Tahadhari ya utapeli mpya Dar kwa sasa

jerryempire

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
5,128
8,648
Habari zenu wanajukwaa,

Maisha yamekuwa magumu sana kwa sasa hivyo kupelekea watu kubuni njia mbali mbali ili kujipatia kipato cha kuendelea kuishi.

Tupo kwenye kipindi ambacho ikifika asubuhi nyumba nzima kila mtu anaondoka kwenda kutafuta maisha tofauti na zamani ambapo ilikuwa nyumba nzima anatoka mwanamme tu hali ya wengine wanasubiria mzee alete wale.

Kupitia thread hii naomba kwa aliyewahi kutapeliwa kwa aina yoyote basi nae ashare na wengine ili watu wachukue tahadhari hakika mtaani watu wanalizwa vibaya mno.

Huu ni aina ya utapeli ambao mimi mwenyewe yalinikuta.

1. Utapeli wa simu

Huu ni utapeli ambao unagusa wengi tena mpka watu fulani wanahusishwa sana na michezo hii hasa kwenye hizi simu used,Nilinunua simu used baada ya week nilikuja kudakwa nikalazwa ndani na ilinitoka zaidi ya 500k,mpaka sasa ni bora nikanunue simu dukani na kama nitanunua kwa mtu basi nakuja nyumbani kwako kabisa tunaandikishana mkataba kabisa.

2. KUUZIWA GARI YA MKOPO
Hapa watu huwa wanalizwa sana pia unakuta gari inauzwa kwa bei nyepesi sana lakini ukienda kuikagua mhusika anakwambia kuwa kadi ya gari ilipotea hivyo anakupa copy card tu na kukupa uhakika kama ote ukiinunua tu ili uende kubadilisha kadi mwenyewe basi unakutana na bonge la deni TRA, mwisho wa simu gari inakuja kukamatwa unakuwa hupati chako,hili nalo limeshanikuta kama dalali na kulazwa ndani mpka nikaamua sitouza gari tena isiyokuwa na card.

3. WAAGIZAJI VITU TOKA CHINA
Kwa sasa kuna watu wengi sana utawaona facebook au instagram wanaagiza vitu china kwa bei ya kutupa na wengine mpaka wana ofisi kabisa wanafungua unakuta tv inch 50 smart wanauza 400k bei ya kutupwa wanachokifanya wanaita kukusanya mizigo mnakuwa mnaenda kupeleka hela kwa ajili ya kununua vitu mkifika kama watu 40 au 50 wanafunga order. Then mnaaambiwa baada ya mwez au miez miwil mzigo utakuwa umefika na mara nyingi husema wanatumia meli, basi itapita miezi hata 10,mzigo haufiki na mkienda ofisini walishasepa hapa nlilizwa 600k japo kuwa mjanja wa mjini

Kuna utapeli mwengine kama hawa mawakala wanaotembea wa tigo pesa/airtel/zantel ntaendelea kushare npatapo muda

Muhimu tushtuane ili tuwe makini zaidi mtaani watu wamevurugwa
 
Utapeli wa mabenki

Hapa ninachojiuliza ni kuwa .....Nina pesa nying kwenye account .....na hyo ni siri yangu...( kama kawaida wabongo kuficha siri kuhusu pesa zangu)
Je siku nikifariki ......benk inapeleka WAP ....fedha zanguuuu
Lazma uandike beneficiaries kama una akili na bank lazma waulize familia nani apewe mzigo kama hujaandikisha the moment mmetoa taarifa ya msiba!
 
Kuna wale wazee wa Michenzani Zenji, wapo insta wanauza vitu bei chee...

TV ya 65", unapata jamaa wanauza 1mil hivi halafu kitu LG au Samsung, hahaha na ukiwapigia mnaongea fresh kabisa, sasa tuma pesa uone vumbi kwenye maji 😂😂
 
Back
Top Bottom