Tahadhari: Uwezekano wa "goli la mkono" ni mkubwa Oct 25

SNAP J

JF-Expert Member
Dec 26, 2013
7,079
7,967
Baada ya zoezi la kujiandikisha kupiga kura kwa kutumia mfumo wa kidigitali, a.k.a BVR kukamilika nchini,taarifa nilizozipata ni kuwa ifikapo October 25, zoezi la kupiga kura litafanyika manually, na sio kidigital kama wengi tulivyokuwa tukifikiria.

Yaani,wananchi watapiga kura kwa mfumo ule ule wa zamani kwa kutumia kalamu na karatasi kwenye vituo maalum vya kupigia kura vitakavyo teuliwa nchini.

Kwanini nasema uwezekano wa "goli la mkono" ni mkubwa?

Taarifa nilizozipata zinasema kuwa hawa jamaa wamejipanga kisawasawa kuhakikisha wanaingia ikulu mwaka huu, kwani ukweli wameshaujua kuwa upinzani lazima uchukue nchi mwaka huu.

Taarifa hizo nilizodokezwa zinasema kuwa karatasi zitakazotumika kupiga kura zitachakachuliwa kwa kuwekwa "material maalum" katika visanduku vya upinzani.

Hii itakuwaje?

Pale mpiga kura atapotiki kwa kalamu kuchagua mgombea wa upinzani, mfano EL katika kisanduku chake, na kukunja karatasi hiyo mara moja katika pande mbili zinazolingana, ili kuweza kuitumukiza katika sanduku la kupiga kura, basi wino huo utapogusana na upande wa mwingine wa karatasi, ambapo ndipo patakuwa na kisanduku cha mgombe wa ccm, mfano, JPM, basi tiki hiyo itafutika ( kwa lugha ya kiingereza tunasema "cut and paste" )na kuhamia upande wa kisanduku cha mgombea wa ccm, na kuonekana kana kwamba mpiga kura aliweka tiki katika kisanduku cha mgombea wa ccm.

Ndio maana haingii akilini kusikia serikali imepoteza Mabilioni ya fedha kwa ajili kuandikisha wananchi kwa huu mfumo mpya wa kidigital (BVR), na mwisho wa siku watu waje wapige kura kwa mfumo ule ule wa zamani.
 
Duh kama ni kweli basi kazi ipo.Hizo Karatasi za kura zifanyiwe QAQC (lugha nyepesi UHAKIKI wa Kutosha) basi kabla ya kutumika nchi nzima.Lakini yote hayo tatizo ni nini?
 
Tatizola tume MZee wetu Lubuva ni mwoga anaogopa ccm vibaya mno,kwanza huyu MZee ameshazeeka anaogopa kufa kwa kutenda haki ??yaani MZee Lubuva anaogopa ccm kuliko mungu wake,yaani upande Wa haki Wa mungu haogopi Bali Anaogopa upande Wa shwetani ccm ni shida !!
 
Jamani haiwezekani chedema na vyama vyote vya upinzani kuna wasomi wengi sana siwezi amini kuwa ccm wanaweza kufany hiyo then wasomi wetu wanyamaze haiwezekani kabisa lowasa lazima awe rais wa nje.

Tumaamua kubadilisha.
 
Mbona mnaanza kuogopa si mlisema mna Lowassa? si mnasema na nyie mmejipanga? alafu si mnasema mnashinda asubuhi? shindeni sasa.
 
Zoezi la goli la mkoni lilishaisha bro..kinachosubiriwa ni muda na saa..
 
Watanzania na wapenda mabadiliko anzeni mazoezi ya kulizuia hilo goli. Arusha tumeshaanza Mazoezi mepesi kulizuia hilo goli.
 
Hii ni changamoto kubwa kwa upinzani kwani ccm wapo radhi kufanya kila aina ya uchakachuaji ilimradi tuu waendelee kubaki madarakani kwani tangu 1995,wameshakomaa katika hili.
 
Jamani haiwezekani chedema na vyama vyote vya upinzani kuna wasomi wengi sana siwezi amini kuwa ccm wanaweza kufany hiyo then wasomi wetu wanyamaze haiwezekani kabisa lowasa lazima awe rais wa nje.

Tumaamua kubadilisha.

mkuu, ndio maana hawa jamaa wanasisitiza ushindi kwao lazima mwaka huu.
 
Tatizo mfungaji wa goli la mkono kavunjika mkono....sijui atalifungaje

Ngoja nimalizie hizi picha kabla ya Sept 1

1439451149853.jpg
 
Jamani haiwezekani chedema na vyama vyote vya upinzani kuna wasomi wengi sana siwezi amini kuwa ccm wanaweza kufany hiyo then wasomi wetu wanyamaze haiwezekani kabisa lowasa lazima awe rais wa nje.
Kuchukua tahadhari ni muhimu
Tumaamua kubadilisha.

kuchukua tahadhari ni muhimu
 
kama ndivyo elimu itolewe wapiga kura wasikunje kura kwa tiki kuwa ndani badala ya wakunje kwa nje ili ishindikane kupesti.
 
Sidhani kama hili litaezekana. Besides hata kama watafanya halitafika mbali maana CCM yenyewe mmeguko hii habari italeak haraka sana na itadhibitiwa na wapambe wa Lowasa ndani ya CCM
 
wasomi wengi na hizo njama kama zipo hapa basi wanazifahamu so kitaeleweka tuu hakuna wizi utaopita mwaka huu
 
Dawa ya ujanja kama huo ni rahisi kwa watu walio makini. Unawahi kituoni unapiga kura yako kwenye chumba cha siri, unaikunja karatasi unakaa kama dk 1, the unaikunjua kuona kama kuna mabadiliko yoyote. Kama imebadilika unapiga kelele kumuita wakala wa cdm na msimamizi wa kituo kuona maajabu hayo.Watakachofanya ni kuifanya hiyo karatasi kuwa imeharibika na utapewa nyingine ambayo sasa utaitik mbele yao ili kuthibitisha uovu huo. Mchezo unaishia hapo, tutajuzana tanzania nzima, ndani ya saa moja uchaguzi unafutwa.

Uchaguzi uliopita zilikuwepo tetesi kama hizo, mimi nilikaa kwenye chumba cha siri cha kupigia kura kwa dak 5 nikisubiri kitu kama hicho kitokee kwenye karatasi yangu lakini hakikutokea.

Njia nyingine ni kuikunja kinyume na walivyoelekeza wao halafu nawahi kitumbukiza kwenye sanduku, hawezi kutoa tena
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom