Tahadhari-wizi wa ajabu Dar!

Tahadhari-wizi wa ajabu Dar!

Asante kwa taarifa.
Cha msingi tuwe makini...dunia imeharibika.
 
Bado sijaelewa....
Inakuaje haoo wezi wanaweza kujipaka mkono wasizimie/kuanguka???!!!
 
Mkuu Chloroform haina adhari za hapo hapo naitumia sana kwa kazi zangu naijua ukiinusa au kupaka usoni itakuchukuwa muda kidogo na hasa usiku unapolala unalala sana.

really!! basi tunalo, ila mleta mada hajatoa specifics za time so my guess is kudetermine jibu itakuwa ngumu, ila kama sio chloroform kazi tunayo Tz hii, tuwe makini jamani
 
Ninayeongea nanyi ni shuhuda mara mbili wa wizi husika.Kumetokea aina mpya ya wizi hapa jijini Dar ambapo mwizi hutumia aina fulani ya maji ambayo ukinyunyiziwa unabaki umeduwaa au unazimia.

Wiki tatu zilizopita jirani yangu mwenye biashara ya tigo pesa aliibiwa sh milioni 9 baada ya wezi hao kufika eneo lake la biashara na baada ya kumshika usoni mfanyakazi wake aliduwaa na wezi hao kubeba pesa zote.Hata hivyo wiki iliyopita wezi hao walikamatwa baada ya uchunguzi wa askari na kesi inaendelea.

Leo hii muda wa jioni nilipigiwa simu na staff mwenzangu akilia kwamba amerudi nyumbani na kukuta housegirl wake akiwa hoi huku tv,music system pamoja na fedha vikiwa vimeibiwa.

Nilikwenda huko na tukafuatilia na kugundua kuwa msichana huyo alikuwa akisumbuliwa kwa kutongozwa mara kwa mara na mtu asiyejuana naye vizuri kiasi cha kuzoeana hadi kumwelekeza nyumbani na alikuwa akija kumtembelea jamaa anapokuwa kenda kazini yeye na mkewe na watoto wakiwa shule.

Baada ya kupata nafuu,msichana huyu ametueleza hayo na kusema kuwa leo hii jamaa alikuja na wenzie wawili akiwa na kichupa kidogo chenye maji mkononi na kumwagia usoni,akaanguka na kupoteza fahamu hadi alipostuka mbele yetu jioni hii.

Tumekuta nyumba imepekuliwa sana kama watu waliokuwa na muda wa kutosha kutafuta vitu na nadhani walikuwa wakitafuta pesa nyingi ingawa walikuta tu laki 8 kabatini.

Kilichonifanya niandike hapa ni taarifa tulizozikuta polisi kuwa matukio ya aina hii yameanza kushamiri sana hivi sasa na wamepokea malalamiko mengi ya aina hii na baadhi ya watu kukamatwa wakiwamo akina mama wawili wa kiarabu wanaodaiwa kumuuzia maji hayo mmojawapo wa watuhumiwa.Nawatahadharisha wakazi wenzangu wa Dar kuwa waangalifu.

Inasemekana wezi hummwagia mtu maji usoni au hujipaka mikononi ambapo wakimshika tu kwa mikono hiyo anapoteza fahamu.Sijafahamu kwamba maji haya ni kemikali zenye athari hiyo au ni ushirikina.

Naomba vyombo vya dola vifuatilie kwa undani na kukomesha wizi huu kama ilivyokuwa ule wa kuspray vioo vya magari.Mwenyezi Mungu mwenye haki atawakomesha wale wote wenye kuwaza uovu juu ya wenzao.Tafakari,chunguza,chukua hatua.

Hii inatisha!
 
Kweli bongo, bongo kweli yaaani mnamkuta mtu kazimia nyumba imepekuliwa mnakaa kusubiri housegirl aamuke ?????? Hayo maji mnajua yana nini??? Mnafahamu athari za hayo maji ??????? kweli tukio la namna hiyo mnaendelea kuishi kwenye nyumba tuuuu??????
Plsease iteni crime scene wafunge hiyo nyumba wataalamu wachunguze ni kitu gani hasa???/

Mh!! sisi bado hatupo ki@Digitali
 
Mungu atusaidie jamani

huwezi jua wanakufata saa ngapi na wapi.

mfano kama hao wanaoenda majumbani, wadada wa kazi walivyo mabogas wanaweza kwenda kwa njia nyingi mfano kama mpiga picha, muuza nguo, urembo n.k
 
Tunamshukuru mleta habari, hivyo wananchi wote hasa sisi wenye nafasi ya kupitia humu jf tuwajulishe wenzetu wasio na nafasi hiyo wawe makini, naamini tutashinda kwani mungu yupo na wanadamu.
 
kakobe yeye anatumia pete kwa maana hii hao ni jamaa zake watenda miujiza
 
Mungu atusaidie jamani

huwezi jua wanakufata saa ngapi na wapi.

mfano kama hao wanaoenda majumbani, wadada wa kazi walivyo mabogas wanaweza kwenda kwa njia nyingi mfano kama mpiga picha, muuza nguo, urembo n.k
mabogas?! Wanatamaa halafu hawajatulia, mie siku hizi naona bora wamama tu. Wadada siwataki kabisa. Ila ni neema tu kupona
 
Naomba vyombo vya dola vifuatilie kwa undani na kukomesha wizi huu kama ilivyokuwa ule wa kuspray vioo vya magari.Mwenyezi Mungu mwenye haki atawakomesha wale wote wenye kuwaza uovu juu ya wenzao.Tafakari,chunguza,chukua hatua.


Asante kwa ujumbe,

Ila bora ungesema wananchi tushikamane tuwasake hao watu, vyombo vya dola vimeelekeza nguvu kung'oa kucha na meno ya raia bila ganzi, na hivi umevitaja hapa ndo kwanza vinanyemelewa na usingizi wa alfajiri vinavuta blanketi!!
 
Tiririka Kwa Hoja ueleweke,mbona mii nimesomeka vizuri tuu.Acha upuuzi ukitaka matusi mbona kila mwenye uwezo wa kuandika anaweza akatukana tuu,usiwe kama mpuuzi,utachekwa kwa dharau,

umeingiza udini ngifi wewe, sina issue na story wala nini nina issue na wadini mbwambwa:A S-frusty2:
 
Back
Top Bottom