SNAP J
JF-Expert Member
- Dec 26, 2013
- 7,106
- 8,044
Kama unajijua uu miongoni mwa wenye tabia ya kupenda kuopoa "visu vikali"karibu kwenye kila kumbi za starehe especially night club, basi hii habari inakuhusu.
Mchizi mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja jiji Nairobi, nchini Kenya alijihisi ni miongoni mwa wenye bahati usiku wa wikiendi moja katika night clubu moja( jina kapuni) ya jijini humo baada ya kuopoa ''kifaa kimoja cha ukweli''. Kama ilivyo ada, jamaa huyo alianza kukihudumia kifaa hicho usiku huo kwa kukinunulia bia kadhaa na hata kuanza kuvuta nacho "shisha" na kuanza kujifyatua nacho "selfie" za kutosha.
Lakini jamaa huyo aliona hiyo haitoshi, ambapo aliamua kuanza kuzi upload picha hizo katika mitandao mbalimbali ya kijamii ili kuujulisha ulimwengu ni jinsi gani anavyokula bata na kimwana huyo mkali.
Waswahili husema jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza , jamaa bila ya kujua yupo na mtu wa aina gani aliendelea kujivinjari na mtoto huyo mkali mpaka mida mibaya..
Kunako Alfajiri na mapema, habari na picha za ''blaza meni'' huyo zilianza kusambaa kwa kasi ya ajabu, kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha jamaa huyo akiwa kalala usingizi wa pono chooni, huku akiwa hajitambui.
Baadhi ya mashuhuda walioshuhudia mkasa huo walisikika wakisema jamaa atakuwa aliwekewa ''madawa'' kwenye kinywaji moja ya kinywaji chake usiku wa jana yake. Jamaa alipokuja kuzinduka, huku akionekana kama mtu aliyechangayikiwa baadaye alisikika akilaumu amelizwa na yule binti vitu vyake vya dhamani ikiwemo simu, wallet.., saa, pamoja na raba zake kali.
Mpaka sasa demu huyo mkali wa viwanja anasakwa na polisi kwa udi na uvumba bila ya mafanikio kwani inasemekana ndio mchezo wake, na ameshawaliza wanaume kibao tu jijini humo kwa style yake hiyo.
BEFORE.
AFTER.