Demokrasia ndani ya CCM imekwenda wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Demokrasia ndani ya CCM imekwenda wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, Oct 8, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Chama kikongwe cha siasa nchi Tanzania CCM kinazidi kupoteza demokrasia ndani ya chama chake,ama kwa makusudi au kujisahau.Namaanisha kutokana na staili yake inayofanyika katika chaguzi zake za ndani ya chama.Tumeona rushwa,udini na ukabila umeendelea kushika kasi na kukitesa chama hiki kikongwe nchini.

  Yaliyotokea huko Shinyanga ni mfano mzuri wa CCM kujimaliza ama kujikaanga kwa mafuta yake yenyewe.Kampeni za ujumbe wa NEC kupitia wilaya kwa wilaya ya Shinyanga mjini imekitia doa chama hiki kwa kampeni chafu za ukabila na rushwa huku wagombea wakijinadi wataimaliza CHADEMA kwa kutumia nguvu yao ya kifedha na kiutawala kuelekea uchaguzi wa 2015.

  Uchaguzi umezidisha makundi yanayo hasimiana ndani ya chama.Pia chaguzi hizi zimeibua chuki miongoni mwa wanachama hususani wale wanao kikosoa chama, kwa majina yao kufyekwa na sekretarieti ya chama,huku majina mengine yaliyofyekwa huko wilayani yakirudishwa mfano jina la Mary Nagu.

  Hali hii imesababisha sintofahamu ndani ya CCM kutokana na staili yao ya kujilimbikizia madaraka kitendo kinachooneka mtu mmoja kuwa viongozi ndani ya jamii kama vile hakuna watu wenye sifa za kushika nyadhifa ambazo mtu mmoja anatunukiwa.

  Janga lingine ni kuondoa kundi ambalo limekuwa wasemaji wasio ogopa kukisema chama chao kwa kufuata misingi ya kiongozi akubali kukosoa na kukosolewa.Hali hii imesababisha baadhi ya wabunge majina yao kukatwa kwa vile tu walionyesha msimamo wao wakati wa kumpinga Waziri mkuu kwa kusaini kwenye fomu ya kutafuta saini 70 za Zitto Kabwe za kutaka kumng'oa mtoto wa mkulima.

  Pia chama hiki kimekuwa kokoro katika uchaguzi zake kwa kuzoa hata wale waliopoteza sifa ndani ya jamii husika ama kwa vitendo vya rushwa ,ukatili na hata uharamia kitendo kinachosababisha chama hiki kushindwa kujitenga na kauli ya wapinzani kwa kukiita Chama Cha Majambazi.

  Mwisho ,kauli ya Sumaye aliyekuwa wazir mkuu kwa kipindi chote cha serikali ya awamu ya tatu kuutangazia umma kuwa CCM ina nuka rushwa ni pigo kubwa kwa mustakabali wa CCM kuelekea uchaguzi mkuu,kauli ya Sumaye si ngeni masikioni mwa Watanzania kwani hata Mh. Makongoro Nyerere aliwahi kulalamika katika harakati zake za kuusaka ubunge wa EAC.Ni wakati sasa wa kujitazama na kuangalia wapi wanacheza karata zao vibaya na kutafuta karata turufu na kucheza kadi vizuri.
   
 2. sifongo

  sifongo JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2012
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 4,593
  Likes Received: 2,399
  Trophy Points: 280
  Mkuu hawana muda wa kujiangalia wala kujitathmini, muda walionao ni jinsi gani watabaki madarakani waendeleze ulaji, wameshauriwa sana, mumewashauri sana na mutawashauri sana lakini hamtasikilizwa, lamsingi tuelekeze nguvu katika kutaka mabadiliko waje kustuka wapo nje na hapo ndio watajua kumbe kweli walikuwa watenda dhambi............stop kulalama now ni muda wa kutake action........M4C
   
 3. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Yangu macho
   
 4. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145

  Na kweli chama cha kisultani kinajimaliza chenyewe.Ni cha kisultani kwa kuwa madaraka yanakaimisha kwa mujibu wa matakwa ya familia.Ndo maana leo hii huwezi kushangaa Kikwete family imeaidi wamepita bila kupingwashika hatamu ndani ya chama mbaya zaidi wamepita bila kupingwa.Na kweli hii ndiyo ukomavu wa demokrasia ndani ya chama twawala
   
 5. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Demokrasia ndani ya ccm ipo sana tu inaitwa hongo
   
 6. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Chama kinachungulia kaburi! kinapumulia machine! 2015 tunakizika rasmi.
   
 7. T

  Tabby JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2012
  Joined: Jan 8, 2008
  Messages: 9,871
  Likes Received: 5,466
  Trophy Points: 280
  Huwezi kuadvocate democrasia wakti hata wewe unakalia kiti kwa kuchakachua. Democrasia inakuwa ya kweli pale tu penye nia safi inayolenga kulinda maslahi ya wengi. Katiak CCM hakuna hicho kitu zaid ya kubuni mbinu za kuendelea kutawala hata kama ni kinyume cha matakwa ya wengi. Anzia mwenyekiti hasikiki anaongelea maendeleo halisi ya watanzania wala kero zao muhimu. Kwa mtazamo finyu wa kibinafsi na uchu wa madaraka, kinachoongelewa sasa hivi ni CCM kubaki madarakani 2015 hat akama wananchi hawana dira ya maendeleo.


  Utasikia "Wapinzani wana uchu wa madaraka". Kama ndivyo kwa nini ccm na serikali inachakachua hadi kupoteza uahi wa wanaoonekana kui querry?

  Rushwa imetawala chaguzi zote ccm lakini husikii hatua yoyote kuchukuliwa.
  TAKUKURU MPO? AU KWA VILE RUSHWA ZIKO CCM HIZO HAMHUSIKI NAZO? Ni ajabu kweli.

  Chama kinacho palilia rushwa hadharani mchana kweupe ni chama kisichofaa kuwepo katika jamii ya wapenda haki. 'TENDWA, HADIDU ZAKO ZA REJEA HAZIHUSIANI NA HAYO YANAYOFANYWA NA WANA CCM? KWAN INI USIKIFUTE HICH CHAMA? AU KWAKO BADO KINAUADILIFU UNAOKIDHI VIWANGO VINAVYOTKAIWA?


  Maandalizi machafu ya kubaki madarakani 2015, kwa gharama yoyote hata kama ni damu ya wa TZ. MWAMUNYANGE, UNAWEZA KUSHAURI NINI JUU YA HILI LABDA?

  CCM sahihi ilijuwa ya Mwalimu Nyerere iliyosema - Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa; Cheo ni dhamana, nitatumia cheo changu ... n.k

  USANII WA LEO SIYO KABISA. NDIYO MAANA WAUNGWANA WANASEMA CCM SI MAMA. KIMESHAINGILIWA
   
 8. A

  Arsenal fc New Member

  #8
  Oct 8, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vita ya panzi furaha kwa kunguru,ni wakati sasa M4C kujipanga kuizika kabisa CCM.
   
 9. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #9
  Oct 8, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ni kweli bila hela huwezi kuwa kiongozi shame on them
   
 10. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #10
  Oct 8, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  dalili za mvua ni mawingu,dalili za kifo ni mauti yako ndo maana hata sikio la kufa haliskii dawa
   
 11. S

  Savannah JF-Expert Member

  #11
  Oct 8, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 238
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Imeperusha na ufisadi na hongo. Watu wananunuliwa kama nyanya sokoni.
   
 12. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #12
  Oct 9, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Anacho jaribu kukizungumzia mh Sumaye NI Ukomavu wa rushwa na ukiukwaji wa maadili japokuwa chama hiki kilianza kukumbatia matajiri katika kipindi cha uongozi wa awamu aliyokuwa akiiongoza kama waziri mkuu.

  Mawe na mapigano ya kugombea madaraka ndani ya CCM ni ishara tosha kuwa bila kuwa mjumbe wa NEC mwanachama wa CCM huwezi piga hatua za kimaendeleo.Hatua hizo ndizo zilipelekea kipindi cha mh. Sumaye yeye mwenyewe kutamka hadharani kuwa ukitaka mambno yakoyafanikiwe ingia CCM mbaya zaidi aliwataka wafanyabiashara.

  Kwa maneno haya ndiyo ile dira iliyokuwa inaonyesha CCM chama cha wakulima na wafanyakazi ilipopotea na kukosa mashiko ndani ya CCM.Anguko la wanyonge kukosa nafasi za kiuongozi ndani ya CCM na kukaimisha madaraka kwa wenye nacho,ndiyo hali iliyosababisha ufisadi kutamalaki
   
 13. S

  Skillionare JF-Expert Member

  #13
  Oct 9, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Namshukuru Mungu ccm inakufa
   
 14. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #14
  Oct 9, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kufa pekee haitoshelezi bali msiba wake uwe ni mawaidha kwa vyama vingine ambavyo vina mrengo unao shabihiana na CCM.Pia iwe fundisho kwa watawala madhalimu wasio na haya katika mkakati w kuhakikisha Tanzania imeuzwa na kuwa nchi ya wageni kwa kutoa ardhi ytu kwa thamani ya shilingi 200/- kwa acre moja ya ardhi na kuwaacha wazalendo wakiendelea kuwa wakimbizi ndani ya nchi yao kwa kuwanyang'anya ardhi kwa kigezo cha uwekezaji.
   
 15. babykailama

  babykailama JF-Expert Member

  #15
  Oct 9, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Pasipo kuchukuwa hatua sasa wakati wa uchaguzi wa ndani ya chama hakutakuwa na namna ya kurekebisha wakati wa uchaguzi mkuu ujao 2015.

  Rushwa si ya kuichekea hata kidogo!!
   
 16. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #16
  Oct 10, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  pamoja na kifo chake kinacho kuja kwa kasi,si vibaya kama CDM au chama chochote cha upinzani chenye nguvu kitaingia kwenye ushindani wa uchaguzi wa 2015 kwa kushindana na CCM dhaifu.Tunataka umakini wa CDM na uwezo wa kusimamia sera zake katika ushindani kwa kupambana na chama chenye nguvu.

  Wote mashahidi tunaona jinsi Republican na Democrat wanavyo pambana,kiasi ni vigumu kutabiri nani atachukua nchi.
   
 17. M

  Mr jokes and serious Member

  #17
  Oct 10, 2012
  Joined: Oct 4, 2012
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani sababu kwanza ya kuitoa ccm madalakani ni kupa red kadi ili waone wenzao wanaotaka uchezaji bora uwanjani wanatakavyo cheza kwa juhudi na nguvu zote kuhakikisha ushindi unapatikana kwa nguvu zote tuache kupiga kelele na tueleweshane kwa wale wasio elewa kwa kuwapafaida na hasara kwa chama kikitawala mda mrefu madalakani ili mwisho wa cku tukiweke madalakani chama kitakacho leta maendeleo kwenye nchi kongwe naendeleo haya lingani na raclimali na umri ulikuwa nao aibu ata viongozi hawana haya kabisa.
   
 18. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #18
  Oct 10, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mwalimu Nyerere aliwahi kutamka hadharani bila kufinya maneno kuwa serikali ya CCM inanuka wakati ana zungumzia Tanzania na hatima ya uongozi.Ni kweli mwalimu aliona mbali sana na alikuwa na kipaji cha kuitwa mwalimu kutokana na maono yake.

  Ukisikiliza hotuba za mwalimu Nyerere utagundua kuna kitu zaidi ya uzalendo ndani ya moyo wake.Miongoni mwa matamko yake,aliwahi kusema"ukiweza kumwambia mkeo kwa ukali kuwa,Ikulu ni mahali pa takatifu,basi hata marafiki zako watakuogopa na kukuheshimu"mwisho wa kunukuu.

  Maneno haya ya mwalimu leo hii yamegeuka shubiri ndani ya CCM,kutokana tu na kuacha yale mwalimu aliyaona yana athari kubwa kwa mustakabali wa chama na nchi.Leo hii mwalimu akijaliwa akafufuka na kukuta uozo aliokuwa akionya na sasa ndiyo umeshika kasi nadhani angekufa mara ya pili kwa uchungu.

  CCM ya leo si CCM ya mwalimu.Maadili,madhumuni,miiko na misingi ya chama imetupwa mbali na kuachia usisi,umimi na undugunazion umetawala.Leo hii maskini gani anayeweza kusimama kugombea nafasi ya uongozi ndani ya chama akapita.Hata wale wanaopita bila kupingwa katika chaguzi za ndani ya chama ni matajiri wakubwa.Toka lini ukasikia mkulima wa Chakware,Tanganyika masagati,ipililo na masanwa wamepitishwa bila kupingwa.Hali hii ndo iliyopelekea CCM kukimbiwa na umati mkubwa kujiunga na upinzani wakitafuta pambazuko jipya.

  Ukiangalia majina ya wajumbe waliochaguliwa utagundua kuwa chama hiki si cha wakulima na wafanyakazi kama walivyoaminishwa wananchi zama hizo.Leo kuna watu kama Dickson Membe,Fred Lowasa.Ashura Hussein Mwinyi,Ridhiwani Kikwete,Beny Samwel,Debora Mwandosiya,Irene Pinda,Felister Ndugai,Christopher Ndejembi,,Sharifa Bilal,Hawa Kigoda,Judith Mukama na Jarome Msekwa.Majina haya na mengineyo mengi unafikiri yana ashiri nini katika mustakabali wa amani na udugu aliotuachia mwalimu.

  Majina kama haya ndiyo yalisababisha wananchi wa Libya kutokuwa na imani na Gadaffi hata kama aliwajali kwa kila kitu.Wananchi waliamini Hayati Gaddaffi alijali sana watu wa familia yake na kuwapa upendeleo kuliko wananchi wengine wowote.

  Cha msingi katika mada hii ni jinsi ya kukifanya chama hiki kuwa na malengo ya kifamilia zaidi kuliko matakwa na madhumuni ya waasisi wake.Kwa staili hii kutokana na matokeoya chaguzi za ndani ya chama nina uhakika uchaguzi huu utaibua makundi zaidi ya yaliyokuwemo kwasababu chama sasa kinaendeshwa kama vanguard party(wateule wachache).

  Hata falsafa ya kujivua gamba nayo imewekwa pembeni na watu kujikita zaidi na uchaguzi wa 2015 kuliko kuangalia matatizo ya wapiga kura kama walivyo ahidi kwenye manifesto yao.Watuhumiwa wa ufisadi nao wamerudi kwa kishindo kiasi cha kuwadondosha wapinga ufisadi,hali ni tete kila mmoja ana jaribu kuweka vision ndani ya chama kwa kigezo cha kuisaidia CCM kushinda 2015,kwa nguvu zaidi ya pesa,ubabe zaidi ikibidi na uwizi zaidi.

  Wako wapi wadhamini wa chama kina Peter Kisumo na wenzake,wamegubikwa na nini kiasi cha kushindwa kukemea yanayotokea.Chama kimekosa dira na mwelekeo,yaliyosemwa na marehemu Horace Kolimba leo yamejitokeza hadharani.Imekuwa ni kawaida sasa kumsakama anaye kosoa kuliko kuyafanyia kazi yale aliyoyalalamikia.Kwa mtazamo wangu mzimu wa Horace Kolimba utaendelea kukitafuna chama badala ya kuangalia nini walichokosea kiasi cha mtendaji mkuu wa chama kwa wakati kufikia kutoa tamko hilo.

  Mwisho,wanachama madhubuti walio ndani ya chama hawatatishwa na kuzibwa midomo yao kukemea maovu kwa kunyima au kukatwa majina yao makusudi.Cha msingi mkiona hali inazidi kuwa tete na chama mnakipenda fanyeni harakati za makusudi kufanya mapinduzi ya kukiimarisha chama kwa kukemea kila uozo ndani ya vikao na hata nje ya vikao.Dhamira ya kweli tu ndiyo silaha madhubuti kuelekea njia bora ya kukinusuru chama.Angalieni yaliyoisibu KANU na maprofesa wa siasa kwa vyama vikongwe visivyotaka kutazama wakati na matarajio ya wakati husika.
   
 19. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #19
  Oct 10, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  CCM imeshaoza sasa sio kunuka!
   
 20. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #20
  Oct 10, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ngoma ikipigwa sana mwishowe hupasuka,yetu macho mwisho wa siku tutasema tuliwaambia lakini hamkutusikia.
   
Loading...