Tahadhari ya Taharuki Tanganyika

Tahadhari ya Taharuki Tanganyika

Kwakuwa la ndugu zetu Wamasai tulishalisema sana lakini tukapuuzwa na kukejeliwa sana.. Ngoja sasa tuliache litutumke! Likifika pa kupasuka..TUSITAFUTANE!

Tahadhari ya taharuki kuu iliyopo mbele yetu ni ya mafuta.. Ukweli useme hali ni mbaya na tunakoelekea inaweza kuwa mbaya zaidi na zaidi

Pengine linaweza kuvumilika kwa muda kikomo, lakini sasa kuna baadhi ya maeneo nchini Tanganyika kwa sasa
Hakuna dola
Hakuna umeme
Hakuna maji
Hakuna mafuta

Hiyo dola kwakuwa wengi hawana ufahamu nayo kukosekana kwake tunaweza kuiweka kando.. Lakini vipi hayo mengine matatu?

Kwenye biashara hakuna umeme
Barabarani hakuna mafuta
Nyumbani hakuna maji, hakuna umeme.. Uchumi wetu unapigwa kelebu tatu bila!

Tunakoelekea ni kwenye state emergency.. Lakini viongozi wako busy na mengine yasiyo muhimu
Wengine wako kimya
Wanaotoa matamko wanachanganyana
Huwezi kuamini mpaka sasa hakuna aliyejiuzulu kuonesha uwajibikaji!

Katikati ya mtanziko mkubwa kama huu, jeshi letu tukufu linatoa kauli kuingia mitaani na majumbani kusaka nguo za mitumba kafaulaya zinazofanana fanana na za kwao! Hiki ndio kipaumbele jeshi letu la ulinzi kwa sasa[emoji848][emoji24]..... Ambalo mmoja wa viongozi wake aliongopa wazi ni la sita kwa ubora duniani[emoji1544][emoji1550][emoji23]
Wacha ikae hivyo hivyo
 
JE, MUUNGANO NA TANGANYIKA VIMEBAKIA KUWA MFUPA WAKATI ZANZIBAR INANAWIRI?

Kila mtu anaweza kutafsiri tofauti kazi yoyote ya sanaa ingawa maana iko kwa mtunzi. Tafsiri yangu kwa hiki kikaragosi (katuni) cha Masoud Kipanya ni hii: Skeleton (huyo samaki mkubwa aliyebakia mkia na kichwa) huonyesha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (iliyowakilishwa kama kichwa) na Tanganyika (iliyowakilishwa kama mkia).

Samaki wadogo walionenepeana ni Zanzibar (samaki mkubwa kidogo) na Visiwa vya Unguja na Pemba (samaki hao wadogo) pamoja na visiwa tegemeo ambavyo huunda Zanzibar. Wanaonekana siha au afya yao inatokana na wao kupata lishe kwa kumla samaki mkubwa.

Tafsiri hii katika literature (fasihi) ndio ambayo tunaita reader response ikiwa na maana kuwa msomaji anaweza pia kutoa maana yake katika kazi ya faisihi hasa ambayo mtunzi wake yuko mbali au hawezi kuwa huru kufafanua maana.

Tafsiri yangu inakwenda na muktadha na siku ambayo kikaragosi hiki kimetolewa, tarehe 12 Januari 2026 ambayo ni siku ya maadhimisho ya miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Lakini kama wewe huamini katika uhuru wa kazi za fasihi waweza kwenda kumtia pingu Kipanya hata 'kumpilipili' Askofu Mwamakula ambaye ndiye mchambuzi wa kikaragosi cha Kipanya.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandakile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 12 Januari 2026; Saa 12:03 asubuhi.
1768227936756.jpg
 
Back
Top Bottom