Taifa likiingia vitani leo,Itakuwaje?

nyie si mnasema Tanzania ni nchi ya Amani
amani yenyewe haipo zaidi ya viini macho
siombei vita mungu aepushe mbali cause tutakaoumia ni sisi wananchi wenye hali ya chini

Watu wanashindwa kutofautisha Amani na Ujinga!
Tanzania hakuna Amani bali Ujinga
 
Wanajeshi hawana cha kupigania'hawana noble cause". Utajitoa mhanga kupoteza maisha ili Riz aishi vizuri zaidi, nani yupo tayari?
 
Hadi Malawi sasa wameshagundua udhaifu wa serikali yetu muda wowote watatutandika.
 
hao malawi waache waje kichwa kichwa tutawapiga na dodoki wakafie mbali...!! nia tunayo moyo hatuna..
 
DHAIFU atatoa kauli kwamba "Serikali haina uwezo" wa kuingia vitani.

Yaani kama umesoma akili zangu. Chini ya Dhaifu Malawi watachukua Tukuyu, Songea, Rungwe, Mbeya na kuchora mpaka mpya.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Askari waliopigana vita vya KAGERA wengi wako hoi bin taaban serikari imewatelekeza bila support kitendo hicho kinaitia doa kwa askari waliopo maana wanawaona hali zao zikiwa taabani kiuchumi wengine wamekuwa walinzi kwenye maduka ya wahindi shame on you JWTZ.
 
Yaani kama umesoma akili zangu. Chini ya Dhaifu Malawi watachukua Tukuyu, Songea, Rungwe, Mbeya na kuchora mpaka mpya.

Nyakati kama hizi unamkumba yule Mzee wa shoka ambaye hakukubali hata siku moja Tanzania ichezewe kwa namna yoyote ile na nyang'au/nduli yeyote yule duniani. RIP Mwalimu.
 
Nimejiuliza sana swali hili bila majibu. Nisaidieni.

Mwaka 1978 tuliingia vitani na Uganda chini ya Idd Amin, lakini tulipambana kama Taifa vita ile kwa pamoja yaani viongozi wetu, makamanda, askari, Taasisi mbalimbali na Raia wote hadi tukashinda.

Sasa hivi hatuna tena maelewano ya aina ile. Tunachokiona ni uhasama kati Bunge na Serikali, Serikali na Raia wake, Taasisi na Taasisi na hata Askari na Raia. Ufisadi umeshika kasi ndani ya Taasisi muhimu za Umma kiasi kufikia kununua vifaa vya kijeshi vinavyodhaniwa kuwa viko chini ya kiwango (fake) hasa tukikumbuka vitu kama Helicopter zinazoanguka hovyo na mabomu yanayolipuka hovyo.

Jee kwa hali kama hiyo, ikitokea nchi jirani kushambulia mipaka yetu tunao uwezo wa kuhimili mapigo kama ule wa mwaka 1978 kama Taifa? Ama tutaita wawekezaji wa kijeshi kutulindia mipaka yetu huku sisi tukiendelea kupiga soga la malumbano?

MUNGU AEPUSHE tusiwe na mgogoro na nchi jirani utakaofikia vita! Kwa MTAWANYIKO wa KIUTAIFA unaotukabiri; tutadundwa kama MBWA MWIZI!

Wapiganaji wetu wanaweza kuwa bado ba UTAIFA MWINGI TUU; bahati mbaya wakikumbuka story ya MABILIONI ya Shimbo; akikutana na mazingira ya AFE KUTULINDA hakawii kudai RISK ALLOWANCE yake kabla hajamkabiri ADUI!

Kwa ufupi katika hali ya sasa hivi hata vita ya ndani hatuiwezi!
 
Kwa jinsi wananchi walio wengi walivyokata tamaa lazima watatoa ushirikiano kwa hao wavamizi. Hii haina tofauti na jinsi wapiganaji wetu walivyopata ushirikiano kutoka kwa wananchi wa iliyokuwa uganda ya iddi amini.

Watu kama walimu madaktari n.k unategemea watakua upande upi? Lazima wasaidie maadui ilikuwaondoa mafisadi.

Hata hivyo wanaofaidi nchi hii si mafisadi wananchi wa kawaida wana nini chakupoteza hapa? Bora tupigwe mafisadi wakimbie halafu watakao salimika waanze upya, hapo ndipo heshima na utu vitarudi.
 
kama tukivamiwa UGOMVI wetu pembeni silaha begani twende kazi ila tukitoka huko kishujaa basi mafisadi na wengine tutajuana nao lakini maslahi ya Taifa mbele kwanza.
 
mimi nitakuwa na ombi JF iwe hewani muda wote wa vita .. ikiwezekana wengine wajitolee mstari wa mbele kutumwagia updates .. hahaha!

AstaghafirAllah! .. Mwenyezimungu aepushie mbali hivi vita.. wakae mezani waelewane
 
Jamani kuna siku nshawahi kuwaskia ccm eti ile vita ya mwaka 78 mpaka leo ndio mana uchumi wetu umedumaa sasa kama leo tukipigana si itachukua miaka mia kutengemaa
 
Mimi naona nalaumu kwanini wamalawi mpk saiv hawajaanza kushusha makombora na nitakua wa mwanzo kuwaonyesha maadui zao. mimi nipo hapa mpakani na ikianza tutaingia mpk magogoni. kila mmoja atamuheshimu mwenzake viburi va viongozi wetu imevuka mipaka wanajiona kama wao tu ndio wameletwa kugaiana madaraka.
 
kama tukivamiwa UGOMVI wetu pembeni silaha begani twende kazi ila tukitoka huko kishujaa basi mafisadi na wengine tutajuana nao lakini maslahi ya Taifa mbele kwanza.

Vipi wewe, tuna maslahi ya taifa au ya mafisadi na wapambe wao wachache, unajua sikuelewi au na wewe fisaidi, mpambe wa fisadi nini.
 
nyie si mnasema Tanzania ni nchi ya Amani
amani yenyewe haipo zaidi ya viini macho
siombei vita mungu aepushe mbali cause tutakaoumia ni sisi wananchi wenye hali ya chini

Bibi kwanza muumie mara ngapi? si mnaendelea kuumia itakuwa ni muendelezo wa maumivu ambao pengine utaweza kusaidia kuwaondoa wanao sababisha haya maumivu.
 
Back
Top Bottom