Tahadhari leo kwa wateja wa M-PESA.

Tahadhari leo kwa wateja wa M-PESA.

Leo nilikuwa nahamisha pesa kiasi cha 500,000/= kutoka kwenye akaunti yangu ya M-Pesa kwenda Tigo-Pesa nikapata message hii,

"Samahani, muhamala wako haukukamilika kwasababu za kiufundi. Tafadhari wasiliana na huduma kwa wateja".

Nilipoangalia salio pesa ikawa imekatwa lakini haijafika kwenye akaunti ya Tigo pesa, nilipopiga Huduma kwa wateja wakasema kuna matatizo ya kiufundi NISUBIRI MASAA 72 yaani siku tatu.

Hiyo mitambo inaweza kukata pesa tu isitume? kama ina tatizo kwanini isikatae kukata pesa mwanzoni kabisa? na kwanini wakae na pesa yangu masaa 72 bila riba kama sio wizi ni nini.

Yaani hapa nimechoka na pesa ilikuwa ya kusafirishia msiba.
Kukatwa bila kutumwa inawezekana
 
Hata sisi huwa tuna tuma pesa zetu kwa Latinos system hizohizo unazo tumia wewe na kwamafanikio makubwa changamoto ya siku moja isikufanye usahau umuhim wa hiyo mitandao
Na sisi wateja wasisahau umuhimu wetu kama kuna tatizo lazima tuwaambie, halafu ujue hatutumii mitandao yao bure kila transaction wanakata pesa ndefu tu.
 
Hill tatizo liliwahi kunitokea nilituma pesa kutoka m pesa kwenda tigo pesa nilituma Alhamisi waliniludishia Jumatatu
Ukute pesa uliokuwa unaitegemea ndiyo hiyo.
 
Daaaahh yn ingekua ni mim, kwa jinsi nivo na hasira kama za kwale.....ningepiga piga ukutani mpka ningekufa.......laki tano!!!!!!?????
 
Pesa huwa haipotei kwa Mpesa, itarudi tu mkuu vuta subira wa confirm, au ipo pending
 
Jambo tusiloelewa wengi wetu ni kuwa:- tiGo pesa inasumbua sana kupokea pesa kutoka mitandao mingine. Mimi ilinitokea hivyohivyo nilipotuma pesa Airtel kwenda tiGo pesa. Katika hili sitathubutu kuwanyooshea kidole M-pesa maana nawafahamu vzr, huduma zao upande wa kipesa ni bora zaidi ya huduma zote hapa nchini. Tigo wanapaswa kujitafakari na kulifanyia kazi hili maana hata ukitoa pesa Benki kwenda tiGo pesa mara nyingi tatizo kama hili hujitokeza.
 
Nilijuta na sitarudia kuhamisha pesa kutoka M-Pesa kwenda Tigo pesa hii huduma haijawahi kwenda vizuri kwangu.
 
Leo hata Tigo ni balaa, hapa bado nasubiri pesa iliyotumwa toka Bank iingie... ni zaidi ya masaa mawili sasa!
hii ya kuhamisha toka benki ilisha nitokea nimehamisha vi thilingi (sio sh.) naona muhamara unazingua mwishoni ile kulala kuamka kitu cha laki 4 kimejaa (nilifanya mara 4 kutoa thilingi laki 1) nikashidwa zirudisha na matumizi yangu ya hovyo nkaishia ziharibu tu
 
hii ya kuhamisha toka benki ilisha nitokea nimehamisha vi thilingi (sio sh.) naona muhamara unazingua mwishoni ile kulala kuamka kitu cha laki 4 kimejaa (nilifanya mara 4 kutoa thilingi laki 1) nikashidwa zirudisha na matumizi yangu ya hovyo nkaishia ziharibu tu

Uwiii.... ikitokea hivyo nitakuwa nimeshamaliza akiba yote niliyodunduliza...... dah.... unaharibiwa mipango hivi hivi unajiona..... dedeeeek
 
Ilikataa. Network problem.
Siku zote ukiona kuna network problem usiendelee kufanya miamala mpk network itakapostablelize... ukiondoa usumbufu ulioupata pesa yako iko salama. Nimeshakutana na ishu kama hizi mara nyingi... nazungumzia uzoefu, sio utaalam.

Pole sana kiongozi
 
Back
Top Bottom