Tafsiri ya neno "Nimekubali kuolewa"

mrdocumentor

Member
Nov 27, 2021
43
53
Nimerudi tena kuzungumzia Suala la ndoa hususan pale mtu anapokiri kuwa "nmekubali kuolewa" anamaanisha nini?

Inawezekana kuna kundi kubwa la wanawake sasa hivi wanatoa machozi majumbani na kujilaumu wenyewe kutokana tu na kutoelewa tafsiri ya hayo maneno machache, Leo tutaenda kuangalia hapa baadhi ya tafsiri ya maneno hayo.

Kwanza kabisa tufahamu ndoa nini? Katika swali hili nimejaribu kukidhi mahitaji ya watu wa makundi matatu, Kundi la kwa kwanza nmeangalia maana ya ndoa kisheria yaani sheria ya Tanzania ambayo inasema
"Ndoa ni muunganiko wa hiari kati ya mwanaume na mwanamke unaokusudiwa kudumu kwa muda wa maisha yao yote."
Kundi la pili ni uislamu unasema nini kuhusu ndoa "Ndoa ni Mkataba wa hiari unaofungwa kati ya mwanamke na mwanaume ili kuwa mume na mke kwa mujibu wa sheria za kiislamu "
Biblia nayo inasema nini kuhusu Ndoa? "Tangu mwanzo, Mungu alikusudia ndoa iwe muungano kati ya mume mmoja na mke mmoja. (Mwanzo 2:24)"

Kama ulikuwa makini kufuatilia maana hizo za ndoa utagundua kuwa wote wanakubaliana kuwa ndoa ni "Muungano" lakini kingine wote wanakubaliana kuwa muungano huo ni wa jinsia mbili tofauti.
Tofauti ambayo Biblia imejitofaitisha na zingine ni kuwa imebainisha kuwa huyo mwanaume na mwanamke anapaswa kuwa mmoja Jambo ambalo linakinzana na uislamu ambao kupitia Surat Nisa' inabainisha kama ifuatavyo “…. BASI OENI MNAOWAPENDA KATIKA WANAWAKE (maadam mtafanya uadilifu) WAWILI AU WATATU AU WANNE (tu). NA MKIOGOPA KUWA HAMWEZI KUFANYA UADILIFU, BASI (oeni) MMOJA TU,.....[4:3].

Tuache hilo turudi kwenye mada, tunatambua kuwa katika mkataba wowote lazima kuwepo na makubaliano kati ya pande mbili, na leo katika ndoa ntazungumzia upande wa mwanamke ili tuone pale anapoulizwa umekubali kuolewa akajibu "nimekubali kuolewa na fulani" anafahamu amekubali nini kuafanyiwa na fulani huyo?
Yafuatayo ni baadhi ya mambo anayoyakubali wakati mwingine kwa kujua au kutokujua na wanaokubali bila kujua ndio wanakuja kusumbua kwenye ndoa;-

Nmekubali kufungiwa.
Ndio unapokubali kuolewa unapaswa kujua kwamba umekubali kufungiwa, Hii haina maana kufungiwa ndani mda wote, hapa unapaswa kufahamu kuwa haupaswi kufanya jambo lolote bila ruhusa ya mumeo, Haupaswi kwenda popote bila ruhusa ya mumeo, Haupaswi kumkaribisha yeyote nyumbani kwako bila ruhusa ya mumeo na mengine mengi.
Npo hapa nmekaa njooni mnipige.

Nimekubali kupangiwa
Yes, Quran na Biblia zote zinakubaliana kuwa mwanaume ndio kiongozi wa familia unabisha? Ngoja tuone Qur'an inasemaje?
"Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake kwa kuwa Allah Amefadhilisha baadhi yao kuliko wengine na pia kwa ambayo wanatoa katika mali zao." [An-Nisaa: 34]
Tufanye bado hujaelewa tuangalie na Biblia inasemaje?
Biblia inasema kwamba “mume ni kichwa cha mke wake.” (Waefeso 5:23). Hii haina maana kuwa mwanamke hana haki kwenye familia, Hapana! maana yake ni kwamba katika safari yeyote ili ifanikiwe lazima iwe na kiongozi kanuni hiyo hata wadudu ambao tunahisi hawana akili wanaifahamu. Kwa kutambua hilo Mungu akamchagua Mwanaume awe kiongozi katika safari hii ya dunia ukizingatia mwanamke alitoka kwenye ubavu wa mwanaume.

Nimekubali kutendewa.

Hapa ndipo unakuta Mwanamke ana kazi nzuri inayomlipa lakini majukumu mengi kama sio yote ya nyumbani Mume ndio atawajibika na kipato cha mama ataweka kwenye kikoba, hapa mwanaume atalipa umeme, ada, bili ya maji n.k, Lakini katika kutendewa uku usisahau kwamba mwanaume pia ana haki ya tendo la ndoa kwako ikiwa kama ni wajibu wake wa msingi pia kuhakikisha anatimiza mahitaji yako ya kihisia ifahamike vizuri hapa wanawake wengi wanajua tendo la ndoa linamfaidisha mwanaume, ukweli ni kwamba 99% ya faida ya tendo hilo inaenda kwa mwanamke ndo mana tunasema mwanaume anakidhi mahitaji yako ya kihisia kama ambavyo anakidhi mahitaji yako mengine na hili ndio limebeba maana halisi ya ndoa bila hilo itakuwa sawa na dada na kaka wameamua kukaa pamoja.

Ndugu zangu zipo tafsiri nyingi sana za neno nmekubali kuolewa ila nimewapa mwanga tu juu ya hayo mambo matatu unayoyakubali lakini pia unakuwa umekubali kufuatiliwa, kuhurumiwa na wakati mwingine kuchungwa na kushughulikiwa pia 😜.

#Lindiicon🇹🇿
 
Back
Top Bottom