ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 21,320
- 50,538
Juzi tarehe 24 siku ya Muungano natoka zangu tabata job saa 5 usiku naelekea mliman city nilivo shuka pale ubungo na daladala nikapiga hesabu nikaona kwann nipotezee hela ya bodaboda akati miguu ninayo na huku ile matata ya barabaran ikanipagawisha nikaona ngoja nitembee mbona sio mbali, Nimekaribia pale mbele wanapouza uza maua mwili ukasisimka nikahisi mtu nyuma ananifuata ile nageuka nimepigwa kabali mwenzake akaja akanipiga na kitu puani damu ikatoka nikchafuka shat kidogo wakaja wengine wawili wametoka kwenye maua mmoja kashika panga, nikaona hii hatari nilikuwa na simu ya kawaida sio smartphone nikawatupia nikwaambia haya chukueni hio simu yenu..
Dogo mmoja akawaambia kwanini huyu tusimmalize tu ile nimeinuka nikimbie wakaniwahi na wallet hao wakaingia ndani ya chaka Lao, kidogo naondoka bodaboda akaja kwa kasi akanivuka kwa mbele nikamwita.. Nikamsimulia akanipakia tumefika hom tukampa hela akakataa akasema amenisaidia tu nikaona safi tu... Ila mwisho wa siku ndo hivo amesema maeneo yale kwa sasa kuna wezi sana na watu wanalizwa sana kila siku matukio mengine ni kama hayasikiki ila Yapo sana, nilikuwa naskia watu wanaibiwa kwa style hizo kwa mara ya kwanza na mimi wameniharibia.. Nimeona niwape stori nzima ili mjue vibaka ni watu wa aina gani, wanaweza wakakuua kwa kweli..
TAHADHARI usiku jijini