Tahadhari ukiwa unakuja Tarime

Tahadhari ukiwa unakuja Tarime

Forfofo

Senior Member
Joined
Aug 22, 2024
Posts
161
Reaction score
359
Tarime bwana watu ni Civilized ila sio wanyonge, humble people lakini hawapendi kuonewa au kujishusha shusha bila sababu ya lazima ya kumfanya ajishushe. Yaani mtu akukanyage tuu bahati mbaya alafu akwambie samahani!! Mura murisia huo ni uoga. Neno samahani kwa tarime ni ngumu sana zaidi atakwambia "haya yameisha" kwaio usije kuwashangaa.

Aisee usimtongoze mke wa mtu, pindi unapofika tu Tarime basi zile tabia zako za kidaslama acha tata.

Ukiolewa na Mtu wa Tarime basi uishi kama mke, kama bado ujawa tayari kuolewa au unafanya majaribio ya ndoa basi kayafanye sehem nyingine ila sio Tarime. Tarime hakuna fala

Huko bwana Watu ni majasiri na misimamo ya hali ya juu, itakuchukua mda kumbadilisha ktk kile anachokiamini kwaio kuna vitu vitakushangaza mwanzoni. Wanapenda sana kufata utaratibu na sheria ya nchi inavyotaka

Ukifika Tarime waheshimu, usitongoze wake za watu hata kwa kutania tu, ukimulewa binti nenda kwao,na ukimuoa mtoto wa mtu ukamletea ujinga ndugu yangu wakikuita kwao usiende,utachezea fimbo vibaya hawataki ujinga.

kuwa bussy na mambo yako, usiwaonee watu. Tarime utaishi vzr sana utapewa mashamba bure utalima.

Tarime bado wanafata sana mambo ya asili kama tamaduni, mila, vyakula. Ukifika utakutana na Busara, ugali wa udaga na mtama kwa nyama choma mixer kichuri, ndo chai kule.

Ukila wali mchana na jioni watu wanakushangaa wanajua wewe wa Darisalama. mtoto miaka mitano ashatahiriwa,miaka 15 ashatahiriwa tena bila ganzi sasa wewe miaka 28 ndo unaenda kutahiriwa aaah kweli sokoro!

karibuni Tarime.
 
Back
Top Bottom