Taifa likiingia vitani leo,Itakuwaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taifa likiingia vitani leo,Itakuwaje?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chakaza, Oct 30, 2009.

 1. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,663
  Likes Received: 21,886
  Trophy Points: 280
  Nimejiuliza sana swali hili bila majibu. Nisaidieni.

  Mwaka 1978 tuliingia vitani na Uganda chini ya Idd Amin, lakini tulipambana kama Taifa vita ile kwa pamoja yaani viongozi wetu, makamanda, askari, Taasisi mbalimbali na Raia wote hadi tukashinda.

  Sasa hivi hatuna tena maelewano ya aina ile. Tunachokiona ni uhasama kati Bunge na Serikali, Serikali na Raia wake, Taasisi na Taasisi na hata Askari na Raia. Ufisadi umeshika kasi ndani ya Taasisi muhimu za Umma kiasi kufikia kununua vifaa vya kijeshi vinavyodhaniwa kuwa viko chini ya kiwango (fake) hasa tukikumbuka vitu kama Helicopter zinazoanguka hovyo na mabomu yanayolipuka hovyo.

  Jee kwa hali kama hiyo, ikitokea nchi jirani kushambulia mipaka yetu tunao uwezo wa kuhimili mapigo kama ule wa mwaka 1978 kama Taifa? Ama tutaita wawekezaji wa kijeshi kutulindia mipaka yetu huku sisi tukiendelea kupiga soga la malumbano?
   
 2. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2009
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  nikipigo tu hapo, mafisadi watakwenda zao kula raha ugaibuni
   
 3. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,663
  Likes Received: 21,886
  Trophy Points: 280
  Mkuu kama tunajua hali ni hiyo,jee tukae tukilumbana na kusubiri hicho kipigo?
   
 4. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nikikumbuka ile vita ya Idi Amini..

  Mola inusuru Tanzania na vita. Tuache kwanza mmalize hiyo vita ya UFISADI
   
 5. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2009
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hapana kusubiri kitu cha kwanza ni kuiondoa ccm madarakani, baada ya hapo kufuta mikataba mibovu yote na kuwachukulia hatua wahujumu wote na kutaifisha mali zao, hapa kutakuwepo namshikamano wa kitaifa.
   
 6. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  yote haya unayoyaona ni mmeng'enyo tu toward a better Tanzania. itafikia kipindi watu wabaya watakuwa wamechujwa, ubaya utakuwa umechujwa etc. vita ni mbaya sana, na viongozi wanatakiwa wajitahidi kuondoa dukuduku mioyoni mwa watu, kwasababu kama mioyo ina machungu kila wakati, vijana wetu wanakuwa rahisi kushawishika hata kurusha jiwe ili hasira yao iishie hapo tu. jinsi mafisadi, kina kikwete na utawala wake wanavyozidi kufanya watz kama hawaelewi mambo, ndivyo watu wanavyoendelea kuishi na madukuduku mioyoni. ole.
   
 7. Nyasirori

  Nyasirori Senior Member

  #7
  Oct 30, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 183
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Kweli ni kipondo tu tutakachoambulia. Hata makamanda wengi wanaotakiwa waongoze vita hiyo ni watoto wa hao mafisadi ambao pamoja na umri mdogo ni Ma-Captain, Major.Hawa hawajawahi kusikia hata mlio wa bomu vitani (Labda kama walisikia ile milio ya mabomu ya mbagala). Wakipewa kuongoza vita, wakasikia mabomu yanalipuka, asubuhi tutaambulia uniform zao na wao hawatajulikana walipo. Watakimbia na baba zao ughaibuni.
   
 8. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,663
  Likes Received: 21,886
  Trophy Points: 280
  Tumeona mahusiano yalivyo kati ya vyombo vya ulinzi na usalama na Raia. Matukio ya Askari kupiga raia wasio na hatia (kama JWTZ na JKT) halafu hakuna hatua za dhati zinazochukuliwa dhidi yao au kurudisha maelewano. Kama vile hakuna anayejali kuwa watafanya nini hao Raia wanyonge. Polisi nayo ndio usiseme katika kubambika kesi kwa uonevu. Vita vinapotokea Askari wanahitaji support kubwa toka kwa Raia ili kutekeleza majukumu yao. Nina mashaka kuwa kwa hali hii Raia bado wataendelea kuwaona Askari kama nao ni adui vilevile.
   
 9. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #9
  Nov 6, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,663
  Likes Received: 21,886
  Trophy Points: 280
  Vita ya ufisadi itaishaje wakati viongozi muhimu kama Waziri anayeshughulikia usalama wa Taifa Anasimama kibwebwe kutoa mipasho na ngebe kutetea ufisadi huko Dodoma? Hujamsikia Sophia? Usalama wa nchi hii uko mashakani. Hilo tulijue kabisa
   
 10. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #10
  Nov 6, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Mungu apishilie mbali kama mita bilioni 1000 hivi!
   
 11. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #11
  Nov 6, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  nyie si mnasema Tanzania ni nchi ya Amani
  amani yenyewe haipo zaidi ya viini macho
  siombei vita mungu aepushe mbali cause tutakaoumia ni sisi wananchi wenye hali ya chini
   
 12. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #12
  Nov 6, 2009
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ahhh!! Hapa Kichapo kwa kwenda Mbele kwani mafisadi wameshajenga New Jesey
   
 13. M

  Mchili JF-Expert Member

  #13
  Nov 6, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Zungumza taratibu wasitusikie. Ka nchi kama Rwanda kanawezaamua kupanua mipaka yake wakigundua huu udhaifu tulio nao.

  Tufanye nini? Tuiondoe kwanza ccm mwakani tujipange upya. Mungu saidia.
   
 14. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #14
  Apr 24, 2012
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,663
  Likes Received: 21,886
  Trophy Points: 280
  Bado swali hili najiuliza hadi leo na jibu sijapata.
   
 15. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #15
  Aug 3, 2012
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,663
  Likes Received: 21,886
  Trophy Points: 280
  Swali linazidi kuchukua nafasi hasa baada ya kusikia chokochoko za Malawi kwa mipaka yetu. Maana tukilemaa kesho tutasikia Rwanda anaitaka Ngara,Burundi anataka Kibondo na Kenya anautaka mlima Kilimanjaro.
  Jee tuko tayari kujilinda au tumebaki na blabla?
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,670
  Likes Received: 82,493
  Trophy Points: 280
  DHAIFU atatoa kauli kwamba "Serikali haina uwezo" wa kuingia vitani.

   
 17. Maarko

  Maarko JF-Expert Member

  #17
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,030
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Hakuna tunacho kiweza kwa sasa،tukiingia vitani ka nchi kama Rwanda katatuchapa mpaka tutashangaa,sehemu ku wa ya jeshi letu waliingizwa kindugu،kama ilivyo kitengo cha usalama wa taifa،zamani ilikua ili ujiunge na usalama wa taifa utachunguzwa hadi kwenu bila wewe kujua،sasa hivi wanaajiriwa kwa kimemo,mtoto wa dada،kaka binamu,
   
 18. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #18
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Sasa hivi atatukipigana na Somalia isiyo na serekali tutapigwa tuu ije kuwa Malawi nchi yeye uchumi mzuri? Nasema ivo sababu
  1. Hazina imekauka wamebakiza coins tuu
  2. Silaha zetu zime expire Ndio maana zinalipuka zenyewe
  3. Watu wamechoka na serikali sababu zinazopelekea umoja wetu kufifia.
  4. Muingereza Ndio atakuwa supporter namba moja wa Malawi.
  5. Wanajeshi wetu wamejenga vitambi badala ya uzalendo jazia apo
  6.
  7.
  8.
  9.
  10.
   
 19. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #19
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Yaani serikali haitapata support hata moja toka kwa watanzania walio mijini...labda wakawadanganye wa vijijini wawape ng'ombe acha tupigwe na tuporwe kila kitu chetu upuuzi mtupu!!hakuna uzalendo!!!
   
 20. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #20
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,455
  Trophy Points: 280
  Vita ni vita, chochote chaweza kutokea.

  Kwangu mimi vita kati ya nchi na nchi ni rahisi kuwa-mobilize watu wako lakini vita ya ndani (civil war) ni mbaya sana.

  Kama hali itaendelea kuwa mbaya kama ilivyo sasa; ugumu wa maisha, uchumi mbovu, kukithiri kwa ufisadi, dhuluma na manyanyaso ya wawekezaji kwa raia wa Tz, Mahakama kutokuwa chombo cha haki, Polisi kuendelea na ukiukwaji wa haki za kibinadamu, ombwe la uongozi, serikali dhaifu na yenye kukumbatia wenye nacho na kpuuza wasio nacho nk nk then tunachoogopa kinaweza kutokea.

  Ndio maana ni lazima tufanye kazi kubwa na kwa bidii sana muda huu ili kuinusuru nchi hii na majanga yajayo kama vita au kuwa failed state.
   
Loading...