gfsonwin
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 18,274
- 20,673
Kwa wale wafuatiliaji wa habari za magazetini, mtakuwa mmesikia kuhusu kuzuka kwa ugojwa uitwao "Dengue fever" ama kwa kiswahili huitwa Homa ya Dengue.
Habari zinasema kwamba tayari watu sita wameshathibitika kuwa na tatizo hili na tayari wako hospitali. Juma lililopita, ugonjwa huu uliua watoto wapatao 6 katika Wilaya ya Ilala na ikasemekana kwamba ni 'Malaria kali' lakini baada ya sampuli za damu kupimwa zaidi ilionekana walikuwa na homa ya dengue!
Wito wangu kwa wana JF wenzangu, nawahusia kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huu.
Labda hapa niwaeleze huenezwa na nini?
Ugonjwa huu huenezwa na Mbu aina ya aedes mosquito, na hawa mbu wamegawanyika makundi 2 hivi, nafikiri watu wa taxonomy wataweza kunisaidia vizuri zaid, na specifically mbu hawa hubeba vijidudu viitwavyo dengue virus. Vijidudu hivi huwa na selflimiting kama walivyo virus wengine hivyo jinsi ya kupona hakuna dawa maalum.
Dalili za ugonjwa huu
Dalili huanza kuonekana siku 4-7 baada ya kuumwa na mbu mwenye hawa virus.Dalili za dengue ya kawaida
TIBA:
HAKUNA TIBA MAALUM AMA KAMILI KWENYE HUU UGONJWA KAMA ILIVYO KWA BAADHI YA MAGONJWA YASABABISHWAYO NA VIRUSI.
Lakini mgonjwa anatakiwa apate muda wa kupumzika, anywe fluids kwa wingi na ameze dawa za kushusha homa hasa paracetamol. Asprin haziruhusiwi kabisa kutumiwa unapoona dalili hizi sababu nitazieleza baadae.
kwa mgonjwa ambaye na shock yani kutetemeka ama yuko na hali mbaya sana basi ni bora awah hospitali na hapo atapatiwa matibabu ya haraka na kumwongezea electrolytes ili kuokoa maisha ya mgonjwa.
cc AshaDii, Riwa, ladydoctor, @mupricino, Kongosho, King'asti, Mtambuzi, DARKCITY, Kipaji Halisi, Paloma, cacico, snowhite, Kaunga,@FP, mwaJ, Madame B, amu Allien Mzee wa Rula, Ruttashobolwa et al

- homa kali zaid ya 40 degrees
- maumivu makali ya kichwa na hasa kipanda uso
- maumivu ya viungo na misuli
- harara mwili mzima ambazo hutokea baada ya siku 3-4 baada ya kuumwa na mbu
- kutokwa na damu puani, kwenye fizi ama kutoka bruises zenye rangi ya wekundu kwa mbali kwenye ngozi
- kutokwa damu kwa wingi massive bleeding
- shock (very low blood pressure)