Taifa stars vs Mozambique.

Taifa stars vs Mozambique.

Tulishazoea!! Acha vijana warudi, next time tutajifunza zaidi!!

mkuu kama ni kujifunza basi tungekua hata kwenye top50 kwenye rank ya dunia,tutafute kitu kingine cha kufanya tu tunashiriki na sio kushindana
 
Hakuna cha kupigana kiume hapo,waliopigana kiume ni walioshinda.Anyway hayo ndo moja ya matokeo ya mpira.Kufungwa,suluhu,sare au kufunga.
Tujipange tugange yajayo.
 
duh! Nilikuwa namuita muhudumu sasaaaaaa!? Naend home kichwa chini! Na kubet nimekosa duh!
 
kiume ndo nini sasa, huo ndo upumbavu wetu watanzania gutimu gumefungwa unasifia eti walipigana kiume,. Tulivo mazezeta tutaenda kulipokea litimu bovu limetolewa uwanja wa ndege,.
hahahahaaah!! Hii Ya wapi hapo kwenye bluu??
 
Ko wamepigwa 8, nae kaseja kwa kufungwa nyingi sjui anamatatizo gani
 
kiume ndo nini sasa, huo ndo upumbavu wetu watanzania gutimu gumefungwa unasifia eti walipigana kiume,. Tulivo mazezeta tutaenda kulipokea litimu bovu limetolewa uwanja wa ndege,.

Mtazamu wako si sawa ndugu yangu.Uzalendo hautoweki mara baada ya kufungwa.Usipomtia moyo mwanao usitegemee kesho atajitahidi kufanye vizuri zaidi ya jana.Inafaa sana kutiana moyo ili kujitoa kwenye shimo la kufungwa kila siku.
 
mkuu kama ni kujifunza basi tungekua hata kwenye top50 kwenye rank ya dunia,tutafute kitu kingine cha kufanya tu tunashiriki na sio kushindana
Mkuu ninahasira hapa acha tu, niliamua kuandika hivyo kuhofia ban!! Timu haifanyi maandalizi ya kutosha, hapo hapo inajaza wavuta bangi, ukiangalia msingi wa soka nchini unakosa wapi/vipi tunatengeza vipaji vya kuweza kushindana. Hatuna viongozi wabunifu, tunao viongozi wanaoongoza kwa kuiga, mazoea na kutaka kujitajirisha bila kujali wananchi kupitia viingilio wanatutengenezea maradhi na kutupunguzia siku za kuishi.
Hili la kutolewa kila mashindano imeshakuwa jadi, system nzima ya nchi yetu inahitaji Total overhaul kuanzia magogoni hadi kwa mwenyekiti wa mtaa. Nasema hivyo kwa sababu M'kiti wa mtaa wanajua wananchi wanaokaa nao, hivyo hata viwanja vya kufanyia mazoezi wanapiga bei, hivyo hivyo pale magogoni kama mzee mzima anapenda mchezo wa soka, anashindwa nini kusema nahitaji kuona mwezi mmoja kwa mwaka kwa ajili ya michezo, inawezekana hizo week nne zikagawanywa kila miezi mitatu mashindano yafanyike kwenye shule na kuna watu wameajiriwa, hakuna gharama za kuendesha ni amri tu.
 
duh! Nilikuwa namuita muhudumu sasaaaaaa!? Naend home kichwa chini! Na kubet nimekosa duh!
Mkuu, achana na mpira wa Bongo!....mpira wa Bongo ni presure tu! usipoangalia utapata ugonjwa wa moyo.
Tanzania hatuwezi soccer ya kimataifa na haitakuja kutokea....labda baada ya miaka 500. FULL STOP...Utaki unaacha
 
Back
Top Bottom