Tahadhari ya matapeli kupitia simu za mikononi

kikahe

JF-Expert Member
May 23, 2009
1,350
282
Wadau, chukueni tahadhari kuhsu hizi namba ambazo kuna watu wanajiita wadau wa Kilimo kwanza wanafanya biashara ya spea za matrekta ya kilimo kwanza. walinipigia simu kwa kubadilisha sauti na kujifanya kuna muuzaji na wanunuzi na mwisho wanakwambia utume fedha ya usafiri sh. 400,00/= Namba hizo ni 0684885948 anajiita Charles Msigwa, Mhasibu ambaye ni mnunuzi anajiita Madam Getrude 0753920800, muuzaji anayejifanya yuko VETA anajiita mzee Saidi 0788337211, anayejiita Boss wa Kilimo kwanza 0759335693, Cashier ambaye walitaka nimtumie hela anajiita Fredrick Amati 0710101445. Kuweni makini na hawa matapeli.
 
Pole sana kwa masaibu, Kikahe.

Nakumbuka mwaka juzi (2015) kijana mmoja wa chuo alinieleza sakata hili.Basi kijana alifurahi sana baada ya kuona kapata tenda (kosa), akawa ananificha ili mwisho wa siku apate zile fedha peke yake.

Mimi namuuliza, mbona unapigiwa simu zisizo na kikomo?. Kuna lipi ambalo hutaki kunishirikisha?.

Anaishia kuniambia "Kuna mshikaji wangu kanipigia simu, ananijua kabisa ila mimi nimepoteza cont za watu wengi majuzi baada ya line yangu kupotea.Sasa kanipigia simu na nikijifanya simkumbuki ataninyima hii dili" (kosa la pili).

Akaendelea kumkubalia mshikaji wake huyo (Tapeli) pasipo kumtafiti hata kidogo.Basi matapeli wakampanga vilivyo, nakuambia kijana akacharuka.Alipigiwa hiyo faida baada ya kuuza majembe ya matrekta akajikuta anajisemea kimoyomoyo "Huyu mshikaji hata kama ni bahili vipi, hapa sikosi mil 9" (Kosa la tatu).

Alipomalizwa zaidi ni pale aliporushiwa namba fulani (sizikumbuki) na kuambiwa mpigie huyu boss, Ni mchina na umueleze kuwa sisi ndio tunahitaji majembe ya trekta.Basi kijana kusikia sauti ya mtu asiyeifahamu kiswahili vizuri (Lafudhi ya kichina) ndipo alipochanganyikiwa mazima.

Hapo mimi naelewa triki zoote za matapeli, kuanzia longolongo zao, Fix zao za hapa na pale nk.Ila kijana aliona akinishirikisha itampasa anigawie hela kidogo baadaye, jambo ambalo ni upuuzi.

Baada ya kupangwa na matapeli akaambiwa aende hoteli fulani kubwa hapa Dsm (Jina nalihifadhi) akakutane na mtu fulani na afanye malipo ya Tsh 400,000/= ndipo baadaye wakachukue mzigo (Jembe za trekta) then baada ya hapo sasa ndipo akapatiwe mil 9 yake.

Akaja kwangu ananiomba nimkopeshe hela then mkopo wake utakapotoka anirudishie hela yangu, Nikamuuliza hela za nini?.Alinificha sana mwanzoni ila baadaye akaamua kunieleza A-Z.

Basi nikaanza kumueleza mwanzo mwisho jinsi anavyoibiwa na baadaye aliishia mdomo wazi.Ahaa zilikiwa nyingi kuliko maelezo.

Nikampa mifano mingi ya utapeli wa namna ile na alinishukuru sana kwa kumtoa midomoni mwa Matapeli.From there akaacha ujuaji na hakuibiwa tena fedha.

My take,

Matapeli wamejaa sana mjini.Kila mtu awe makini na afikiri kabla ya kutenda.
 
walishanipigia awa mkuu . mi nilimwambia hyo tenda mpe ndg yako akakata simu
 
+255782085073; 0689073672 na +255786651060 walijifanya kuwa na NGO wakanitapeli 1.6m 2014. Niliumia hadi leo inanitouch.
 
tatizo kubwa mkuu mpaka m2 anatapeliwa yeye binafsi anakuwa na tamaa na matapeli wanachukulia udhaifu tamaa yake ndo palepale m2 anatapeliwa
 
Wadau, chukueni tahadhari kuhsu hizi namba ambazo kuna watu wanajiita wadau wa Kilimo kwanza wanafanya biashara ya spea za matrekta ya kilimo kwanza. walinipigia simu kwa kubadilisha sauti na kujifanya kuna muuzaji na wanunuzi na mwisho wanakwambia utume fedha ya usafiri sh. 400,00/= Namba hizo ni 0684885948 anajiita Charles Msigwa, Mhasibu ambaye ni mnunuzi anajiita Madam Getrude 0753920800, muuzaji anayejifanya yuko VETA anajiita mzee Saidi 0788337211, anayejiita Boss wa Kilimo kwanza 0759335693, Cashier ambaye walitaka nimtumie hela anajiita Fredrick Amati 0710101445. Kuweni makini na hawa matapeli.
Hao ni matapeli asee,walishawai kunipigia kwa sound izo izo za vipuri vya matrekta.Uzuri huwa nipo very connected na wife when comes to ishu za pesa,Simply tukawashtukia ni maboya matapeli
 
Back
Top Bottom