Tahadhari: Jini la kike lazuka mitaa ya Kariakoo

Tahadhari: Jini la kike lazuka mitaa ya Kariakoo

nzalendo

Platinum Member
Joined
May 26, 2009
Posts
12,984
Reaction score
14,840
Hii imetokea jana baada ya watu wawili tofauti kupoteza kiasi kikubwa cha fedha mmoja alikuwa ana deposit NMB Kariakoo na mwingine CRDB Kariakoo,na wote kwa nyakati tofauti kabla ya kupoteza fedha hizo wanachokumbuka ni kuona mwanamke amejitanda baibui,wa NMB aliulizwa wapi naweza kubadili fedha za kiarabuu?

Hapo hapo akapoteza fahamu kuzinduka yuko mitaa ya kariakoo na hakumbuki kapoteza vp fedha. Wa CRDB nae aliulizwa kitu ambacho hakumbuki na pia kujikuta yuko nje ya benki.

Hii ni kwa kifupi Jumatatu kuna jamaa baada ya kulipwa fedha za kuleta mzigo Kariakoo alikutana na mwanamke mwenye baibui akamuuliza 'Uncle samahani hivi mawakala wa mpesa wako wapi?' Akajikuta yuko maeneo ya Jangwani na fedha zote za mzigo zimepotea.

Kaeni chonjo.
 
Kama ni hivyo inabidi tukiwa mitaa ya kati ya jiji, na ukiwa na pesa kiasi usiongee na mtu usiyemjua.
 
wakazi wa kariakoo,tarehe 25 nendeni mkapange foleni mpige kura.msipumbazwe na hoja za meleta mada ili muingiwe na hofu.
 
Hilo ni pigo jipya kwa mabosi akikutuma mzingo unakimbia akikuhuliza unamwambia nimekutana na mwamnamke bujibuji.



swissme
 
hilo jini sidhani kama litajichanganya kwangu mla kitimoto
 
umekusanyaje taarifa hz zote kwa maramoja mdau ama ni coincidence tu ukajikuta unatupa picture hii?!!!
 
Du...hapo sijui tunakaaje chonjo!!kutojibu tukiulizwa kitu au...nisaidie ninasafari ya kwenda kudepost

Nadhani ni vyema usifungue mdomo kwa mtu usiyemfahamu.
 
Back
Top Bottom