SoC02 Taifa huru gizani

Stories of Change - 2022 Competition

Sun Nicklaus IX

New Member
Mar 23, 2020
2
0
TAIFA HURU GIZANI (TANZANIA)

tmp-cam-6706451353479779981.jpg

Chanzo cha picha: Vectorstock.

Taifa ni jumla ya watu wanaojitambulisha na eneo, lugha, rangi na mila, kwa ujumla ni nchi.

Neno taifa linatokana na Kilatini natutio likimaanisha kuzaliwa, watu (kwa maana ya kikabila), spishi au darasa.

Taifa lina sifa ya kitamaduni, kijamii, kihistoria na kitambulisho cha kisiasa cha watu. Kwa maana hii, hisia za taifa zinaweza kuelezewa kama maoni ya kikundi cha watu ambao hushirikiana na marafiki ambao wanawatambua kitamaduni.

Hivyo basi Kuna mataifa takribani 200 ulimwenguni kwa sasa japokuwa Umoja wa Mataifa unatambua mataifa rasmi kuwa ni 196. Tanzania likiwa miongoni wa Mataifa haya kutokea bara la Afrika, ni miongoni mwa taifa lililopitia madhira ya ukoloni na ubeberu wa Mataifa ya magharibi kama vile Ujerumani na Uingereza.

Pamoja na masaibu ya kutawaliwa katika kila nyanja kwa taifa hili lenye rasilimali za kutosha mnamo tarehe 09 Desemba 1961, Tanzania ilikuwa huru kutoka kwenye makucha ya utawala dharimu wa kiingereza uliongozwa na Malkia Elizabeth II, akisaidiwa na Gavana Richard Turnbull aliyekuwa mtawala wa koloni la Tanganyika.

Chini ya uongozi na harakati za kudai uhuru zilizoongozwa na hayati baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere na viongozi wengine wa chama Cha kisiasa Tanganyika African National Union (TANU) uhuru ulipatikana, ambapo mwaka 1977 kilizalishwa chama kipya baada ya muungano wa vyama viwili TANU kutoka Tanganyika na Afro Shiraz Party (ASP) kutoka Zanzibar na rasmi iliundwa CCM kikimaanisha Chama Cha Mapinduzi. Hivyo kwa ufupi hiyo ndiyo historian ya ukombozi wa awali wa taifa la Tanzania kupata uhuru wake wa bendera na kisiasa.

Licha ya taifa hili mashuhuri barani Afrika na duniani kutoka na historia yake pamoja na vivutio vya kitalii vinavyopatikana hapa na kufanya taifa hili kuwa maarufu sana duniani kote lakini bado ni miongoni mwa Mataifa tegemezi na maskini sana ulimwenguni licha ya kuwa na utulivu wa kisiasa na amani takribani wakati wote wa uhuru wake unaofikia miaka sitini kwa sasa Hali hii imekuwa ikiwafedhehesha wananchi na viongozi katika ngazi na kada zote huku kila mmoja akimrushia mpira mwenzie kukwepa lawama zinazopelekea Tanzania kubaki katika lindi kubwa la ukata na utegemezi

Hali hii inanipa uthubutu wa kusema ni kweli kuwa Tanzania ni taifa huru lakini lililopo katika kiza kinene kisababishwacho na vichocheo vya ndani na nje, hivyo basi taifa hili linahitaji mikakati madhubuti na mtambuka katika kila nyanja na sekta pamoja na mageuzi yenye tija kwa kizazi cha Leo na kesho ili matokeo chanya yaweze kujidhihirisha thabiti na kwa uhakika mkubwa zaidi.

Tukijifunza kupitia historia na uzoefu tutagundua kuwa yapo mataifa yaliyojinasua na kutoka katika hali ya umaskini na utegemezi na kuwa na chumi zilizoimarika na kustawi sana na hata kufika hatu ya kuanza kutoa misaada mbalimbali kwa mataifa mengine, mfano mzuri ni Jamhuri ya watu wa Uchina, Korea ya kusini, Malaya, Vietnam, Taiwan na Indonesia haya ni mataifa yanayodhihirisha ya kwamba kama taifa litaadhimia kufanya mageuzi nakuja na sera tajika kwa maendeleo ya taifa hakika litafanikiwa kupiga hatua ya kuwa taifa huru kwenye nuru inayong'aa.

Nini sasa cha kufanya kama taifa la Tanzania ilituweze kupiga hatua za maendeleo chanya katika kila nyanja ya kimaisha?

Mosi ni lazima taifa na viongozi wake watambue nguvu kubwa waliyokuwa nayo vijana katika kuchagiza maendeleo kwa kasi katika taifa hii ikijumuisha vijana wote bila kubagua tabaka lolote, Falsafa hii ikitumika kwa vitendo, na hasa kwa kulipa nguvu kundi hili muhimu katika ujenzi wa taifa lolote imara duniani hakika taifa hili litapiga hatua kubwa ya kimaendeleo, kundi hili la kijamii linahitaji maandalizi mazuri toka katika hatua za awali za makuzi ya mtoto kwa kutengeneza vijana wenye maadali, uzalendo kwa taifa na watu wake pamoja, haiba nzuri na hisa njema.

Pili Tanzania inahitaji katiba bora zaidi ya nchi ilikuweza kuendesha mambo yake kwa mujibu wa sheria, sera, kanuni na miongozo itakayowekwa kwa matakwa ya kisheria yaliyoridhiwa na wananchi na kusimamiwa na serikali kutokana na katiba itakavyoainisha. Hivyo basi kwa sasa Tanzania kama taifa huru linahitaji katiba mpya ilikuendana na mazingira ya sasa, kwani katiba yetu ya mwaka 1977 Ina mambo mengi ya msingi yanayohitaji marekebisho, kuongezwa na mengine kutolewa ili iweze kukidhi matakwa ya raia wa Tanzania na kuwa dira ya maendeleo ya taifa hili. Hivyo basi sisi vijana kama taifa la leo, viongozi, wananchi, washika dau, vyama vya kisiasa, asasi za kiraia pamoja na jumuiya ya kimataifa ina wajibu wa kutilia mkazo dai hili la msingi kabisa la katiba mpya kwa Tanzania, kwani adhima hii ikitimia dira ya maendeleo ya taifa itadhihirika pia na taifa hili litastawi zaidi katika kila sekta.

Dira ya taifa na mipango ya muda mrefu ya kitaifa iwekwe kwa mujibu wa sheria na ilindwe na sheria bila kuingiliwa na wasiasa ili kama taifa tuwe na mipango ya maendeleo ya muda mfupi, wa kati na mrefu inayolenga zaidi maslahi ya wananchi wote na sio kuwanufaisha wanasiasa katika siasa zao hasa kipindi cha chaguzi za kisiasa. Bunge linawajibika kutunga sera hii muhimu sana kwa mstakabari mwema wa maendeleo chanya ya taifa hili. Mataifa yote yaliyofanikiwa duniani huwa na dira na mpango madhubuti wa maendeleo ya taifa wa muda mrefu unaoonesha uelekeo chanya wa taifa husika katika nyanja zote za kimaendeleo.

Utandawazi ni mwingiliano wa watu wa Mataifa mbalimbali unaohusishwa shughuli azifanyazo mwanadamu na kuwaleta watu pamoja zaidi hasa kupitia sayansi na teknolojia zikiwa ndizo nyenzo muhimu hasa katika kufanikisha dhima ya utandawazi ulimwengu ikiwa imeasisiwa na mataifa mawili ya Uingereza na Marekani. Hivyo licha ya kwamba utandawazi ni zao la ughaibuni limekuja na matokeo hasi pamoja na matokeo chanya. Tanzania ili itoke katika giza nene inalazimika kufuata mienendo chanya ya dhima za utandawazi ulimwenguni ili iweze kujiletea maendeleo kwa haraka na ufanisi zaidi. Mfano, kupitia majukwaa ya kiteknolojia tunaweza kununa na kujifunza teknolojia mpya kutoka kwa mataifa mengine ilituweze kuongezwa tija katika uzalishaji wetu wa viwandani na sekta zingine ilituweze kupata maendeleo makubwa ya kiuchumi, biashara za kikanda na kimataifa zikiimarika zaidi na uchumi hukua kwa kasi pia, mahusiano ya kimataifa huimalisha diplomasia ya taifa husika kwa kuwa na mahusiano chanya na mataifa mengine hasa katika masuala ya kijamii, kisiasa, kitamaduni na kiuchumi na kwa umuhimu wa kipekee sayansi huongeza wabunifu na wagunduzi katika mambo anuai na muhimu kwa ustawi thabiti wa taifa, Hinyo basi utandawazi ni muhimu sana kwa maendeleo chanya kama tu utatumiwa na taifa husika kwa uangalifu mkubwa.

Taifa linawajibika kuwekeza katika sekta nyeti zinazoajiri watu mengi zaidi ili kuimarisha uchumi na upatikanaji wa ajira hasa kwa vijana, Tanzania inatakuwa kuwekeza pakubwa katika sekta ya kilimo, utalii, uvuvi na mifugo pamoja na madini ili iweze kunufaika kwa kiasi kikubwa na rasilimali zinazopatikana nchini na hili likiwezekana basi hata hali za wananchi kiuchumi zitaimarika sana na hivyo kuwezesha uwekezaji katika sekta zingine muhimu kwa maendeleo ya taifa kama vile afya, nishati, elimu na maji.

Mwisho, ni suala zima la elimu na upatikanaji wa ajira rasmi na zilizo rasmi kwa wananchi zenye maslahi bora kwa mwajiriwa na aliyejiajiri, Kama taifa tunalazimika kuboresha na kufanya marekebisho makubwa katika mfumo wetu wa elimu ili uweze kukidhi matakwa ya halisi ya elimu na ujuzi unaotolewa kwa watoto na vijana wetu kuendana na hali ya soko la ajira na mazingira halisi ya sasa nje ya mfumo wa elimu, hatua hii ikifanyiwa mageuzi mazuri tutapata wataalamu tajika wa kada zote za kielimu hivyo uchumi wetu utakuwa maradufu zaidi na kupata taifa lenye watu wenye fikra huru na pevu katika kufanya maamuzi chanya na thabiti kwa leo na kesho ya mama Tanzania. Hivyo basi wote kwa pamoja tuungane katika kuhimiza elimu bora kwa wote ila inayoenda na dunia ya sasa inayobadilika kwa kasi kila uchao kwa namna hii taifa huru gizani hakika litaiona Nuru angavu kabisa. Kwa pamoja kupitia elimu bora na yenye tija kwa watoto na vijana wetu taifa litainuka zaidi kiuchumi, kijamii, kitamaduni na kisiasa.

Hitimisho, namaliza makala yangu kwa kuwahimiza raia ya taifa langu pendwa Tanzania tuendelee kufanya kazi kwa bidii kubwa, maarifa na utayari wa kuyapokea mabadiliko ilikuendana na kasi ya mabadiliko ya kiulimwengu lakini bila kuathiri mila na desturi zetu kama taifa kutokana na athari hasi za utawandazi. Na pia ninawasihi wote mlio na dhamana ya kuwaongoza wananchi kuanzia ngazi ya kitaifa mpaka serikali za ugatuzi za mitaa kufanya kazi za wananchi kwa uzalendo mkubwa na kwa kumtanguliza Maulana ili adhima ya maendeleo ya kweli iweze kufikiwa kwa haraka zaidi. Kama kila mmoja wetu atatimiza majukumu yake na wajibu kama raia wa taifa hili hakika Tanzania itatoka katika kiza hiki na kukaa katika nuru.
 
TAIFA HURU GIZANI (TANZANIA)

View attachment 2310052

Kura yako ni muhimu sana gusa kimshale Cha kijani chini ya makala hii murua
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom