TAIFA STARS: Tatizo kocha au wachezaji? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TAIFA STARS: Tatizo kocha au wachezaji?

Discussion in 'Sports' started by Ulimakafu, Nov 16, 2011.

 1. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #1
  Nov 16, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Hii timu baada ya kuchukuliwa na babu Jan Poulsen imekuwa kama homa ya kipindi,tunashindwa hata na Chad nyumbani?Tatizo mi silielewi kama ni kocha,mfumo au wachezaji wanaounda kikosi hicho.
   
 2. c

  cheseo Member

  #2
  Nov 16, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 81
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Mi naona tatizo ni wachezaji,tutabadilisha makocha mpaka basi ila tusipobadili system nzima ya mpira wetu hatutafika popote!
  Huwezi kua na wachezaji ambao wanafanya mazoezi kwenye viwanja vibovu kabisa,hawana diet ya kimichezo ila ni kula chips mitaani, hawana ari ya ushindi kwasababu wanajua hata wakishinda hawana maslahi ya kueleweka na vingine vingi!!
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Nov 16, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kocha mgonjwa huyu bwana...hawezi kazi
   
 4. c

  cheseo Member

  #4
  Nov 16, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 81
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Kaka embu tuambiane hapa kocha gani tulishawahi kusema ameweza kazi? Nakumbuka paulsen alovyoshinda challenge tulisema kocha mzuri ila leo hafai
   
 5. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #5
  Nov 16, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  TAtizo ni ccm na Kikwete
   
 6. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #6
  Nov 16, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Kocha nae anachangia kwa kweli.
   
 7. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #7
  Nov 16, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Alibahatisha....
   
 8. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #8
  Nov 16, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,555
  Likes Received: 1,041
  Trophy Points: 280
  Si kweli. Alitumia matunda ya Marcio Maximo.
   
 9. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #9
  Nov 16, 2011
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,109
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  ushawahi kumtongozea mtu alafu aakaenda guest house na jimama likamshinda
  tatizo linakuwa kwa nani msaada pls??
   
 10. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #10
  Nov 16, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Tatizo ni wachezaji
   
 11. b

  babojga Member

  #11
  Nov 16, 2011
  Joined: Oct 24, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli taifa stars mimi siipendi kabisa, jana kuna shabiki mmoja wakati wa mapumziko radio free afrika alicomment akiitakia ushindi chad kwani aliona ni jinsi gani timu inavyocheza kwa kubahatisha, fukuzeni huyo babu poulsen, hana faida kwa timu yetu, tunategemea nini tukijapambana ivory coast au morocco kwa timu mavi kama hii?
   
 12. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #12
  Nov 16, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Nimeipenda hii mkuu.
   
 13. mtu chake

  mtu chake JF-Expert Member

  #13
  Nov 16, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 4,090
  Likes Received: 1,262
  Trophy Points: 280
  Tatizo wote wawili...Kocha na Wachezaji
  1.kocha....hana mbinu mbadala....mfumo wake haueleweki...
  2.wachezaji...baadhi hawana sifa tena za kucheza stars...Mfano...Machupa..kafunga goli ngapi ligi ya huko swedeni?...na yuko Kikosi cha kwanza katika timu yake?
  ..Jiulize kuhusu vietnam ligi yao...Timu ya babi na Mrwanda ..inashuka daraja...je wanaisaidiaje timu zao?

  Ukweli ni kwamba hatuna wachezaji wenye ushindani

  CECAFA...wadau wa mpira tunajua ...nini kilifanyika kuchukua kombe lile..na sasa watu wamipango wana malumbano na TFF..tegemea Vichapo CECAFA...nitarudi baadae
   
 14. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #14
  Nov 16, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,328
  Likes Received: 22,172
  Trophy Points: 280
  Timu gani ambayo haichezi mechi za kimataifa? Inaingia kambini wiki moja kabla ya mechi? Piga chini Tenga, kisha tuitishe uchaguzi mpyaa
   
 15. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #15
  Nov 16, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mimi sasa hivi namkumbuka maximo sana... alikuwa anawajengea hari wachezaji na alikuwa amsimamo!
   
 16. Aleyn

  Aleyn JF-Expert Member

  #16
  Nov 16, 2011
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 10,228
  Likes Received: 13,680
  Trophy Points: 280
  Makocha huwa wanazeekea Kwenye Timu sasa huyo Poulsen ndo kwanza anafundisha timu kubwa bora aende kwao tatizo ni Makocha wa Bei Rahisi.
   
 17. Lonestriker

  Lonestriker JF-Expert Member

  #17
  Nov 16, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 641
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kabla ya kumponda kocha tujiulize tulishafanya nini kimataifa?CECAFA mara 2,CAF mara 1.Simba na Yanga wamefanya nini kimataifa?Je kuna mchezaji hata mmoja wa Kitanzania aliyewahi kung'aa kwenye ligi ngumu?
  Hatuna mfumo wa soka,hatuna viongozi makini.Vimashindano vya vijana ni utani mtupu.
  Ok,tunasema kocha wa bei rahisi,kocha gani wa kiwango cha juu atakuja kuharibu Cv yake hapa,Maximo ametoka hapa amekosa timu kabisa kwa sababu hakufanya lolote.
  Hao wazawa wanaolilia kupewa timu wamefanya nini?Kama hawawezi hata kuvuka mipaka na kufundisha klabu za CECAFA Watawezaje Taifa stars?Kwanza wakasome,wengi wao hata leseni A za CAF hawana.
   
 18. mtu chake

  mtu chake JF-Expert Member

  #18
  Nov 16, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 4,090
  Likes Received: 1,262
  Trophy Points: 280
  Pale TFF hakuna Mipango...Si Tenga wala Kayuni ambaye ndiye Mkurungenzi wa Ufundi..wamekaa kusuburi Posho na makato ya mechi...
  Mipango duni...timu inakosa Tiketi ya kwenda sudani kucheza Friend match...unategemea nn...

  Wanashindwa kulea watoto wale wa TSA......Vipi serengeti boys.wapi Ngorongoro Heroes...

  Nina Hasira sana....Mbaya zaidi tukiwaambia wanasema majungu...
   
 19. s

  smp143 Member

  #19
  Nov 16, 2011
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mfumo nzima ni mbovu kabisa.kocha na wachezaji wabebeshwe lawama.Yaani ile mechi ya jana tumeshindwa kushinda.
  Babu Poulsen hana uwezo wa kufundisha national team.TFF kina Tenga hawajali national team wanaangalia vitambi vyao tuu.
  Kinachotakiwa sasa ni kufungisha virago Poulsen, Team apewe kocha anayejua soka ya Afrika mwenye mafanikio.Team apewe Patrick Phiri
  Ambae anwajua wachezaji wa bongo and has a lot of experience with African foootball.

  Kocha aje immedietly, aandae program mapema,achukue wachezaji wenye vipaji na achane na akina machupa,and wachezaji wazee.
  Tujenge team mapema around kina Shomari kapombe,nyooso,and other proffesional players.Serengeti wanamwaga pesa kila mtu anataka kufaidika.hiyo kundi tuliyopangwa
  Tunaenda kama wasindikizaji..ahh
   
 20. mtu chake

  mtu chake JF-Expert Member

  #20
  Nov 16, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 4,090
  Likes Received: 1,262
  Trophy Points: 280
  ki Ukweli sisi hatuna Kiu ya soka....Kipindi fulani nilikua na Tinoco pale TFF...kwa maoni yake..anasema Uongozi haulewei na ndio maana akamua kuondoka...lkn akamwambia Kayuni..hakikisha hawa watoto wa COpa Cocacola ambao nimeenda nao Brazili..na wakashinda...na Pia South Africa...

  Wachomekeni kwenye Timu za wakubwa ..pia wapewe nafasi..yaani iwe kama Sheria ndogo vile kwamba kila timu isajiri Under 18..wawe nao..na wawe wanapangwa..kuwapa Uzoefu..mpk sasa tungewa na Timu nzuri..matokeoa yake Ndio...haya sasa AIBUU

  Si Yanga wala Simba..ambao wana KIU ya mafanikio...angalia usajiri wao...tazama Maandalizi yao....
  Azam nao wameingia kwenye Mkumbo huo wa kutaka ubingwa wa haraka haraka...wamesajiri wachezaji wakigeni wote Maboya Tu....
  .....Nitarudi Tena
   
Loading...