Taifa stars yachapwa 2-1 na Libya jijini Benghazi

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,305
24,198
27 September 2022
Benghazi, Libya

Live Broadcast match Libya vs Tanzania

FINAL SCORE LIBYA 2 - 1 TANZANIA


Head Coach Honour Janza na kocha msaidizi Mecky Mexime
  • Aishi Manula
  • Abdallah Mfuko
  • Dickson Job
  • David Gilbert Ulomi
  • Shomari Kibwana
  • Himid Mao
  • Reliants Lusajo
  • Muzamiri Yassin
  • Sospeter Bajana
  • Simon Msuva
  • Joshua Ibrahim
Source : Jordan Football

Dakika 17' :
Penalti GOAL ! Libya 0 - 0 Tanzania Aishi Manula anadaka lakini alitoka nje ya mstari, penati inarudiwa

Dakika ya 21' GOAL !
Libya wanarudia kupiga penati Abdulati Al Abasi anatikisa nyavu .
Libya 1 - 0 Tanzania

Dakika 25' : Libya 1 - 0 Tanzania

Dakika 40' : Goal ! Said Khamisi ! Taifa stars wasawazisha .
Libya 1 - 1 Tanzania

Dakika 48' Goal! Muhammad Soulah wa Libya ajipatia goli la pili kwake yeye na kwa timu yake, hivyo ubao unasoma Libya 2 -0 Tanzania

Dakika 59' Reliants Lusajo Mwakasugule header safi ndani ya 18 almanusura Taifa wasawazishe, ubao bado unasomeka Libya 2 - 1 Tanzania

Dakika 63' Libya wanaingia ktk 18 za Taifa stars kwa gonga za Abesi na Munir one - two kwa kasi kubwa lakini Aishi Manula anaokoa

Dakika 71' Libya wanaonesha udambwiudambwi kwa gonga safi kwa kumiliki mpira wote zinazowainua mashabiki uwanjani.

Dakika 73' Mecky Mexime kocha msaidizi Taifa Stars anainuka kuwachagiza wachezaji kubadili mchezo

Dakika 74' kona nzuri inachongwa kuelekea goli la Libya, inaokolewa na sasa counter attack


Dakika 75 Libya wanafanya counter attack ya kutisha, sekunde 30 wanamtafuta Aishi Manula lakini Muhammad Sola anapata kigigumizi

DAKIKA 90' Full Time

Libya : Abdulati al Abasi 21' pen, Mohammed Soulah 49'

Tanzania : Said Khamis 40'

MATOKEO:

LIBYA 2 - 1 TANZANIA

====

TAIFA STARS YACHAPWA 2-1 NA LIBYA JIJINI BENGHAZI


TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imechapwa mabao 2-1 na wenyeji, Libya katika mchezo wa kirafiki usiku wa Jumanne Uwanja wa Modern Jijini Benghazi.

Bao pekee la Taifa Stars kwenye mchezo huo limefungwa na kiungo Said Hamisi Ndemla huo ukiwa mchezo wa pili wa kirafiki nchini humo ndani ya wiki moja baada ya awali kushinda 1-0 dhidi ya Uganda. Tanzania ilicheza na Uganda katika mchezo wa kwanza Jumamosi ya September 24 na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0, bao la Simon Msuva.
 
Libya licha ya vita na kutofanya mazoezi kutokana na vurugu lakini bado ngoma ngumu.
 
Back
Top Bottom