Nisha anza kuhisi harufu flan.
Kuna siku katika pitapita zangu nilikutana na mkusanyiko wa watu wengi nikaona itakuwa vyema na mimi nisogee nishuhudie kinachoendelea,Nilipofika nilmkuta kijana mmoja wa kiislam akiwa na wasaidizi wake watatu.Katika eneo hilo kulikuwa na Meza na vipaza sauti,Na wingi wa umati ule walikuwa ni Waislamu katika kufika kwangu yule Bwana alikuwa anaendelea kutoa maelekezo amabpo tayari kuna vijana na wakiume walikuwa kama nane wamejipanga Mstari mmoja mbele ya yule kijna wa kiislam,Yule Kijana wa kiislam(ni mwite kiongozi)alitoa mafuta kwenye chupa akajipaka mkononi(kulia)huku mkono wa kushoto akiwa kashika mic,kiongozi huyu akamwendea mtoto moja baada ya mwingine akawa anamgusa kwenye paji la uso pamoja na maeneo ya puani huku akisema kwa sauti"majini hamna nafasi tena katika mwili wa mtoto huyu" mtoto akiguswa maeneo ya kwenye paji la uso na puani alikuwa akidodondoka kama mzigo huku wasaidizi wa yule kiongozi wakisaidia wale watoto kudondoka vizuri,alifanya hivyo kwa watoto woote nane,6 walidondoka ispokuwa wawili tuu hawakudondoka,Kiongozi akawa anawauliza mtoto mmoja baada ya mwingne "nimekusukuma" watoto karibia woote walisema hapana akasema ila walihisi nini wakajibu "kizunguzungu" sikuendelea kukaka sana pale nilianza kuondoka huku akiwataka wanaume wengine nane wajongee mbele,nikiwa naendelea kupiga hatua kwa mbali nilmsikia kiongozi huyo akitamka ni mafuta yaliyotoka mbali,yamechanganywa na maj ka sio maji basi ya mafuta ya zAmzAm,Huku akihimiza ndugu zake waislam wanunue mafuta ya hayo ili kuchangia Gharama kidogo manake mafuta hayo yame panda ndege kuletwa huku,Yametoka Arabuni na Maji yametoka kwenye kisima Cha Mtume nani sijui(manake nilikuwa nisha fika mbali)
Kwaio maaskari Uchunguzi unaweza ukaanzia Kwenye Mafuta hayo,Kwa kuwauliza waathirika wa wizi huwo hayo maji harufu yake ilikuwaje, huku wakifananisha na hayo wanayotembezaga kwenye mi hadhara.Nna wasiwasi maji au mafuta hayo yakawa na uhusiano ispokuwa wezi washa anza kuyatumia kwa manufaa mabaya.
Ni maoni yangu uki Complain sio mbaya na wewe utakuwa ni Mtizamo wako Tuu.