TAHADHARI: Ugonjwa wa 'dengue' waingia Dar es Salaam!


gfsonwin

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Messages
17,691
Likes
3,661
Points
280
Age
46
gfsonwin

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2012
17,691 3,661 280
Kwa wale wafuatiliaji wa habari za magazetini, mtakuwa mmesikia kuhusu kuzuka kwa ugojwa uitwao "Dengue fever" ama kwa kiswahili huitwa Homa ya Dengue.

Habari zinasema kwamba tayari watu sita wameshathibitika kuwa na tatizo hili na tayari wako hospitali. Juma lililopita, ugonjwa huu uliua watoto wapatao 6 katika Wilaya ya Ilala na ikasemekana kwamba ni 'Malaria kali' lakini baada ya sampuli za damu kupimwa zaidi ilionekana walikuwa na homa ya dengue!

Wito wangu kwa wana JF wenzangu, nawahusia kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huu.

Labda hapa niwaeleze huenezwa na nini?

Ugonjwa huu huenezwa na Mbu aina ya aedes mosquito, na hawa mbu wamegawanyika makundi 2 hivi, nafikiri watu wa taxonomy wataweza kunisaidia vizuri zaid, na specifically mbu hawa hubeba vijidudu viitwavyo dengue virus. Vijidudu hivi huwa na selflimiting kama walivyo virus wengine hivyo jinsi ya kupona hakuna dawa maalum.

Dalili za ugonjwa huu
Dalili huanza kuonekana siku 4-7 baada ya kuumwa na mbu mwenye hawa virus.Dalili za dengue ya kawaida

  • homa kali zaid ya 40 degrees
  • maumivu makali ya kichwa na hasa kipanda uso
  • maumivu ya viungo na misuli
  • harara mwili mzima ambazo hutokea baada ya siku 3-4 baada ya kuumwa na mbu
Pia Dengue hemorrhagic fever huwa ni pronounced zaid na hii huweza kusababisha kifo. dalili zake ni

  • kutokwa na damu puani, kwenye fizi ama kutoka bruises zenye rangi ya wekundu kwa mbali kwenye ngozi
Dengue shock syndrome ni severe form na hii hutokea kwa watoto ambao wamekuwa re- infected na huyu mbu na mara yingi sana husababisha mauti kwa watoto hawa. dalili zake huwa ni

  • kutokwa damu kwa wingi massive bleeding
  • shock (very low blood pressure)

TIBA:

HAKUNA TIBA MAALUM AMA KAMILI KWENYE HUU UGONJWA KAMA ILIVYO KWA BAADHI YA MAGONJWA YASABABISHWAYO NA VIRUSI.

Lakini mgonjwa anatakiwa apate muda wa kupumzika, anywe fluids kwa wingi na ameze dawa za kushusha homa hasa paracetamol. Asprin haziruhusiwi kabisa kutumiwa unapoona dalili hizi sababu nitazieleza baadae.

kwa mgonjwa ambaye na shock yani kutetemeka ama yuko na hali mbaya sana basi ni bora awah hospitali na hapo atapatiwa matibabu ya haraka na kumwongezea electrolytes ili kuokoa maisha ya mgonjwa.

cc AshaDii, Riwa, ladydoctor, @mupricino, Kongosho, King'asti, Mtambuzi, DARKCITY, Kipaji Halisi, Paloma, cacico, snowhite, Kaunga,@FP, mwaJ, Madame B, amu Allien Mzee wa Rula, Ruttashobolwa et al
 
Kongosho

Kongosho

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2011
Messages
36,078
Likes
392
Points
180
Kongosho

Kongosho

JF-Expert Member
Joined Mar 21, 2011
36,078 392 180
Sasa watoto shuleni itakuwaje jamani, mbona kizaazaa hiki.
Bora shule zifungwe siijui, am so worried jamani.
 
Mr Rocky

Mr Rocky

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2007
Messages
15,198
Likes
600
Points
280
Mr Rocky

Mr Rocky

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2007
15,198 600 280
Asante sana gfsonwin hii taarifa niliisikia kwenye magazeti asubuhi na sikupata maelezo ya kina ila asante sana kwa taarifa yako
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Messages
17,691
Likes
3,661
Points
280
Age
46
gfsonwin

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2012
17,691 3,661 280
Asanten sana gf kwa kuanzisha hili, nimesikia leo nikaogopa na nilikuwa nautafuta niusome.
usijali wangu, nimeona nililete ili kuwafahamisha watu.
ni heri kujikinga mapema
 
gfsonwin

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Messages
17,691
Likes
3,661
Points
280
Age
46
gfsonwin

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2012
17,691 3,661 280
Sasa watoto shuleni itakuwaje jamani, mbona kizaazaa hiki.
Bora shule zifungwe siijui, am so worried jamani.
yaani acha tu, but kwenye mashule ni bora sasa wazazi wawaelekeze watoto wao kutumia net.
na hata kwa watu ambao wana immuno compromise na wenyewe wajilinde sana it is scarey kwakweli
 
gfsonwin

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Messages
17,691
Likes
3,661
Points
280
Age
46
gfsonwin

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2012
17,691 3,661 280
Ngoja nitafute fumigation wiki hii, hii ni hatari sana
usafi wa aazingira ni muhimu sana na hasa kuzika makopo na kufyeka nyasi na kufunika masinki na mashimo yanayokuwa mazalia ya mbu.
usiku watoto walale kwenye chandarua na ili wasiguse kuta za chandarua basi wapangie mito pembeni. milango ifungwe na madirisha muda wote kupunguza idadi ya mtu wanaoingia ndani. istoshe muda wa kukaa sebulen kuangalia tv upunguze sana manake hili ndilo eneo ambalo watoto huumwa na mbu zaid wawapo nyamban
 
Ennie

Ennie

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2011
Messages
7,142
Likes
64
Points
145
Ennie

Ennie

JF-Expert Member
Joined Jan 15, 2011
7,142 64 145
yaani acha tu, but kwenye mashule ni bora sasa wazazi wawaelekeze watoto wao kutumia net.
na hata kwa watu ambao wana immuno compromise na wenyewe wajilinde sana it is scarey kwakweli
Inatisha kwa kweli.
Ahsante kwa taarifa dear.
 
Tuko

Tuko

JF Bronze Member
Joined
Jul 29, 2010
Messages
11,192
Likes
435
Points
180
Tuko

Tuko

JF Bronze Member
Joined Jul 29, 2010
11,192 435 180
ugonjwa huu huenezwa na Mbu aina ya aedes mosquito, na hawa mbu wamegawanyika makundi 2 hivi, nafikiri watu wa taxonomy wataweza kunisaidia vizuri zaid, na specifically mbu hawa hubeba vijidudu viitwavyo dengue virus. Vijidudu hivi huwa na selflimiting kama walivyo virus wengine hivyo jinsi ya kupona hakuna dawa maalum.
Asante Mh Dr kwa taarifa. Kama sijakosea mbu hawa ndio wale weusi wenye mabaka meupe. Wanapenda sana kung'ata wakati wa jioni, au mchana maeneo yenye kivuli, lakini hata usiku pia.
Kwa hiyo wanaJF tujihadhari na mbu hawa kwa kuvaa nguo zinazofunika mwili, kutumia repellants na neti wakati wa usiku. Watoto wakingwe zaidi...
Kama sijakosea hawa mbu ndio hiambukiza pia homa ya manjano... (Entomologists watanisahihisha kama nimekosea)...
 
gfsonwin

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Messages
17,691
Likes
3,661
Points
280
Age
46
gfsonwin

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2012
17,691 3,661 280
Asante Mh Dr kwa taarifa. Kama sijakosea mbu hawa ndio wale weusi wenye mabaka meupe. Wanapenda sana kung'ata wakati wa jioni, au mchana maeneo yenye kivuli, lakini hata usiku pia.
Kwa hiyo wanaJF tujihadhari na mbu hawa kwa kuvaa nguo zinazofunika mwili, kutumia repellants na neti wakati wa usiku. Watoto wakingwe zaidi...
Kama sijakosea hawa mbu ndio hiambukiza pia homa ya manjano... (Entomologists watanisahihisha kama nimekosea)...
hapo red wish to become one some day lol! thanks for the wishes ................ cacico najua utalia wivu.
hata mie nilidhani ni hawa mbu wa mchana wale weusi wenye madoa meupe. lkn kwa wanaoeneza manjano hawa ni tofauti mbu hawa huitwa taigae kwa kiswahili naomba kusahihishwa ambao hubeba Hepacivirus wa jamii ya Flaviviridae??


binafsi sio mtaalam sana wa magonjwa yaenezwayo na vectors lakini hapa babu DARKCITY, na mzee wangu chuachakara can tell more. mwalimu wa biolojia anaishia hapo kwa leo ........................lol!
 
Last edited by a moderator:
Mvaa Tai

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2009
Messages
6,177
Likes
2,230
Points
280
Mvaa Tai

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Joined Aug 11, 2009
6,177 2,230 280

Forum statistics

Threads 1,274,858
Members 490,833
Posts 30,526,190