SNAP J
JF-Expert Member
- Dec 26, 2013
- 7,079
- 7,976
Baada ya zoezi la kujiandikisha kupiga kura kwa kutumia mfumo wa kidigitali, a.k.a BVR kukamilika nchini,taarifa nilizozipata ni kuwa ifikapo October 25, zoezi la kupiga kura litafanyika manually, na sio kidigital kama wengi tulivyokuwa tukifikiria.
Yaani,wananchi watapiga kura kwa mfumo ule ule wa zamani kwa kutumia kalamu na karatasi kwenye vituo maalum vya kupigia kura vitakavyo teuliwa nchini.
Kwanini nasema uwezekano wa "goli la mkono" ni mkubwa?
Taarifa nilizozipata zinasema kuwa hawa jamaa wamejipanga kisawasawa kuhakikisha wanaingia ikulu mwaka huu, kwani ukweli wameshaujua kuwa upinzani lazima uchukue nchi mwaka huu.
Taarifa hizo nilizodokezwa zinasema kuwa karatasi zitakazotumika kupiga kura zitachakachuliwa kwa kuwekwa "material maalum" katika visanduku vya upinzani.
Hii itakuwaje?
Pale mpiga kura atapotiki kwa kalamu kuchagua mgombea wa upinzani, mfano EL katika kisanduku chake, na kukunja karatasi hiyo mara moja katika pande mbili zinazolingana, ili kuweza kuitumukiza katika sanduku la kupiga kura, basi wino huo utapogusana na upande wa mwingine wa karatasi, ambapo ndipo patakuwa na kisanduku cha mgombe wa ccm, mfano, JPM, basi tiki hiyo itafutika ( kwa lugha ya kiingereza tunasema "cut and paste" )na kuhamia upande wa kisanduku cha mgombea wa ccm, na kuonekana kana kwamba mpiga kura aliweka tiki katika kisanduku cha mgombea wa ccm.
Ndio maana haingii akilini kusikia serikali imepoteza Mabilioni ya fedha kwa ajili kuandikisha wananchi kwa huu mfumo mpya wa kidigital (BVR), na mwisho wa siku watu waje wapige kura kwa mfumo ule ule wa zamani.