mekuoko

JF-Expert Member
Nov 15, 2012
418
365
Speech Mh. Samia Suluhu Hassan jana akihojiwa na Kikeke wa BBC naona imeligawa taifa. Kwamba tabaka la watawala na Watawaliwa.

Na kwamba ukishaazishwa uongo basi unasimamiwa na wote ili kulinda madaraka.

Kundi hili la watawala wanawatoza watawaliwa wanyonge makodi makubwa bila kujali kama hawa watu wanaowatoza waana uwezo au la.

Narudi nyuma sana na kuona ni heri kodi za wakoloni kwani walizingatia mtu alichonacho kuliko hawa wanatutoza kwa uwiano mmoja na wenyewe wakiendelea kuneemeka.

Madarakani na ndugu zao. Mfano ni awamu ya 5 kutaka kuigeuza kijiji cha Chato kuwa Jiji kwa utawala wa miaka 10 ila Mungu lakataa.

Watawala wa Tanzania ni genge la watu wachache, wanoishi na familia zao kwa kuwatoza wananchi kodi/tozo lukuki za miamala ya simu na mabank, kodi za bidhaa, mafufa, umeme, nyumba, ardhi, mazao, material za ujenzi kama mchanga, mawe, udongo, mbao fito, kodi ya maji, kodi ya kulima shamba, ukilipa ada unalipia na kodi hiyo ada etc.

Ila mama jana kasema wanaoulizia Katiba wanaleta siasa za fujo na ni Magaidi na iachwe mahakama iamue.

Mungu yupo, Hawa watu watawala ikiwa ni pamoja na mh. SSH, wao kila kitu wanaishi kwa hizo kodi wanazotutoza, nyumba, malazi, chakula, usafiri mzuri na wa kisasa, vinywaji, mawasiliano, usafi wa nyumba, mazingira ya nyumbani, elimu zao na familia zao kwa kifupi kila kitu wanagharimikiwa na kodi kubwa wanazotutoza kwa kila kitu, wamebakisha tu kututoza tukipumua.

Mungu tuepishe na janga hili la utawala kandamizi, onevu, dhulumati etc.

Mungu hujibu maombi.
 
Yote hayo ni kwa sababu mbowe amekamatwa, Chadema mnamuona kiongozi wenu kama Mungu.
 
Anaapishwa Rais Samia ndani ya mwezi humu ukaletwa uzi wa kumshukuru kwa kushusha kodi ya manunuzi ya magari.

Ukaja uzi wa kumshukuru kuwaachia mashehe wa uamsho.

Ukaja uzi wa kusema amelenga kuleta maridhiano, maridhiano yakaja na Nyagali kuachiwa na kesi zaidi ya 100 kufutwa. Biswalo akawa hakimu, Kakurwa na Polepole wabunge wa kuteuliwa. Herry James akaomba msamaha hadharani na akateuliwa kua D.C

Kisha chadema wakaweka kongamano la kujadili katiba, vitisho vikaanza wakiwa hapo kwenye kongamano. Lisu anasisitiza atendewe kama kesi maalumu ila na vitisho vikahusika.

Alivyosikia juu ya katiba mpya akasema isubiriwe kidogo tuweke sawa uchumi. Bwana wee huko kushambuliwa kulipoanzia!!? Wengi hoja yetu ilikua hivi "Ameonyesha anaelekea uelekeo sahihi, kwanini isitumike njia ya majadiliano kuliko vitisho kama hivi?"

Wakajibu hapana haki haiombwi hapa ni kwenda naye kibabe.

Well, a week later Mbowe yuko ndani. Nyagali wa viwembe is nowhere to be seen. Waliosema mwendo unaotakiwa ni wa kibabe wanaandika nyuzi kumuomba Rais aingilie kati hili swala.

Common sense is not so common.

Wako busy kusema "Hata Mandela alifungwa gerezani" ni kweli alifungwa lakini approach yake towards ending apartheid ilikuaje?

Unafikiri Nyerere angeshindwa kutishia waingereza considering hata yeye aliungwa mkono na wengi?

Once nilijadiliana na member mmoja humu.

Hoja yake ni ccm kutuchelewesha kiuchumi wakati nchi kama Malaysia na Thailand tuliwahi kua nao sawa kiuchumi.

Nikamuuliza unajua Malaysia na Thailand zilipaa kiuchumi wakiwa chini ya udikteta? And people died maelfu kwa maelfu? Akawa kimya coz he didn't knew ila ndiyo hoja anazotumia.

Nimechelewa ila angalau nimejifunza kwamba wachangia hoja za siasa wengi hua wanakuja kusutana ndiyo maana mtu hata ukimuandikia kitu cha kawaida cha kutumia akili anakujibu 'Tutakutana barabarani'

And then kesho anatuma picha za wenzake wakiwa wapi barabarani huku yeye yupo nyuma ya keyboard.
 
Back
Top Bottom