TAG Waonesha njia: Je EAGT wataifuata?

TAG Waonesha njia: Je EAGT wataifuata?

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
14,191
Reaction score
19,115
TAG wameonesha ukomavu wa kiroho kwa kuamua kuachilia na kusamehe mali zake ambazo mahakama ilikuwa imetoa uamuzi zirejeshwe TAG.

Ifahamike kuwa EAGT pia ina mgogoro na makanisa mengi tu yaliyojimega toka EAGT yakienda na majengo na mali za EAGT. EAGT wamekuwa wakidai mali hizo na baadhi yake walifanikiwa kuzirejesha kupitia suluhishi mbalimbali kama za wakuu wa wilaya na mikoa, japo mahakamani walikwama.

Ni vizuri sasa na EAGT kwa hiari yao watangaze rasmi kuachilia na kusamehe mali hizo kama walivyofanyiwa wao! Bila shaka Askofu Mwaisabila anasubiri kwa hamu EAGT nao waachilie! Swali ni je watafanya hivyo?
 
Makanisa mengi kwa sasa yanaendeshwa kama kampuni, kuachia mali kunaweza kuonekana kama bad for business.
Lakini mwenye business yake ni Mungu na makanisa ni nyenzo zake, kwa hiyo siyo vibaya kuachilia maana wote ni watoto wa Baba mmoja kama alivyosema askofu wa EAGT Mwakipesile, kwa hiyo macho yote na masikioyako kwake! Je ataifuta hiyo njia aliyooneshwa na TAG? ikizingstiwa yeye pia anadai mali zilizochukuliwa na waliojimega likiwemo kanisa la Askofu Mwaisabila lililomega sehemu kubwa sana ya EAGT. Askofu Mwaisabila alImega zaidi ya wachungaji elf moja toka EAGT!!
 
EAGT aiseeh! Ilijimega kutoka TAG, Mwaisabila akajimega kutoka EAGT na kuanzisha AGGCI, nako AGGCI ikajimega na kuwa mbili. Haya mambo ya madaraka ni mbaya sana.
Kuna kitu kinaitwa karma kile unachomfanyia mtu basi lazima kikurudie tu.

Wanasiasa nao wanajisahau sanaa.
Ila yote wanayofanya ipo siku na wakati kitawarudia tu.
 
Hadi muda huu hakuna dalili kuwa EAGT wataifuata njia waliyooneshwa na TAG ili waachilie mali zote na majengo yaliyochululiwa na wsliojimega toka EAGT!!
 
Back
Top Bottom