Tahadhari kwa wanaume wanaosafiri nje ya nchi... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tahadhari kwa wanaume wanaosafiri nje ya nchi...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtoboasiri, Apr 16, 2011.

 1. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Wana JF,

  Hii ni maalum kwa wanaume wanaosafiri nje ya nchi yetu ama kikazi au kimasomo hasa safari za muda mfupi (mwezi na chini ya hapo). Kuna tukio limetokea usiku wa kuamkia leo. Samahani sitataja jina la muhusika wala mji yalikomkuta, ila nimehakikishiwa na chanzo cha kuaminika kilicho kwenye sehemu ya tukio. Kisa kiko namna hii:

  Kuna Mtanzania mwenzetu (ni mtu wa makamo na kiongozi kwenye moja ya taasisi zetu za fedha) alikuwa na safari kwa short course ya wiki moja. Jana (siku moja kabla ya shule kwisha) akaenda na mwenyeji wa hiyo nchi na mji usiku kwenye masanga, huko akapata timu pinzani ya mechi ya mchangani na akamleta hotelini alipofikia. Binti akang'ang'ana kuwa hawezi kwenda peke yake, ni lazima aende na mwenzie. Mzee akamshirikisha na mwenzie (Mbongo pia) ili akubali kuondoka na ule mzigo mwingine. Jamaa namba mbili akakubali, wakawachukua hao "Chips funga" kama Watani zetu wa jadi (Wakenya) wanavyowaita.

  Asubuhi ya leo walinzi wa hoteli (ona tofauti ya hoteli zetu na wenzetu) wakawasimamisha wale wadada getini kwa upekuzi na wakawakuta na laptops za jamaa. Wakawashitukia, (hoteli hiyo ina utaratibu kuwa mgeni akija na laptop inasajiliwa, ukitoka unaonyesha risiti ya laptop uliyopewa wakati wa kuingia). Kuangalia details, ni laptops za Wabongo. Walinzi wakawashikilia wadada ili kuhakikisha usalama wa wateja wao. Piga simu za vyumbani weee! Hakuna majibu, wakaita polisi (wadada wakiwa bado wamezuwiwa wasiondoke), kufungua milango kwa master key, HAMAD! Jamaa wako uchi wa mnyama hoooi wanakoroma, kuwaamsha hawaamki. Kuwapekua wadada wana dola 3,500 na Shilingi kadhaa za kibongo (mbali na laptops).

  FUNDISHO

  Wanaume kwani ni lazima tutafute totoz ughaibuni hata ukimwacha mamsap kwa wiki moja tu?

  NA NYIE WADADA,

  Kwani ni lazima ukombe kila kitu? Si angalau tunza utu wa huyo unaemkomba ukichukulia ulipata "service" hata kama haikuwa ya kuridhisha?
   
 2. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #2
  Apr 16, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...mtoboasiri acha hizo bana, unamwaga punje kwa kuku wengi.
  mgeni kukarimiwa ni kawaida, hata wao wakija Bongo wanapewa
  'escorts'

  Anyway, thanks kwa tahadhari.
   
 3. M

  Mkare JF-Expert Member

  #3
  Apr 16, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haya, nitawaambia....
   
 4. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  Duh!
  Mijanaume mingine haiwezi kuvumilia hata siku moja. Kama vile wana kale kapepo.
   
 5. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #5
  Apr 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Ningebeba na mashuka..
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Apr 17, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,499
  Likes Received: 19,914
  Trophy Points: 280
  hahahhahahh! wewe binti una mambo, utasababisha nikutafute buree):):)
   
 7. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #7
  Apr 17, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Hahha hahha yaani nimecheka jamni acha tu we kiboko
   
 8. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #8
  Apr 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Kwanini ubebe nusu nusu
  ukifanikiwa kupita umefaidi zaidi..
  ukikamatwa umekamatwa kweli..
   
 9. M

  MagMat Member

  #9
  Apr 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 51
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 15
  Du asante kuliweka wazi hilo ni kweli hasa mademu wa hapo bondeni usiguse mi iliwatoke jamaa wanne tukiwa nao na mmoja tu ndo vitu vyake vilipona, please watanzania tuwe makini na tujiepushe make wale vikuku walikuwa wanasema ''Tanzanian are very kind'' pengine walimanisha warahisi kukamata who knows? Cha ajabu hata mwenyeji wetu ambae ni mtanzania lkn anaishi huko siku nyingi nae chaaliii
   
 10. c

  chui New Member

  #10
  Apr 17, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wandugu hilo haliko Ughaibuni pekee, mbona hata hapa Bongo yanafanyika sana? Ni mtindo kwa akina dada wenye njaa kali!
   
 11. Likasu

  Likasu JF-Expert Member

  #11
  Apr 17, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  AD wee kiboko.
   
 12. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #12
  Apr 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  siachi kitu mkuu..
  sabuni ya kunyolea ndevu..
  ntakachouza na kitaniingizia shilingi na beba..
   
 13. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #13
  Apr 17, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,828
  Likes Received: 930
  Trophy Points: 280
  Haya mambo yako sana Manzini ukienda macho juu inakula kwako
   
Loading...