TAIFA STARS ni Siasa pia

TAIFA STARS ni Siasa pia

Acha utani.Kodi za watu zimeliwa we unaleta utani.Kufungwa ndo kujitahidi gani huko na kocha mnaye expert?Haya mambo ya kujenga ghorofa hewani.Sawa na mambo yenu ya fly overs.
Mangi........Haujamuelewa Katavi.......Anamaanisha kwamba tumejitahidi kupunguza idadi ya magoli......Tungeweza kufungwa hata 10 kwa kiwango kibovu tulichonacho...Maximo ni bora sana kuliko hiki kibabu Poulsen......Alikuwa na uwezo wa kuwajenga wachezaji kisaikolojia na kuwa na morali ya kushinda hata wakiwa ugenini....Bado tunayo safari ndefu sana na hakika tumerudi nyuma sana kihatua ukilinganisha na enzi za Maximo....
 
Timu yetu ya mpira imekuwa kama migodi na madini yetu. Tumewatafuta wawekezaji (Maximo na sasa Paulsen) wametafuna kodi za Watanzania, matokeo yake ni kukung'utwa karibu kila mechi.

Kichekesho ni kwamba Kabla ya Maximo kwenye viwango vya FIFA Tanzania ilikuwa inashikilia nafasi ya 115. Miaka 5 chini ya wawekezaji tunashikilia leo nafasi ya 127 !!! Kama huamini angalia hapa FIFA.com - Classement mondial FIFA/Coca-Cola
 
Tatizo hatuna mipango, unapeleka timu iliyozimamoto kwa kuweka kambi ya siku 3 bila hata mechi za kirafiki halafu unataka ishinde!
 
Acha utani.Kodi za watu zimeliwa we unaleta utani.Kufungwa ndo kujitahidi gani huko na kocha mnaye expert?Haya mambo ya kujenga ghorofa hewani.Sawa na mambo yenu ya fly overs.

Tulitegemea kufungwa mengi zaidi ya hayo...
 
Tatizo hatuna mipango, unapeleka timu iliyozimamoto kwa kuweka kambi ya siku 3 bila hata mechi za kirafiki halafu unataka ishinde!

Kamura nakubaliana na wewe. Kila siku tupo kwenye mipango ya Zima mote.

By the way, timu yetu hii inafanana na JK mwenyewe. Je ni mradi upi alioanzisha tangu ameingia Ikulu ukafanikiwa ?
Kumfukuza tu Kocha haitoshi, Kikwete naye anapaswa awe wa kwanza kufukuzwa kazi. Wote hawa ni janga la Taifa kwani wanakula tu bure kodi za wananchi bila kutuletea maendeleo yoyote !
 
Back
Top Bottom