Mimi na zungumzia imani yangu unless tukubaliane kuwa iko Taurati, injili, Zaburi, Methali nk ambazo ni za Kikristo tu na nyingine za Kiislam tu. Lakini kama Abraham, Musa, Daudi, Bwana Yesu akiwa hapa duniani, kuwa hizi ni nafsi mojamoja, basi wale wa imani ya Kikristo watakuwa wanafanya makosa wakisema Yesu Kristo ndiye Issa SA. Sio Kweli kwa mujibu wa Biblia.
Yesu Kristo hakuacha kusema kwa uwazi kabisa ni amri/utaratibu gani wanadamu wanapaswa wafanye ili kumfuata yeye. Lazima kama Mkristo ujue kuwa Bwana Yesu alikuwa Mungu kweli na pia Binadamu Kweli. Hivyo alipokuwa anaelekeza ni taratibu gani zitumike ili kuwa mfuasi wake alikuwa akitimiza majukumu mawili kwa wakati mmoja, yaani lile la Kiungu na lile la kinabii mwanadamu.
Hawa manabii wengine wote tunao wajua walikuwa wanatimiza majukumu waliotumwa na Mungu/ Bwana Yesu kwa wanadamu ili hatimaye wanadamu waweze kufika kwa Mungu wao mbinguni na wasiishie jehanamu/motoni.
Kwa mkristo anaye ijua Biblia vizuri kumuambia Mtume Muhamad SA ni mtume/ nabii wa Mungu kamwe hawezi kukubali. Maana atakuuliza, je alibatizwa kwa maji na Roho? Jibu ni hapana. Na kama ni hapa wala huyo hamjui Bwana Yesu/Mungu si mmoja kati ya wale wa Yesu. Kusema unamjua Bwana Yesu wakati hufuati yale maagizo aliyokupa ili uwe mfuasi wake ni kujidanganya kwa ajili ya kujifariji kibinadamu. Kweli Mungu ni mmoja kwa maana wote tunao amini katika umbaji twa amini yeye ndio muumba wa vyote. Lakini katika ufuasi/kumfuata Mungu hakika hatumfuati Mungu mmoja. Wako waliopata neema ya kumfuta Mungu wa Kweli na wako ambao hawajaipata hiyo neema, Wamepotea/wamepotezwa lakini hawajui.
Kuhusu Taifa teule la Mungu ni kweli huu ndio utaratibu wa Mungu alio jiwekea ambao unajidhihirisha kwetu hata kwa kutumia logic ya akili za kibinadamu.
Umeeleza Vizuri kuhusu Abraham kuchaguliwa kuwa uzao wake ndio utaunda hilo taifa teule la Mungu . Nimesha sema mara kadhaa humu ni taifa teule kwa maana ya kuwa Mungu ageliwatumia wazawa/baadhi ya watu kutoka vizazi hivyo kwa ajili ya kuwa humbiria/kutoa ujumbe/ unabii uhusuo mambo ya Mungu na jinsi gani ya kumtii na kumtumikia.
Utaona alimchagua Abraham kwanza, katika watoto wa Abraham akachaguliwa Isihaka, katika watoto wa Isihaka akachaguliwa Yakobo nk ,nk, Mwishowe alichaguliwa Mfalme Daudi ambaye hatimaye kwa kupitia uzao wake Mungu mwenyewe alikuja hapa duniani kama Emanuel ambaye ni Bwana Yesu.
Baada ya Bwana Yesu Kuja hapa duniani wafuasi wake, yaani wale walio mpokea yeye kuwa Bwana na Mwokozi wao, nao kwa kupitia YESU wamekua/wamefanywa kuwa taifa teule la Mungu. Na ndio maana Mungu Mwana au nafsi ya Mungu ya uana/ubinadamu ilitia timu yenyewe hapa duniani kufanya kazi hiyo.
Kuhusu dini ya kiyahudi ni kweli kuwa asilimia kubwa ya Wayahudi, Mungu kawanyima hiyo neema ya kumkubali na kumtambua akiwa hapa duniani. Hata hivyo Tora yao imewawekea wazi kabisa kupitia manabii ambao ni ndugu kati yao wanadamu, kuwa atakuja Masihi/Bwana Yesu kuchukua pahala pa Mfalme Daudi. Wao wakaishia kufikiria mambo ya kimwili zaidi na wakasahau ya Kiroho. Wakadhania Masihi angewashindia vita hivi vya adui wa Kimwili,. Kumbe Masihi ni kweli kawashindia ile vita ya kiroho ambayo ni kupambana na dhambi na kushinda adhabu yake ya kifo cha kiroho na kimwili. Ukisha shinda vita vya kiroho ndio umemshinda shetani, wafuasi wake na kazi zao zote.
Utaona kuwa baada ya Bwana Yesu/Mungu kuja hapa duniani na kuwa fanya wafuasi wake walio mpokea kuwa taifa teule, aliwapa wale wafuasi baraka za kwenda kuuhubiri ulimwengu mzima habari njema za Wokovu wa Mungu kwa mwanadamu. Pia akawapa msaidizi Roho Mtakatifu ambayo ni nafsi ya Mungu ya tatu kuwa ongoza.
Yeyote aliye kuja na Imani ya Kiislam alikuwa makini kwa kujinasibisha kwa Mungu pale aliposema tunamkubali Nabii Issa SA (kwa mujibu wao Bwana Yesu/Issa bin Mariam) na mafundisho yake na akaenda mbali kwa kutengeneza mazingira ya kuwa aminisha wanadamu kuwa Mungu/Bwana Yesu ndio Nabiii Issa bin Mariamu ndiye Yesu. Wakati kama wewe ni mkristo uliye pataa neema ya Mungu ya kulijua neno la uzima la Mungu/Biblia kinachotajwa na wenzetu wa Uislam kusuhu Bwana Yesu eti ndiye Nabii Issa SA sio kweli. Na Mkristo kusema Nabii Issa wa Quran Tukufu ndiye Bwana Yesu wa Biblia anatenda dhambi ya uongo na anapaswa kutubu.
Sawa Mkuu,sote tuko sawa kwa Mungu,isipokuwa Bani Israel wao walichaguliwa kama binaadamu wa kusambaza yale aliyoyataka Mungu,yaani kuabudu Mungu mmoja na kufuata sharia zake..
Mapenzi ya Mungu kwa Bani Israel,na ule uteule aliowapa wa kusambaza aliyoyaamuru kayaondoa kwasababu hawa jamaa wameshindwa kuyafanya yale anayoyataka Mungu,Hawa jamaa wamelaaniwa,hakuna hata Mtume mmoja walioletewa wakamkubali…
Baada ya kumkana Musa,Bani Israel(Wayahudi) walikuwa wanasubii Masaya(Kristo kwa lugha ya kigiriki),Mungu akawaletea Masaya(Yesu aka Isa aka Iso aka Yoshua aka Jesus) lakini hata hivyo wakamkejeli na kumsulubu Msalabani..
Kuna watanzania humu JF wanafikiri dini ya kiyahudi(Hebrew) inamkubali Yesu(Isa) lakini hawajui kuwa Wayahudi wa kale na hawa wa sasa hawana habari kabisa na Yesu kwao wao wanamuona Yesu tapeli,mzushi tu..
Kutokana na Kukataa na kuwakejeli Mitume,Mungu kaahidi kwenye Quran kuwa,wale wataowakejeli na kuwakataa Mitume atawaondoa na kuwachagua Wengine,Mungu kamleta Muhamad ambae ni mtume pekee ambae sio Myahudi,Muhamad kafundisha yale yale aliyoyaleta Musa sema akasawazisha mengine na kuzidisha yale yaliokuwa hayajamaliza kuyafundisha Isa(Yesu)...