Tahadhari: Huu ni msimu wa nyoka!

Tahadhari: Huu ni msimu wa nyoka!

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,745
Reaction score
830,866
Wataalamu wa hali ya hewa na wanyama/wadudu kwa pamoja wanasema huu ni wakati wa majoka hasa jamii ya swira na hongo weusi kufuatia ongezeko la joto, hivyo majoka kutafuta makimbilio majumbani

Dondoo za usalama:

1. Epuka kuacha madirisha wazi kama hayana nyavu. Majoka kama swila na hongo wanaweza kukwea vimo virefu

2. Usiache mlango mkuu wazi jioni. Majoka huingia kimya kimya na kwa upole

3. Kabla hujaketi chini ya mti kivulini kagua matawi kama kuna majoka yamening'inia

4. Kagua kitanda na mazingira yake, swira hupenda kujiingiza kwenye mashuka kujipooza

5. Acha kukaa nje kama zamani kupunga upepo kwenye matandiko. Majoka yanapenda kuwinda usiku

6. Siyo nyoka tu wanatambaa na kuweza kukung'ata usiku bali hata tandu wenye sumu kali

7. Ondoa vichaka inayozunguka nyumba yako. Vichaka huvutia panya ambao ni chakula lishe kwa majoka

8. Nunua dawa za kufukuza nyoka mwaga kuzunguka boma, inaweza kufukuza nyoka kwa 90%

9. Ukiamua kumpiga nyoka uwe makini. Majoka yanaua. Nyoka aina ya hongo ('black mamba') akitishiwa atakukimbiza huku anakugonga. Sumu yake inaua ndani ya dakika 40.

Chukua tahadhari, huu ni msimu wa majoka. Ni joto sana na majoka yanakereka na kuudhika haraka.

Sambaza ujumbe huo kwa wote, ili kuokoa maisha.

Ernest Laizer

Kwa hisani ya watu wa mashambani na Health Safety and Environment (HSE)

ringel-schleiche2.jpeg
paarung-m.jpeg
sinai-cobra.jpeg
 
ngoja usiku niamke kimya kimya nafyeka haya maua ya mama wa nyumba yotee, au kesho nikanunue ile dawa ya kuyakaushaaa.

Na anavyoamini uchawi alooo mchungaji lazima amle kichwa, maana nishawahi ona kitu kinatereza tereza kwenye dirisha leo ndio nimegundua sio ndoto ilikuwa kifoo.

Ubarikiwe mkuu
 
kUNA NYOKA MWINGINE HATARI wengi hawamjui. Ni kama mwoga ila ukimchokoza ndio asili yake hujionyesha. Green Mamba ni yule nyoka wa kijani. Sifa zake ni kama Black Mamba. Ila Wengi humuita nyoka wa kijani. Ni mpole na kama mwoga vile mana unaweza mkaribia yeye akakukimbia. Ila ukimfuatilia zaidi au akajua unataka kumdhuru ndio dhoruba yake huanzia hapo. Tabia yake inakuwa kama Black mamba.
 
ngoja usiku niamke kimya kimya nafyeka haya maua ya mama wa nyumba yotee.....
Au kesho nikanunue ile dawa ya kuyakaushaaa....
Na anavyoamini uchawi alooo mchungaji lazima amle kichwa....
Maana nishawah ona kitu kinatereza tereza kwenye dirisha leo ndio nimegundua sio ndoto ilikua kifoo..

Ubarikiwe mkuu
 
Noma sana huyo namuongapa kuliko black mamba,

State agent
kUNA NYOKA MWINGINE HATARI wengi hawamjui. Ni kama mwoga ila ukimchokoza ndio asili yake hujionyesha. Green Mamba ni yule nyoka wa kijani. Sifa zake ni kama Black Mamba. Ila Wengi humuita nyoka wa kijani. Ni mpole na kama mwoga mana unaweza mkaribia yeye akakukimbia. Ila ukimfuatilia au akajua unataka umdhuru ndio dhoruba yake huanzia hapo. Tabia yake inakuwa kama Black mamba.
 
Back
Top Bottom