Tahadhari: Mbinu mpya wizi wa pesa vijana wanaosajili laini za simu

Huu mchezo ulioelekeza hapo juu waliutumia kumpiga laki 7 mfanyabiashara mkubwa sana pale mafinga ..maana yeye alizoea wateja wakimtumia pesa anaziacha humo humo kwenye simu afu ndiyo anawatumia mzigo ...kilichompata sidhani kama atakuja kusahau.
 
Hii Ni kweli kabsaa Nina shuhuda mbili,
1. Mama mwenye nyumba wangu aliibiwa na hawa wasjili laini walihamisha pesa zake ,
2.jamaa angu aliibiwa 500000 kwa Mara ya kwanza Kisha 76000.aliwaambia anataka kupata lipa namba akawapa smu wakacheza na simbanking wakawa wanaamisha pesa kdog kdog mpak 500000 .
SKU alipoenda kutoa pesa ndo akagundua ,akawa bdo hajajua Kama washa hack account yake ya bank akaweka Tena 76k wakapita nayo.

Kwa ufupi uskubali kuhudumiwa huduma za kimtandao na wapita njia Ni wezi sanaaa ,na hata ikitokea tatizo hujui pakuwapata .
Pia simbanking Ni nzuri Ila inahitaj umakini Mana simbanking huwa wantuma sms hta ya namba yako ya siri ko mtu akichukua smu yako akasima umeishaa. Mi stumii simbanking Mana nkiweka Ela huwa stoi mpak dharura kubwa ela za kutumia naacha kwa smu tu.
 
Teknolojia mpya zinakuja zikiwa na faida na hasara zake, hii ni mojawapo ya hasara zake. Umakini mkubwa Sana Unatakiwa muda wote.
 
Sema sisi wabishi sana ndio maana tunapigwa, kila siku kampuni za simu na police wanasema kupitia sms kuwa hupaswi kufanya hivi lkn hatuelewi.
Si sms za mitandao ya simu zikiingia, akiangalia pale juu akaona sijui voda anamark as read au anaifutilia mbali.
Wengine washabloc kitambo hizo no za taarifa na mafunzo ati ni usumbufu.
 
Hapo cha kufanya ni mitandao ya simu isiruhusu screen record kwenye apo zao.
Hii itasaidia usalama wa mtumiaji maana kuna app haziruhusu screen record na screenshot
 
5G ni hardware? Ama mimi ndo sielewi haya mambo
 
5G ni hardware? Ama mimi ndo sielewi haya mambo
Yes, 5g inawezeshwa na hardware(chipset) ya smu yako. Kama smu yako ina processor yenye uwezo wa ku support 5g, then ukitumia line ya 5g itafanya kazi. Not otherway round.
 
Watanzania wengi kutafuta maarifa madogo madogo ni wavivu sana..

Mtu ana simu kali ila hajui hata offline mode ni kitu gani?
Mwingine anakwambia nifungulie e-mail kwenye simu,tena password anasema weka no yangu ya simu ya airtel...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…