovu kama haya...
Ubarikiwe mkuu intro maridadi kabisa ukipata fursa uje unimalizie maana hii topic ya uteule wa Israel huwa inanipa maswali mengi sana.... Ukirudi pia utanitoa tongotongo kuna mahala nilisikia ''mtu'' anasema waisraeli hawatokanyaga jehanum hata kama walikuwa dhambini na wamepotea!!! Nilishtuka sana nikabaki na maswali mengi mno naomba ukirudi usisahau na hilo
Usiku mwema
Mkuu kwanini utata uwe kwa Yesu tu mbona kuna wengine wamezungumziwa pia kwenye Qur'an ila suala la Yesu ndiyo limekuwa na mvutano?Hakuna mtenda dhambi ambaye kama hakupata bahati ya neema ya Mungu na kutubu kabla hajafa atakaye epuka kwenda motoni/jehanamu. Hawa Waisrael wenyewe katika mlolongo wa maisha yao ya kikuhani wali adhibiwa na Mungu papopapo bila kuchelewesha kila walipo kengeuka.
Yuda ni mwanafunzi wa Yesu na Myahudi/Muisrael alitenda dhambi ya kumsaliti Bwana Yesu ingawa alitahadharishwa kuwa dhambi imemuingia lakini akamua kumtumikia shetani kwa vipande 30 vya pesa. Hatima yake iko wazi kwa kila mmoja kuelewa.
Hili fundisho la kuwa kama hukupata neema ya kutubu dhambi unaenda jehanmu liko pale msalabani Bwana Yesu alipo sulubiwa na wale wahalifu wawili mmoja upande wake wa kuume na mwengine kushoto. Kilichotokea kwa hawa wawili kina julikana.
Ni ongezee chabuso, ina onekana unatatizo la usahaulifu hapahapa si kuna posts zenye mistari ya Biblia zinazo onesha kuwa tunaunganishwa na Israel,Isack na Abrahamu kwa kupitia Bwana Yesu, kwa ubatizo. Na bila kupitia kwa Bwana Yesu hakuna kuona ufalme wa Mungu.
Na kwa vile shetani analijua hilo na anayajua vizuri sana maandiko ndio akataka kuaminisha watu/umma kuwa Issa SA ndiye Bwana Yesu. Na asinge fanya hivyo na kuhakishia ange kwama kabla hata ya kuanza. Kwa kufanya hivyo kawapata wengi mno.
Ziko taratibu maalumu katika Biblia ni jinsi gani ya kumpokea, kumfuata na kuwa mfuasi wa Bwana Yesu, nje ya hizo ni upotevu mtupu.
Asante Mshana Na ubarikiwe Nimekuelewa hayo maswali 4 ya hapo juu uliyo Uliza yameniongezea kasi Kama power safe kwa bacteria sijutii wala kuhofia kusema mungu hayupo kwangu
Na mm naongeza swali moja ELOI ELOI LAMA SABAKHTANI?
Kama mungu wetu wote mbona unawapandelea taifa moja? Ni Sawa Na baba ktk familia uwe Na watoto wengi halafu uwe kila ukirudi kazini unamletea zawadi mtoto mmoja
HADHAA MIN FADHWIL WARABI
Mungu akupe hekima Na busara Na upendo kwa watu wote bila ya kubagua rangi,Kabila wala Imani za kidini
Mwezi mchanga uyo. Usisumbuke naye mkuuJifunze kufuatilia mjadala wote hatua kwa hatua kabla hujaamua kuchangia... Ungekuwa umefanya hivyo usingekuja na swali lako hili
Ahahaha! Eti "mwezi nchanga"Mwezi mchanga uyo. Usisumbuke naye mkuu
mshana. Jr