Tahadhari-simu za mkononi

Technician

JF-Expert Member
Mar 30, 2010
841
222
TAHADHARI-SIMU ZA MKONONI

Wanabodi:
Nashauri kila mwenye simu ya mkononi
Amtambulishe mke wake kwa maneno "My Wife" au "Mke wangu"
Au kwa wanawake "My Husband" au "Mume Wangu"
Na kwa bachelors "My Fiancee" au "Mchumba wangu"
Na kwa watu wa kawaida majina muhimu kama "Mjomba,Kaka,
Dada,Shemeji,Baba Mzazi,mama Mzazi Nk.nk.nk

Sababu za haya majina:
Kwanza unapopata matatizo ya ajali zisizotegemewa kama wanafanikiwa Kuokota simu yako wasamaria
wema wanaweza kutoa taarifa mara moja either kwa mumeo au mke wako Au ndugu yako wa karibu.

Watu wengi wamezoea kuandika majina kama Sophia, Zainabu, shabani, Julius, Esther nk huwezi kujua Mtu
muhimu kwa huyu marehemu aliyepata ajali akafariki porini mara moja. Hii ni muhimu Sana wanaJF.

Tuzingatie hili wanaJF lisijekupata lililompata jamaa
mmoja baada ya kupata ajali na kuzimika (kuzimia) bahati nzuri alikuwa na ka-mchina kake lakini hawakuweza kumpata Mke wake mpaka jamaa anapelekwa hospital baada ya siku tatu ndo mke anapata Taarifa toka kwa mumewe.
 
Je sisi tunaoweka "security Lock" kwenye simu ili kumpata tabu mwizi asiitumie kwa urahisi?
Itasaidia nini?
 
Kuna ukweli kwenye somo lako lakini kiusalama sii sahihi sana kuji- expose kiasi hicho. Inaweza kutokea bahati mbaya sim yako ikaibwa na watu wenye nia mbaya na wakatumia majina hayo (ya mke au mume) kukufanyia kitu mbaya zaidi.
 
ni kweli mkuu ni muhimu ila UZINZI UNATUSUMBUA KWELI!

Angalia pia upande wa pili wa shilingi. Suppose unapoteza simu na ATM card yako na ume-save namba ya mke/mume kwa namna itakayo mtambulisha alieokota/alieiba na mwizi akatuma msg kama hii: Baby, hebu nikumbushe password ya Barclays", hutamjibu huyo mwizi na mkaibiwa mara ya pili?

Uzinzi unazuwiwa toka rohoni na si kwa ku-save namba ya mume/mke au kuvaa pete!
 
Ki-usalama siyo njema sana! Basi kama jamaa hawakuweza kumsaidia itakuwa bahati mbaya sana! Kinachofanyika kwenye tukio kama hilo ni kuangalia kwenye call log na kuangalia namba ya karibuni, mbona wife au husband utampata tu?!
 
Wazo zuri ila kama alivyosema gmosha hapo juu kuna wakati matapeli walikuwa wanatumia namba hizo zenye majina ya Dear,Sweetie,Husband na pia Wife kutishia kuwa wamemteka nyara mhusika na kudai malipo.Muhimu mara inapotokea ajali namba yoyote iliyoko kwenye simu atakuwa anamjua mhusika,we piga tu
 
Kwa wanaume au wanawake wazinzi ni rahisi sana kuvunjiwa ndoa endapo mngonokaji mwizi atapata nafasi kidogo ya kushika simu na kukutana na majina kati ya haya kama Honey, Wife, Sweetie, Dear au Husband na kupiga simu na kujisifia kwamba yuko na muhusika wanangonoka na wakati huo niwa mapumziko kidogo kabla ya kuendelea na mchezo. Mara nyingi kuna wivu na kupenda kuharibiana kunakofanywa na wezi wa mapenzi wanapofanikiwa kumjua mwenye mali, sijui ni kwa nini. Nawashauri wazinzi waache uzinzi Baba hapendi (Mungu).
Kwa wezi na matapeli itakuwa ni rahisi sana kufanikisha wizi au utapeli wao pia. Ila kwa kurahisisha kuwahisha ujumbe ni vizuri kuwa na majina ya kueleweka. Kwa hii kesi ingekuwa ni vizuri kama msamaria mwema angejaribu namba mpaka apatikane mtu wa karibu kabisa, hapo ndio angekuwa ameonyesha usamaria wema wa ukweli.
 
mi nashauri mtu atembee na kitambulisho au kitu chochote kitakachomtambulisha
 
Ila tumesahau kwamba watu wengi siku hizi simu zao password protect kila sekunde...Sasa hapo labda pia tushauri kwamba matumizi ya password pia ni hatari
 
Simu yangu ina "tracking system", so ukiniibia at least nitajua namba (na jina) la/ya anayeitumia.

Kwenye waleti (wallet) yangu daima kuna kadi yenye taarifa zifuatazo:
NANE: Nyetk Nyetk
NATIONALITY: Mbongo
HOME TOWN: Chitunja
CONTACTS: Reserved phone NO. & Email
MARITAL STATUS: Divorced
FAITH: Traditionalist
BLOOD GROUP: B+
HEALTH COMPS: Diabetic
ALLERGY: Magamba ya SISIMII
EMERGENCY CONTACT PERSONS: Namba ya swahiba, namba ya boss (huwezi jua) & kiongozi wa imani.

Mwenye uwezo wa kuniibia waleti sina uwezo wa kumzuia mengi, so this is a manageable risk.
 
TAHADHARI-SIMU ZA MKONONI

Wanabodi:
Nashauri kila mwenye simu ya mkononi
Amtambulishe mke wake kwa maneno “My Wife” au “Mke wangu”
Au kwa wanawake “My Husband” au “Mume Wangu”
Na kwa bachelors “My Fiancee” au “Mchumba wangu”
Na kwa watu wa kawaida majina muhimu kama “Mjomba,Kaka,
Dada,Shemeji,Baba Mzazi,mama Mzazi Nk.nk.nk

Sababu za haya majina:
Kwanza unapopata matatizo ya ajali zisizotegemewa kama wanafanikiwa Kuokota simu yako wasamaria
wema wanaweza kutoa taarifa mara moja either kwa mumeo au mke wako Au ndugu yako wa karibu.

Watu wengi wamezoea kuandika majina kama Sophia, Zainabu, shabani, Julius, Esther nk huwezi kujua Mtu
muhimu kwa huyu marehemu aliyepata ajali akafariki porini mara moja. Hii ni muhimu Sana wanaJF.

Tuzingatie hili wanaJF lisijekupata lililompata jamaa
mmoja baada ya kupata ajali na kuzimika (kuzimia) bahati nzuri alikuwa na ka-mchina kake lakini hawakuweza kumpata Mke wake mpaka jamaa anapelekwa hospital baada ya siku tatu ndo mke anapata Taarifa toka kwa mumewe.

Pamoja 100%
 
Angalia pia upande wa pili wa shilingi. Suppose unapoteza simu na ATM card yako na ume-save namba ya mke/mume kwa namna itakayo mtambulisha alieokota/alieiba na mwizi akatuma msg kama hii: Baby, hebu nikumbushe password ya Barclays", hutamjibu huyo mwizi na mkaibiwa mara ya pili?

Uzinzi unazuwiwa toka rohoni na si kwa ku-save namba ya mume/mke au kuvaa pete!

nimeikubali hii cna ubshi mze.
 
Back
Top Bottom