Mtoa Taarifa
Member
- Sep 21, 2024
- 90
- 252
Mtu mmoja aliyedaiwa kuwa ni Afisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Derick Derick Junior (36) amefikishwa katika Mahakama ya Kinondoni akikabilia na mashtaka mawili ikiwemo kutishia kwa silaha.
Mshtakiwa amefikishwa mahakamani hapo leo, huku akisomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Hakimu Mfawidhi Is-haq Kuppa huku aliyejeruhiwa pia akifika mahakamani hapo.
Inadaiwa alitenda makosa hayo Oktoba 27, 2024 maeneo ya Masaki ‘1245 night club’ Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo alimjeruhi kijana Julian Bujuru kwa kumpiga na kitako cha bastola.
Pia inadaiwa alimjeruhi Julian Bujuru sehemu ya jicho na pua.
Soma Pia: Polisi wamtia mbaroni anayedaiwa kuwa "Afisa Usalama" aliyemjeruhi raia kwa 'kitako cha bunduki'
Baada ya mshtakiwa kusomewa mashtaka hayo alikana makosa, huku mahakama ikimpa masharti ya dhamana ya mtumishi wa umma atakayesaini bondi ya Shilingi Milioni Nane.
Mtuhumiwa huyo alitimiza masharti hayo ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 20, 2024 itakapoitwa tena mahakamani kwa ajili ya kutajwa.
Hata hivyo mtuhumiwa aliweza kutokea mlango wa nyuma ili kukwepa mapaparazi ambao walijipanga maeneo hayo.