Tahadhari: TRA wanatengeneza crisis ya mafuta ya kula makusudi

Mafuta ya alizeti lita 10 huku ninakoishi ni Tsh. 36,000/= na mafuta mengine yaliyokuwa yanauzwa Tsh. 27,000/= hafi 28,000/= sasa hivi yanauzwa 33,000/= Nahisi wanataka kuyaondoa kabisa mafuta mengine coz kwa hali ya kawaida huwezi kuacha kununua mafuta haya ya alizeti eti ukanunue labda Masafi au Korie kwa sababu ya tofauti ya 3000....
 
Kwa Tanzania,hizi dili zimekuwepo katika vitu tofauti mfano katika mafuta ya nishati hapa nazungumzia petroli,sukari,vitabu vya rejea n.k
Acha tunyongwe,Mungu yupo!
 
"...........na hii lengo kuu ni kuhakikisha afya za waDanganyika zina imarika kwelikweli, tutapandisha kodi ya mafuta ya kupikia mpaka ishindikane kununua, na hivyo kupunguza magonjwa yatokanayo na LEHEMU.....sisi wakemia tunajua hilo na kwa hili, waDANGANYIKA tembeeni KIFUA MBEREEE......"

Nani anaweza sema maneno kama hayo? Otea.....
 
Uzi umelala kama wabongo walivolala, wakiamka wanapitia kurasa za diamond,wema na wakaa uchi wengine.

Hawana time na maslahi yao. Nyuzi za aina hii haiwez kuchangiwa.

Mungu tuokoe Waja wako na vizazi vyetu.
Wenye akili na nia ya kweli ya maendeleo ya nchi hii wamechoka kuchangia ndugu yangu.., na sio ktk JF tuu.. Hata ktk majukwaa mengine watu wamechoka kupiga domo lisilo leta mabadiliko..
Watanzania ili tuamke tunatakiwa kumwaga damu ya kutosha kwanza..., tupimwe tezi dume.., wake zetu tunyanganywe kwa kua ni weupe, watoto wetu walawitiwe mbele zetu , Mahakama zimlinde muuaji na mwizi mkuu..
Hebu fikiria.., Raisi wa nchi anasema hatatoa msaada wa chakula kwa watu waliokumbwa na mafuriko , hebu fikiria.., Rais wa nchi anasema maendeleo ya Kaskazini yasubiri kwanza awamu hii ya Tano..., na watanzania tuna ona mambo yanaendelea kama kawaida tuu..??!

Hata mimi nanyamaza sasa.., ccm (kama kweli bado wapo..) watajua wenyewe pa kumpeleka mungu wao..
 
TRA ndio chanzo kikuu cha kuua uchumi wa Tanzania wanahama tuu leo wafanye nini na kesho wafanye nini hamna wanachokijua...wamewapa watu tenda za kuuza machine za efd hatafu mbovu wao hilo hawajui na wauzaji wajanja wajanja tuu hawatoi warrant ya ukweli ni majanga kwa wafanyabiashara...
 
TRA wamepewa mamlaka ya kimungu nchi hii.. Wao kuua biashara yako ni kwa barua moja tuu..., tayari unapelekwa ICU kama sio makaburi ya Kinondoni..

Ulizeni wafanyabiashara wanavyobambikiwa kodi..
 
TRA ndio chanzo kikuu cha kuua uchumi wa Tanzania wanahama tuu leo wafanye nini na kesho wafanye nini hamna wanachokijua...wamewapa watu tenda za kuuza machine za efd hatafu mbovu wao hilo hawajui na wauzaji wajanja wajanja tuu hawatoi warrant ya ukweli ni majanga kwa wafanyabiashara...

Kaka TRA ni kama mbwa tu wanatumwa na mamlaka za juu kufanya haya unayoyaona kwa wafanyabiashara. Wao ni kama wakamuaji wa maziwa, mwenye ng'ombe akilazimisha anataka lita 10 wakati ana uwezo wa kukamuliwa lina 6 lazima waongeze maji.
 
Uzi umelala kama wabongo walivolala, wakiamka wanapitia kurasa za diamond,wema na wakaa uchi wengine.
Hawana time na maslahi yao. Nyuzi za aina hii haiwez kuchangiwa.
Mungu tuokoe Waja wako na vizazi vyetu.
Wao andika mambo ya vibamia, mabwawa, wapenzi kung'ang'aniana, uchawi, kufumaniana, yakina Zari na Hamisa..hapo utawapata, usishangae watawala kujiona Miungu, ni Taifa lilolala, vivu la kufikiri na lilokosa hamasa kwa vijana..
Inasikitisha mno mno...
 
"Ninavyoandika usiku huu wamesambazwa maeneo yote ya pwani ili kuzuia wanaoingiza kwa magendo tokea zanzibar kwa majahazi."

Kwani hii inaruhusiwa kisheria? Magendo ni kosa kisheria?


Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom