Mkuu ninahasira hapa acha tu, niliamua kuandika hivyo kuhofia ban!! Timu haifanyi maandalizi ya kutosha, hapo hapo inajaza wavuta bangi, ukiangalia msingi wa soka nchini unakosa wapi/vipi tunatengeza vipaji vya kuweza kushindana. Hatuna viongozi wabunifu, tunao viongozi wanaoongoza kwa kuiga, mazoea na kutaka kujitajirisha bila kujali wananchi kupitia viingilio wanatutengenezea maradhi na kutupunguzia siku za kuishi.
Hili la kutolewa kila mashindano imeshakuwa jadi, system nzima ya nchi yetu inahitaji Total overhaul kuanzia magogoni hadi kwa mwenyekiti wa mtaa. Nasema hivyo kwa sababu M'kiti wa mtaa wanajua wananchi wanaokaa nao, hivyo hata viwanja vya kufanyia mazoezi wanapiga bei, hivyo hivyo pale magogoni kama mzee mzima anapenda mchezo wa soka, anashindwa nini kusema nahitaji kuona mwezi mmoja kwa mwaka kwa ajili ya michezo, inawezekana hizo week nne zikagawanywa kila miezi mitatu mashindano yafanyike kwenye shule na kuna watu wameajiriwa, hakuna gharama za kuendesha ni amri tu.