Mi naona tatizo ni wachezaji,tutabadilisha makocha mpaka basi ila tusipobadili system nzima ya mpira wetu hatutafika popote!
Huwezi kua na wachezaji ambao wanafanya mazoezi kwenye viwanja vibovu kabisa,hawana diet ya kimichezo ila ni kula chips mitaani, hawana ari ya ushindi kwasababu wanajua hata wakishinda hawana maslahi ya kueleweka na vingine vingi!!
tatizo ni kocha,
Hana mfumo unao eleweka kachagua wachezaji yeye mwenyewe
anag'ang'ania wachezaji wa nje (soka la kulipwa)
Kocha mzuri utaona timu yake kipindi cha pili
lakini jana ameonyesha udhaifu mkubwa
Sisi waTz tunamchekea tu, watu wanaqualify na wanafukuza kocha......
tusiangalie matokeo tuangalie trend nzima, tunaelekea wapi?
Posho kwa Siku Taifa Stars..ni Elf 15.....mayb wapandishe Juzi...unategemea nini...mchezaji anaweza kuwa na ushindani Hapo?
Kocha mwenyewe muoga..eti anawatumia mapro zaidi...hahahaha...mapro gani hao wakati timu zao zinashuka daraja kila mwaka?..na wengi wao hawako First Eleveni katika hizo timu zao...
TFF nao wamekosa ubunifu..wako pale kama mazuzu...tu....Wadhamamini nao hawaoni hasara cjui...una market kitu ambacho hakileti Tija..
Kazi kupiga Picha Tu wakitoa zawadi...Kesho timu inafungwa watu hawanunii hiyo Bia yenyewe kwa hasira za kufungwa.....
naunga mkono kijana.
tatizo ni kocha,
Hana mfumo unao eleweka kachagua wachezaji yeye mwenyewe
anag'ang'ania wachezaji wa nje (soka la kulipwa)
Kocha mzuri utaona timu yake kipindi cha pili
lakini jana ameonyesha udhaifu mkubwa
Sisi waTz tunamchekea tu, watu wanaqualify na wanafukuza kocha......
tusiangalie matokeo tuangalie trend nzima, tunaelekea wapi?
great great idea kama vile ulishawahi kuwa kambin na hii timu, imagine hata traki suit unazoona wamevaa kambin wanapokonywa kambi ikiisha, unamfanyisha mazoez mchezaj asbh,mchana na jion humpii chochote umempotezea the whole day nina familia,natakiwa nilipe kodi ya nyumba bado mahitaji madogo.. HALAFU UNANIAMBIA NIWE NA MORALI NA TIMU YA TAIFA...THUBUTU WEWE... Tutaendelea kuwakilisha tu uwanjan lkn nawakikishien hatuendi popote wajen..nyie subirien tu muone..club inanigaramia vizur kuliko timu ya taifa sasa kwann nisijitoe kwny club kwa nguvu zote..samata,nizar wata prove hili...naumia nikiitumikia timu ya taifa lkn TFF watoi hata mia kunitibu ila kwny magezet wanabakia kuudanya umma tumemfanyia hiv kumbe uwongo mtupu...tunasikia ahad kibao za hela kwa wachezaji ila kaz nafanya mm viongoz wanagawa kiraiic ukijidai kuhoj mtovu wa nidhamu then unafukuzwa au kusimwamishwa kambin.. Jasho nitoe mie hela yangu kiongoz anaenda kununulia vogue kwan mie sipend kuwa nalo..hata iweje siwez kuitumikia kwa moyo wote stars kama mambo yataendelea kuwa hiv.. C u when u c me..
Vyote ulivyovitaja ni matatizo.
Taifa Stars kweli ni mahututi.Tatizo wote wawili...Kocha na Wachezaji
1.kocha....hana mbinu mbadala....mfumo wake haueleweki...
2.wachezaji...baadhi hawana sifa tena za kucheza stars...Mfano...Machupa..kafunga goli ngapi ligi ya huko swedeni?...na yuko Kikosi cha kwanza katika timu yake?
..Jiulize kuhusu vietnam ligi yao...Timu ya babi na Mrwanda ..inashuka daraja...je wanaisaidiaje timu zao?
Ukweli ni kwamba hatuna wachezaji wenye ushindani
CECAFA...wadau wa mpira tunajua ...nini kilifanyika kuchukua kombe lile..na sasa watu wamipango wana malumbano na TFF..tegemea Vichapo CECAFA...nitarudi baadae
Umenena mkuu.Binafsi nadhan tatizo sio wachezaji wala kocha, tatizo ni uongozi wa tff, wanajua kabisa Tanzania hatuna wachezaji wa kulipwa ambao unaweza kuwakusanya ndani ya siku tatu na wakazoeana, lakini TFF wataandaa kambi chini ya wiki moja unategemea timu kama hiyo itafanya vizuri, timu ikishinda mechi kibahati bahati itapelekwa bungeni au ikulu, juzi hapa tumeibahatisha Chad, badala ya timu kuondoka siku hiyo hiyo au kesho yake asubuhi kwa ajili ya mazoezi timu inarudi baada ya siku mbili na wanajua kabisa mechi ilikuwa karibu hivyo wakawa na siku moja ya mazoezi, lakini inashauriwa hutakiwi kuuchosha mwili kwa mazoezi makali siku moja kabla ya mechi, Chad wanakutangulia kufika kwenu halafu unategemea timu ishinde, tutawalaumu tu hawa vijana lakini wafanyeje viongozi wenu wanafikiria hela after all sisi ni wazuri kwenye nini kwa nini tuwalaumu footballers ambao kwanza hata hawajaandaliwa vizuri, mimi siwalaumu hata kidogo na nawapongeza kwa kufuzu hatua ya makundi, watu wako kambini wanapewa elfu 15, jiulize hela zote hizo zingine zinaenda wapi, lawama ziende wizara husika, baraza la michezo na Tenga na grupu lake hapo Ilala.
Kwa kweli hii Timu inatia kichefuchefu sana, timu imepoteza mvuto kabisa.Lawama ziwaendee makocha na wachezaji.Yaani haingii akilini huyu Mwalimu kuendelea kuwatumia akina Machupa na wenzie ambao wamechuja vibaya, hivi akina Kayuni ni maoni gani ya kiufundi mnayompa huyo babu? Au ndio bora liende tu? Kama hamuwezi Kazi jiondoeni. Mnatubore sana.