Tahadhari: CCM, Msikilizeni Sumaye

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
17,882
13,171
Maoni yaliyotolewa na Mh F Sumaye, pamoja na kushindwa kupata U-NEC, ni wake up call kwa CCM.
Sina uhakika kama Mh Sumaye angetoa maoni hayo kama angeshinda kinyang'anyiro hicho cha kugombea U-NEC.

Hata hivyo kwa wanacha waaminifu wa CCM aliyosema Mh Sumaye ni common knowledge, ufisadi utaiangamiza CCM kama chama cha siasa makini.

Nimeona maoni kama haya haya ya mtoa mada ambaye vile vile inaelekea ni mwana CCM:
Chama kikongwe cha siasa nchi Tanzania CCM kinazidi kupoteza demokrasia ndani ya chama chake,ama kwa makusudi au kujisahau.Namaanisha kutokana na staili yake inayofanyika katika chaguzi zake za ndani ya chama.Tumeona rushwa,udini na ukabila umeendelea kushika kasi na kukitesa chama hiki kikongwe nchini.

Yaliyotokea huko Shinyanga ni mfano mzuri wa CCM kujimaliza ama kujikaanga kwa mafuta yake yenyewe.Kampeni za ujumbe wa NEC kupitia wilaya kwa wilaya ya Shinyanga mjini imekitia doa chama hiki kwa kampeni chafu za ukabila na rushwa huku wagombea wakijinadi wataimaliza CHADEMA kwa kutumia nguvu yao ya kifedha na kiutawala kuelekea uchaguzi wa 2015.

Uchaguzi umezidisha makundi yanayo hasimiana ndani ya chama.Pia chaguzi hizi zimeibua chuki miongoni mwa wanachama hususani wale wanao kikosoa chama, kwa majina yao kufyekwa na sekretarieti ya chama,huku majina mengine yaliyofyekwa huko wilayani yakirudishwa mfano jina la Mary Nagu.

Hali hii imesababisha sintofahamu ndani ya CCM kutokana na staili yao ya kujilimbikizia madaraka kitendo kinachooneka mtu mmoja kuwa viongozi ndani ya jamii kama vile hakuna watu wenye sifa za kushika nyadhifa ambazo mtu mmoja anatunukiwa.

Janga lingine ni kuondoa kundi ambalo limekuwa wasemaji wasio ogopa kukisema chama chao kwa kufuata misingi ya kiongozi akubali kukosoa na kukosolewa.Hali hii imesababisha baadhi ya wabunge majina yao kukatwa kwa vile tu walionyesha msimamo wao wakati wa kumpinga Waziri mkuu kwa kusaini kwenye fomu ya kutafuta saini 70 za Zitto Kabwe za kutaka kumng'oa mtoto wa mkulima.

Pia chama hiki kimekuwa kokoro katika uchaguzi zake kwa kuzoa hata wale waliopoteza sifa ndani ya jamii husika ama kwa vitendo vya rushwa ,ukatili na hata uharamia kitendo kinachosababisha chama hiki kushindwa kujitenga na kauli ya wapinzani kwa kukiita Chama Cha Majambazi.

Mwisho ,kauli ya Sumaye aliyekuwa wazir mkuu kwa kipindi chote cha serikali ya awamu ya tatu kuutangazia umma kuwa CCM ina nuka rushwa ni pigo kubwa kwa mustakabali wa CCM kuelekea uchaguzi mkuu,kauli ya Sumaye si ngeni masikioni mwa Watanzania kwani hata Mh. Makongoro Nyerere aliwahi kulalamika katika harakati zake za kuusaka ubunge wa EAC.Ni wakati sasa wa kujitazama na kuangalia wapi wanacheza karata zao vibaya na kutafuta karata turufu na kucheza kadi vizuri.

Nimesoma gazeti la NIPASHE leotarehe 9 Oct. 2012, Katibu Mkuu Mukama akijibu tuhuma za Sumaye kuwa azipeleke kwenye vikao husika.Tunasahau kuwa waamuzi wa mustakabali wa chama ni wanachama wanaoona yanayoendelea hukohuko mitaani.
Tumeona jana ngumi na kurushiana viti katika kikao cha uchaguzi huko Musoma, sababu ikiwa hiyohiyo rushwa.

Mukama akisubiri kuletewa hoja ofisini, basi uhalali wa chama kwa wanachama wake utaendelea kushuka.

Wahenga walisema mwenye masikio na asikie!
 
Maoni yaliyotolewa na Mh F Sumaye, pamoja na kushindwa kupata U-NEC, ni wake up call kwa CCM.
Sina uhakika kama Mh Sumaye angetoa maoni hayo kama angeshinda kinyang'anyiro hicho cha kugombea U-NEC.

Hata hivyo kwa wanacha waaminifu wa CCM aliyosema Mh Sumaye ni common knowledge, ufisadi utaiangamiza CCM kama chama cha siasa makini.

Nimeona maoni kama haya haya ya mtoa mada ambaye vile vile inaelekea ni mwana CCM:

Nimesoma gazeti la NIPASHE leotarehe 9 Oct. 2012, Katibu Mkuu Mukama akijibu tuhuma za Sumaye kuwa azipeleke kwenye vikao husika.Tunasahau kuwa waamuzi wa mustakabali wa chama ni wanachama wanaoona yanayoendelea hukohuko mitaani.
Tumeona jana ngumi na kurushiana viti katika kikao cha uchaguzi huko Musoma, sababu ikiwa hiyohiyo rushwa.

Mukama akisubiri kuletewa hoja ofisini, basi uhalali wa chama kwa wanachama wake utaendelea kushuka.

Wahenga walisema mwenye masikio na asikie!

Sidhani kama kulikuwa na haja ya kuwa na utaratibu ndani ya chama kama maamuzi yangekuwa yanafanyika mitaani. Sumaye anatapatapa tu, Fisadi mkubwa yule. mara hiyo tu ameshasahau soko la machinjio kule kibaigwa na Mashamba aliyojitwalia huko kibaha? Kupigana na viti ni kawaida tu kwa vyama vyetu hivi kwani siyo siku nyingi haya tumeyashuhudia ndani ya CDM kule Ilemela.
 
Wameshindwa kusikiliza nukuu nyingi za Nyerere ambaye wanajifanya kumuenzi itakuwa Sumaye? Kifo cha hiki chama ni dhahiri na kikinusurika kitabaki mahututi.
 
Aanze kujihukumu yeye na serikali yao alipokua madarakani kwa kuacha nyufa na kudharau kuiziba sasa ukuta ndo ushamwangukia ananyooshea watu kidole
 
Dalili za malaria huwa zinaanza polepole....hatma yake huwa ni kifo mgonjwa akikosa matibabu.
 
Hata Sodoma na Gomora ilikua vivyo hivyo ujue.....Na NUHU pia aliwahubiria au kama hao wote hukuwaona basi hebu cheki Movie za kinaejeria. Siku zote Theme inabebwa na Mwendawazimu
 
Sidhani kama kulikuwa na haja ya kuwa na utaratibu ndani ya chama kama maamuzi yangekuwa yanafanyika mitaani. Sumaye anatapatapa tu, Fisadi mkubwa yule. mara hiyo tu ameshasahau soko la machinjio kule kibaigwa na Mashamba aliyojitwalia huko kibaha? Kupigana na viti ni kawaida tu kwa vyama vyetu hivi kwani siyo siku nyingi haya tumeyashuhudia ndani ya CDM kule Ilemela.
Kwa hiyo unakubali kuwa rushwa katika chaguzi za CCM ni msingi sahihi wa kupata viongozi!
 
HATA KIKIFA SAIZ KWAN VIP WE UNAONAJE??CHADEMA NDIO MBADALA WA TANZANIA TUITAKAYO???
MGANGA WA KIENYEJI NA MCHAWI LAO MOJA TUH
:msela::juggle:
 
Naona sasa mzee wa hanang anaanza kumzidi mzee mamvi umaarufu humu JF, au kawanunua watu wa kumpandisha chat?
 
sumaye hana jipya,kama ye mjanja atoke ccm ili tumwelewe vizuri! Sio kulalama tu.....!
angetoka ccm tusingejua haya aliyotueleza, muda muafaka ukifika atatoka tu, kila jambo na wakati wake.

Kuhusu ufisadi wa sumaye, mi siukubali, sumaye alichafuliwa na kikwete kwenye zile mbio za urais za 2005, kuwa na shamba kibaha hata wewe uanweza kuwa nalo heka moja ni kama laki 2 wakati huo. Jiulize kuhusu lowasa na akina rostam, richmond nk, kibaya zaidi wewe na mimi sasa ni bidhaa za lowasa, ananunua wapiga kura wake ccm toka mabilioni ya richmond sasa symbion, na sasa njia ni nyeupe kukufikia wewe na mimi kutununua. Mimi sita kubali kuwa bidhaa ya lowasa 2015, je wewe?
 
kama fisadi anaweza kuona ufisadi wa kutisha zaidi ya kuushangaa basi ni wazi hali si shwari.Hii ni ishara kwamba alichoona Sumaye hakuwahi hata fikiri ndio maana anashangaa.Hii ndio kazi waliyoiasisi kupitia Takrima.
 
Maoni yaliyotolewa na Mh F Sumaye, pamoja na kushindwa kupata U-NEC, ni wake up call kwa CCM.
Sina uhakika kama Mh Sumaye angetoa maoni hayo kama angeshinda kinyang'anyiro hicho cha kugombea U-NEC.

Hata hivyo kwa wanacha waaminifu wa CCM aliyosema Mh Sumaye ni common knowledge, ufisadi utaiangamiza CCM kama chama cha siasa makini.

Nimeona maoni kama haya haya ya mtoa mada ambaye vile vile inaelekea ni mwana CCM:

Nimesoma gazeti la NIPASHE leotarehe 9 Oct. 2012, Katibu Mkuu Mukama akijibu tuhuma za Sumaye kuwa azipeleke kwenye vikao husika.Tunasahau kuwa waamuzi wa mustakabali wa chama ni wanachama wanaoona yanayoendelea hukohuko mitaani.
Tumeona jana ngumi na kurushiana viti katika kikao cha uchaguzi huko Musoma, sababu ikiwa hiyohiyo rushwa.

Mukama akisubiri kuletewa hoja ofisini, basi uhalali wa chama kwa wanachama wake utaendelea kushuka.

Wahenga walisema mwenye masikio na asikie!

Huyo Mkama hafahamu methali ya kiSwahili, "Asiyesikia la mkuu mbele huvunjika guu." Subiri 2015 CCM ikiwa kilema.
 
Naona sasa mzee wa hanang anaanza kumzidi mzee mamvi umaarufu humu JF, au kawanunua watu wa kumpandisha chat?
Mkuu usiifurahishe nafsi yako kwa kufikiri mtu unaweza kumshabikia mtu badala ya principle.
Rushwa ni adui wa haki, huo ndio msingi wa argument yangu, na hili likisemwa hata na wewe litabaki kuwa kweli.
 
Kufa kufaana, wao wanakufa sisi tunachukua nchi
Msishabikie sana kifo cha CCM maana hakitakuja bila a price tag ya machafuko ndani na nje ya CCM.
Tumeona uhasama uliopo kati ya wanachama wenyewe,na hata Mwenyekiti aliwahi kutamka kuwa huwezi kuacha glasi yako ya maji ukiondoka mezani walipo wana CCM wenzio.
Watu hawaaminiani.

Vitendo hivi vya kutoaminiana vinatokana na uhasama wa kutotenda haki, rushwa ikichukua nafasi kubwa kuinunua hiyo haki.
 
Ukweli husemwa:

kama fisadi anaweza kuona ufisadi wa kutisha zaidi ya kuushangaa basi ni wazi hali si shwari.Hii ni ishara kwamba alichoona Sumaye hakuwahi hata fikiri ndio maana anashangaa.Hii ndio kazi waliyoiasisi kupitia Takrima.

Mkuu, hapo umenena. CCM walipoingiza neno takrima ndani ya katiba ya chama, huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kuasisi rushwa. Watu kama Sumaye walifikiri haitawafika. Too late, maji yameishamwagika. CCM kila siku inapoteza imani kwa wananchi wa kawaida, imenishangaza kusikia imeanza kupoteza imani kwa mafisadi pia.

Nakugongea LIKE kwa nje
.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom