Siku ya wanaume duniani

Jtee

Senior Member
Dec 27, 2022
186
297
Ikiwa leo ni siku ya wanaume duniani...
Wakati ambapo wasichana/wanawake wanaamshwa kwa makongamano na semina za kuwainua kiuchumi. Mikutano na mijadala yenye kuwajengea kujiamini na kujitegemea. Warsha na vikao vya kuwajenga kiimani...

Vijana wengi wa kiume/wanaume wameachwa nyuma mno. Kama vile siyo binadamu katika jamii. Hawaandaliwi hata kisaikolojia tu juu ya namna wanavyopaswa kukielewa na kuishi na kizazi hiki kipya cha wanawake hawa ili kwenda nao sambamba.

Afya ya akili inapaswa kuwa mada ya kipekee kwa wanaume. Wao kwa wao na jamii kwa wao. Wengi wanapambana na mizigo mizito sana wanayotakiwa na jamii kuibeba kimyakimya.

Ni vema jamii ikakumbuka kumpa mwanaume hata nafasi ndogo ya kueleza madhila yake kwa uhuru. Magonjwa yaletwayo na Depression hayajui wewe ni mwanaume au mwanamke. Yanamkuta yeyote. Hushangai idadi kubwa ya watu wanaojiua au kufa mapema ni wanaume.

Wapo wanaume na vijana wa kiume wanaopitia mitihani na magumu mengi, unyanyasaji na ukatili mkubwa. Hawa ni binadamu kama wengine. Wanahitaji nafasi ya kujieleza bila kuhukumiwa, kusikilizwa bila kudhihakiwa, kufarijiwa, kusaidiwa kisaikolojia nk.

Kuna wakati hata mara moja tu mwanaume akirudi nyumbani. Pasipo sababu mkumbatie tu umpe pole na asante kwa uwepo wake na kutambua juhudi zake katika kuhakikisha ndani kuna chochote kinapatikana mezani na kuna usalama na amani. Itamfariji sana kiakili.

Kuna wakati mtazame kaka yako anayekupambania mwambie AHSANTE. Mwonyeshe unaziona juhudi zake hata kama ni wajibu wake.

Kuna muda mwambie baba, wewe ni bora sana kwa hiki unachotufanyia. Maisha si rahisi, hata akiwezesha chai kavu mezani mshukuru.
Tee nasema Maisha sio rahisi

Idadi ya watoto wa kiume wanaolawitiwa inapanda. Wanasaidiwa vipi? Hawa ni wanaume wa taifa la kesho. Tuna mijadala ya kuwalinda? Wanaume kwa wanaume mnahitaji kuzungumza.
Nimewaza sana hili

Vijana wa kiume wanaotumikishwa kinyume cha sheria na utu. Hawa wanalindwa na nani? Wanasemewa na nani? Wanatetewa na nani?

Vijana wetu mitaani tunawakumbuka vipi kuwajenga kiimani, kisaikolojia na kiuchumi? Na wao wana hofu nyingi nafsini wanazozificha kwenye kivuli cha uanaume lakini matokeo ya hofu hayajifichi ata siku moja.

Ziko wapi warsha, semina, mikutano na makangomano yenye kuwaleta wanaume pamoja ili kukuza na kuboresha connection, uchumi, afya ya akili, exposure, uhusiano, imani, mitazamo na hata kujadili kwa uwazi maovu yanayotendeka katika jamii nk.

Ziko wapi!?

Zaidi, katika jamii yenye kuwatazama wanaume kama viumbe wa ovyo(Ajabu leo status za wanawakeWanaume ni ... NO Ikumbuke wanaume wema wapo.

Baraka nyingi...
Kwa wanaume wanaojitambua, wastaarabu na wenye kujiamini.

Kwa wanaume wenye utu ndani yao. Wasionyanyasa wala kudhalilisha hisia au utu wa mtu.

Kwa wanaume wanaolinda na kuheshimu wanawake na watoto.

Kwa wanaume wanaopambania familia zao usiku na mchana. Natambua kuwa mwanaume si kazi rahisi hata kidogo.

Kwa wanaume wanaolea watoto wao na wasio wao. Wamevaa uhusika wa ubaba japo wao pengine ni kaka, baba wa kambo, baba mkubwa, au mjomba tu.

Kwa wanaume wanaojinyima mengi kwa ajili ya wapendwa wao. Anaacha kununua shati, mtu mwingine apate alichomwomba.

Kwa wanaume wenye kupambania Jamii/Taifa/Nchi mambo yakae sawa. Heshima kwenu.

Kwa wanaume wenye kumjua Mungu.

Kwa wanaume wenye kuyajua na kuyaishi mahaba. Wenye kujua kuyapokea na kuyatoa.

Kwa wanaume waliopitia magumu ila nafsi zao hazina chuki wala vinyongo.

Kwa wanaume watafutaji na watoaji.

Mungu awabariki sana!
Nawapa Maua yenu…

 
Back
Top Bottom