Tahadhari kwa Chadema!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tahadhari kwa Chadema!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Butola, Apr 27, 2011.

 1. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,222
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Itashangaza CHADEMA kikipoteza nafasi hii adimu!

  Lula wa Ndali-Mwananzela​
  Aprili 20, 2011[​IMG]
  [​IMG]CCM imeanza kuteka hoja zao, moja baada ya nyingine

  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kisipotumia nafasi hii ya kisiasa kukidhoofisha chama tawala (CCM) na hatimaye kujijengea mazingira ya kuweza kushinda vizuri katika uchaguzi mkuu ujao, kitakuwa hakina mtu wa kumlaumu isipokuwa chenyewe.

  Katika ufuatiliaji wangu wa siasa za nchi mbalimbali za Kiafrika, naweza kusema, pasipo shaka, kuwa hakuna chama kilichopendelewa kwa kupewa nafasi lukuki za kujijenga na kubomoa chama tawala kama CHADEMA.
  Nafasi ambazo kina Kibaki na Raila walipewa wakati wa kuimong'onyoa KANU kule Kenya zinafanana kwa mbali tu nafasi ambazo CHADEMA hapa Tanzania kimepata kuweza kuiletea matatizo CCM. Hili ni kweli pia ukilinganisha na nafasi walizozipata kina Bakili Muluzi kule Malawi au kina Chiluba kule Zambia.

  Vyama hivyo vya upinzani kwenye nchi hizo havikupata nafasi nzuri za kisiasa kuweza kuwashawishi wananchi kuigeuka serikali kama zile nafasi ambazo zimeiangukia CHADEMA.

  Kwa muda mrefu CCM imekuwa ikijitahidi kujichimbia kwenye shimo refu la matatizo ambamo kwa kadri kina chake kilivyozidi ndivyo ilivyokuwa vigumu zaidi kwa CCM kutoka ndani yake. Sihitaji kurudia mlolongo wa kashfa mbalimbali, sheria mbovu mbalimbali au maamuzi mabovu yaliyoligharimu taifa kiasi kikubwa. Mambo mengi tayari yanajulikana na hakuna lililo geni.
  Na nafasi hizo zilikuwa zifikie kilele chake kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2010 ambapo CHADEMA kama chama kilichokuwa na mvuto wa pekee (baada ya CUF kupatana na CCM) kilihitaji kutumia nguvu ya ziada tu kuhakikisha kuwa CCM haitoki kwenye shimo hilo ambalo kimechimba chenyewe.
  Mtu yeyote ambaye anafuatilia siasa anaweza kukubaliana nami kuwa kwa karibu miaka 15 ya vyama vingi, hakuna nafasi ya pekee ya kuiondoa CCM madarakani kama ile iliyoletwa na kimbunga cha historia katika uchaguzi wa mwaka jana.

  Kwamba uchaguzi wa mwaka jana ulikuwa ni nafasi pekee halina utata. Sote tuliofuatilia kwa karibu siasa za uchaguzi na hata ambao tulithubutu kuunga mkono na kuipigia debe CHADEMA tuliamini kuwa njia pekee ya kuweza kuleta mabadiliko ya haraka katika taifa letu ni kubadilisha chama kilicho madarakani na kwa kufanya hivyo kubadilisha sera zinazotuongoza na pamoja nazo kufanya mabadiliko makubwa ya kisheria ikiwemo kusimamia kwa haraka mchakato wa kupata Katiba Mpya ifikapo 2015.
  Hata hivyo, matokeo ya uchaguzi ule na hasa kampeni yake ilivyoendeshwa, matokeo yalivyogombewa na mwitikio wa baadaye, umetufanya wengine tuamini na kushukuru kuwa ni vizuri CHADEMA haikuweza kushinda nafasi ya urais.

  Si kwa maana ya kufurahia kwamba haikuwa hivyo; bali ni kwa sababu tunaweza kuona wazi zaidi kuwa ukiondoa Dk. Slaa na kundi la watu wachache sana ndani ya CHADEMA, watu wengine hawakuamini na hawakuwa tayari kuona CHADEMA inashika dola ya nchi.

  Kundi hili kubwa ndani ya chama halikuweza kupima joto la uchaguzi vizuri na badala yake liliweka msisitizo wake mkubwa kwenye kupata wabunge wengi ili hatimaye waweze kupata nafasi ya kuwa chama kikuu cha Upinzani Bungeni na wengine kuweza kushika nafasi za "uongozi wa Upinzani" Bungeni. Matokeo yake ni kweli nafasi hizo zilipatikana na CHADEMA ikawa chama kikuu cha upinzani nchini. Lengo la kundi hili likawa limefikiwa.
  Hata hivyo, lengo hilo halikuendana na lengo la Watanzania karibu milioni 2.3 ambao walitaka Dk. Slaa awe Rais wao. Rais Kikwete alirudishwa na Watanzania wapatao milioni 5.3 hivi ukilinganisha na milioni karibu 9 waliomchagua mwaka 2005. Watu wengi wanaangalia anguko la asilimia 20 kutoka asilimia 80 ambazo alishinda nazo kuja asilimia 61.
  Anguko hilo halioneshi hali halisi; kwani kutoka wapiga kura milioni 9 na kupata wapiga kura milioni 5.3; kwa idadi ya watu ni kuwa asilimia 41 ya watu waliomchagua Kikwete mwaka 2005 hawakurudi kumchagua tena 2010!

  Haikuwa nafasi ndogo hiyo. Lakini hatuwezi kuilaumu Tume ya Uchaguzi kwa mapungufu yote yaliyotokea. CHADEMA kama chama cha upinzani kilikuwa kinajua kwa uhakika kabisa kuwa Oktoba 2010 kungelikuwa na Uchaguzi Mkuu.

  Haikuwa siri. Walijua kabisa mfumo wa kutangaza matokeo na kuhesabu kura ulikuwa ni mbaya kwani tayari waliushuhudia ukiwanyanyasa Kiteto, Tunduru, Tarime, na sehemu nyingine kadha wa kadha. Hawawezi kulalamikia CCM kuwa inatumia vyombo vya dola vibaya kwani walikuwa wanajua kabisa hilo lilikuwa linatarajiwa.

  Lakini walienda kwenye Uchaguzi Mkuu wakiombea kuwa CCM itabadilika. Waliamini kabisa kuwa ‘CCM imejivua gamba' na hivyo ingeweza kuona serikali yake inaendesha uchaguzi katika mazingira ya uwazi, haki na usawa. Sasa mambo yalipobadilika baadhi ya watu wakawa wanalalamikia "uchakachuaji". Lakini sisi wengine tuliendelea kushangaa; walitarajia nini? Kweli walitarajia CCM ingeacha au kutengeneza utaratibu ambao ungesababissha chama hicho kiondolewe madarakani kirahisi kiasi hicho?
  Ni kwa sababu hiyo, basi, tunapozungumzia kuelekea 2015, nafasi iliyobora zaidi ya kuleta mabadiliko nchini imepotezwa. CCM imeanza kujinyanyua kutoka kwenye shimo lake! Baadhi ya watu wanataka isitoke shimoni au hawaamini kuwa inaweza kutoka. CCM imejionesha kuwa inaweza kwa kutumia hata mbinu za ukinyonga ikabadilisha rangi yake ikafanana na udongo na watu wakadhania imetoka shimoni!

  CHADEMA bado sijashawishika kuwa inaelewa tatizo lililoko mbele yake. Ndugu zangu, CCM baada ya kuteka hoja ya Katiba Mpya, ikateka hoja ya mswada wa kusimamia mchakato wa kuelekea Katiba hiyo mpya, na sasa imeteka hoja ya ufisadi. Sitoshangaa siku chache zijazo CCM hiyo hiyo ikaanza kuteka hoja za kuwajibishana, maadili, utendaji bora na kuanza kuonesha kutofurahishwa na yale yaliyomo kwenye ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali.


  Mtindo huu ambao CCM inautumia wa kuteka hoja za wapinzani unaitwa kitaalamu political triangulation. Ni mtindo unaotumiwa na chama ambacho kimepoteza mvuto na kinazidiwa hoja na wapinzani wake kwa kuanza kuzichukua hoja za upinzani, kuzipamba na kuzifanya kuwa hoja zake. Mbinu hii ilitumiwa vizuri na Bill Clinton kule Marekani, na hata Uingereza pia ilitumika katika uchaguzi wao uliopita. Mbinu hii ina lengo la kudhoofisha Upinzani kwa kuunyang'anya hoja.

  Hapa ndipo CHADEMA inajikuta kwenye matatizo; kwani itakapoamka asubuhi na kukuta hoja zake zote ziko mikononi mwa CCM (kina January, Nape na Mukama), itabidi wajiulize waje na lipi jipya!
  Hapo ndipo watajikuta kuwa wamepoteza mvuto kwa kubakia wafuataji badala ya kuongoza; kwani kama nilivyowahi kusema huko nyuma, usipoongoza utajikuta unafuata.

  Mikutano ya mikoani ni mizuri, lakini haiwezi kuwa mikutano ya kuwaeleza wananchi ubaya na matatizo ya serikali yao. Wananchi wengi Tanzania wanajua tatizo lao. Jamani, watu milioni 2.3 waliomchagua Dk. Slaa hawakuhitaji semina au warsha ya kuwaambia tatizo ni CCM.

  Watu hao walishajua tatizo lilipo na kuwarudia tena kujaribu kuwashawishi ni sawasawa na mhubiri anapoendelea kuihubiria kwaya yake badala ya watu hasa wenye kuhitaji mahubiri!

  CHADEMA isipoangalia na isipoanza kujipanga mapema zaidi, itajikuta inageuzwa kituko na kichekesho kwa muda mrefu na kubakia kuwa sehemu ya simulizi za siasa za Tanzania kwamba "hapo zamani za kale kulikuwepo na CHADEMA"!

  Kwa kadri viongozi wa CHADEMA wanavyoamini kuwa wanapendwa na wanakubalika na kwamba wananchi wanathamini mchango wao, na hivyo mambo yatakuwa vizuri tu, ndivyo hivyo mambo yatakavyozidi kuwa mabaya kwao.

  Ni mpaka pale watakapotambua kuwa miaka mitano kueleka uchaguzi mkuu ujayo imeshapungua kwa miezi karibu saba sasa ndio watajua wanakabiliwa na "udharura wa sasa." Kiongozi yeyote wa CHADEMA anayefikiria kufanya mabadiliko mwaka 2012 au mwaka 2013 ili afanye vizuri kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 anawadanganya wenzake!
  Nikiri ya kwamba, uharaka wa CCM kuanza mabadiliko ndani yake bila kuchelewa; japo kuwa ndio walifanya vizuri zaidi (japo siyo vizuri sana kuliko huko nyuma) kwenye uchaguzi uliopita, umenifanya nikubali kuwa wanamkakati wao wameelewa "udharura wa sasa".

  Wametambua kuwa hawawezi kusubiri uchaguzi wao mkuu wa 2012 kuanza mageuzi. Wametambua kuwa historia haiwasamehi wanaochelewa. Na kama wale waliojikuta treni la mabadiliko limeondoka kituoni, CCM wanakimbia na kutaka kudandia gari lolote la kujaribu kuwakimbiza kuliwahi treni hilo ambalo linazidi kuongeza mwendo.

  Wakati CHADEMA ikijiaminisha kuwa treni la mabadiliko ni lao kwa vile limeandikwa jina lao, wana uhakika kuwa hata wakifika kituoni wasipolikuta bado wanaweza kuliita likasimama na kuwangoja. Bahati mbaya CCM watakuwa wameshashika usukani, na CHADEMA watakapoanza kulikimbiza wapita njia watakuwa na kitu cha kucheka na kupiga gumzo.

  CHADEMA hawana nafasi kubwa ya kufanya vizuri kulinganisha na ile ya 2010. Hawana, hata wakijiaminisha kuwa wanayo. Ni jukumu lao kutengeneza nafasi hiyo mpya wao wenyewe bila kutegemea kile kinachofanywa na CCM.
  Hapo ndipo tutajua tofauti ya uongozi na ufuasi, siasa na porojo, uthubutu na woga! Huu ni wakati wa kutambua udharura wa sasa. Sio kesho, sio keshokutwa. Laiti wangejua….!
  [​IMG]  Itashangaza CHADEMA kikipoteza nafasi hii adimu!


  My take: Huu ni ushauri sahihi uliotolewa kwa wakati sahihi, Chadema ichukue hatua kabla majuto hajawa mjukuu!!
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Nimekuelewa ila ondoa unafiki sema A,B,C,D gani zifanywe na CDM na kivipi ili kuiweka katika nafasi saama zaidi.

  (point out the problems zisizo propaganda na utoe suluhisho za hayo matatizo)
   
 3. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,222
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Sasa unafiki wangu upo wapi tena mkuu?mie nilichofanya ni kuiweka tu hapa habari ya Lula wa Ndali Mwananzela kama ilivyo!!
   
 4. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,263
  Trophy Points: 280
  muambie mjumbe hauawi!asante kwa kushare.Ila hii trick ya ccm ya kutelekeza ilani yao na kuitekeleza ya chadema ni ya aina yake.kweli siasa mchezo mchafu!
   
 5. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  MIMI NIMEKUELEWA,UPANDE WANGU NAOMBA CHADEMA WASIRIDHIKE,SIO MAMBO YOTE YANAYOTOKEA CCM TUNAELEZWA,KUNA SIRI WANAONGEA NA HATUJUI:smile-big:
   
 6. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #6
  Apr 27, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,500
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ushauri wa kuwa cdm wasilale ni mzuri; lakini pia tunahitaji kujua cdm ifanye nini ili kura zisichakachuliwe?
  ccm ilitumia vyombo vya dola kuhakikisha watu wake wanatangazwa washindi; tunajua watu walipigwa mabomu, virungu, majiwasha nk ili wakubali matokeo yaliyochakachuliwa. Sasa cdm ifanye nini katika hilo?
  Tayari mchakato wa katiba mpya umeanza ambao utazaa katiba mpya na sheria nyingine zote kurekebishwa; lakini kama mwandishi alivyosema "...Kweli walitarajia CCM ingeacha au kutengeneza utaratibu ambao ungesababissha chama hicho kiondolewe madarakani kirahisi kiasi hicho?" ni wazi ccm hawako tayari; sasa tuwalazimisheje?
  Kenya yalitokea mauaji, je njia kama hiyo inatufaa? Mauaji ya Arusha hayajasaidia chochote; je tunaelekea wapi?
  Hatutaki vita wala mauaji, hivyo ni vyema mwandishi akaeleza mbinu mbadala zisizo na vurugu.
  CCM HAIWEZI KUTENGENEZA UTARATIBU WA KUSABABISHA IONDOKE MADARAKANI KIRAHISI......HIVYO!
   
 7. THE GAME

  THE GAME JF-Expert Member

  #7
  Apr 27, 2011
  Joined: May 30, 2010
  Messages: 441
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  ni ukweli ulio wazi kuwa ccm kwa vyovyote vile haiko tayari kuachia ngazi kirahisi,inatumia dola zaidi kujiweka madarakani.ufumbuzi ni sisi watanzania kuamka na kukataa kuendelea kuburuzwa kupitia njia mbalimbali mfana kuundwa katiba mpya,au ikishindikana tutumie nguvu ya uma.
   
 8. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #8
  Apr 27, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  katika hoja ya ufisadi chadema waendelee:
  1. kukandamiza kwa JK kutotenganishwa na maswahiba wake wakuu RA na EL aliowatetea wakati wa uchaguzi picha zake zitumike uwaelewesha wananchi, lazima afe nao kama anataka kuwaua.
  2. mafisadi kutolewa tu kwenye ccm haitusadii sisi watanzania hayo ni mambo ya chama chao sisi tunataka watu wanafikishwa mbele ya sheria na wanahukumiwa sawasawa na makosa yao vinginevyo huu ni usanii tu wa kuwafanya watanzania wajinga ambao hawawezi kufikiri.
  3. Pia chadema kila ccm wanapotekeleza walichowaamuru wafanye basi warudi kwa wananchi wawaambie kuwa kile tulichokuwa tunawalazimisha ccm wafanye wametii amri wamefanya ili chadema ipate credit na siyo ccm.
  4. Chadema lazima wawaambie wananchi kuwa ccm na serikali yao hawawezi kufanya kitu bila kulazimishwa hivyo hivyo kama si chadema basi mafisadi wangeendelea kula kuku tu huku wananchi wakilia njaa.
  5. Chadema komaeni na maandamano ya kuwalalzimisha serikali kushusha bei ya bidhaa kwa kufuta kodi, hii ndo itakuwa a big credit kwa chadema take action quickly before they respond to it because there is no way they can escape this.
  6. Pia chadema mnapofanya mikutano mpitie pia na kwenye baadhi ya vijiji ili mjitambulishe mijini watu wameshawajua sasa ni zamu ya vijijini ili watu wajue kuwa chadema ni ya watu wa hali ya chini siyo wasomi tu kama wanavyodanganywa na ccm.
   
 9. N

  Ndelamochi Member

  #9
  Apr 27, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimeupenda sana ndgu, Dr Slaa cdm should read this
   
 10. m

  mjombajona JF-Expert Member

  #10
  Apr 27, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 262
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Haya ni maneno makali na ya busara sana ... yafanyiwe kazi na CDM, yatawang'oa watawala 2015. Binafsi nakushukuru sana mkuu.
   
Loading...