Tahadhari: Siku ya UKIMWI duniani 2019

Gluk

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
1,856
2,953
Leo ikiwa ni siku ya UKIMWI duniani hatuna budi kukumbushana mambo kadhaa juu ya janga hili hatari, hususani sisi vijana ambao ni wahanga wakubwa wa janga hili.

Naona siku mbili tatu humu jukwaani kumekuwa na mada nyingi zinazohusu janga hili.

Ila nilichoona ni kuwa vijana wengi tumejisahau sana na kutokujali kabisa afya zetu.

Hapa tunajifariji na kuona ni masihara ila ukweli ni kwamba huu ugonjwa usikie tu kwa jirani.

Binafsi nimewahi kupata ushuhuda kwa marafiki zangu wawili vipenzi sana. Mmoja aliupata kwa kutembea na Jimama wakati anasoma na mwingine kaukwaa hivi majuzi tena bila shaka nahisi ni kwa mtu waliyekutana humu JF japo sina uhakika sana..

Vijana, hupaswi kucheza kamari katika afya yako huwezi kutumia kondom ni bora utulie maana hutapungukiwa na chochote kabsa.
Starehe ya dk 10 isikufanye ujutie maisha yako yote.

Leo utaona kuwa ni jambo dogo ila siku yakikupata ya kukupata utasaga meno.

Acha niishie hapa.
 
Mwaka 1983 ukimwi ndio unaingia Tz kutoka Uganda kupitia mto ngono alongside kijiji cha katerero ila mpaka mwaka 1986 takwimu zaonyesha TZ yote ilikua imetapakaa Gonjwa tayari.
Unaweza ona jinsi gani wazee walikua serious kwenye ishu ya kugege...na

Watu 10000 kila siku wanakadiriwa kuambukizwa Gonjwa
 
Hatufanyi tena Mwili-bet.
Tumeshashtuka zamani sana aisee!

Simba mwenda pole ndiye mla nyama.
Sasa Ukimwi ulikuwa kimya sana ila watu walijisahau na kujua labda umepata tiba au umesafiri kwenda kwa Mfalme Mswati.

Tuwe makini tutateketea wakati sisi ndiyo tegemezi katika mechi za nyumbani na ugenini.
Taifa bado linatuhitaji zaidi.
 
@SK2016,Kabsa huu ugonjwa ni hatari kuliko watu wanavyofikiria.
Maisha ni matamu sana ukiwa mzima wa afya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom