Tafasiri ya kuacha kupokea simu

kotelyimola

JF-Expert Member
Oct 9, 2015
1,457
1,504
Naomba kufahamu tafasiri ya kuacha simu ikiita hadi ikatike yenyewe.

Kuna jamaa yangu alikuwa na mpenzi wake katika kikao. Simu ya mpenzi wake ikaita, jamaa waliokuwa nao wakamtonya mpenzi wa jamaa yangu kuwa simu inaita. Mpenzi wa jamaa akajibu sitaki kuipokea acha itakatika yenyewe. Baada ya kurudi geto jamaa yangu anakuta ni namba ya simu ya dume. Je kama ungalikuwa wewe ungatafasiri vipi?
 
Mtu anakudai na muda huyo huna cha kumjibu.....
Upo katika mazingira ambayo huwezi ongea....
Mchepu unapiga....
Rusha roho tu kumuwekea baby roho juu, roho ifurukute kijasho kitiririke awaze why hupokei simu....
Hasira, anaekupigia kakuuzi....
Namba ngeni n.k

Hizo zote zaweza kuwa tafsiri
 
Huyo demu atakuwa na uhusiano hasi na huyo aliyepiga simu. Nadhani alikataa kuikata asije ulizwa kwa nini umekata simu yangu.
 
Mtu anakudai na muda huyo huna cha kumjibu.....
Upo katika mazingira ambayo huwezi ongea....
Mchepu unapiga....
Rusha roho tu kumuwekea baby roho juu, roho ifurukute kijasho kitiririke awaze why hupokei simu....
Hasira, anaekupigia kakuuzi....
Namba ngeni n.k

Hizo zote zaweza kuwa tafsiri
Jamaa alikuta ni namba ya mwanaume anayemfahamu, demu kajitetea kuwa ilikuwa simu ya kikazi. Jamaa anauliza kwa nini hakukata ilipopigwa hana la kujitetea. Je, jamaa yangu akifikiri ni mchepuko atakuwa amekosea?
 
sema ni wewe mkuu, ila haya maisha tu unachofanya unalipwa hapahapa duniani, aidha unajua au hujui!
 
Ni kweli maji yakimwagika hayazoleki. Mtu ukimfumania mweza wako ni donda lisilopona kama donda ndugu. Sie yalishatukuta
Duu ULIFUMANIWA MKUU? minaona kwa mwanamme ina afadhali mwanamke ni baraaaaaaaaaaaa,na ukisamehewa ujue utaitwa majina ya kila aina bora ubebe virago vyako tuu..
 
mm pole namuomba mungu kila siku asinionyeshe hayo kwa mume wangu naweza Kufa au nikapata maradhi ya moyo..
Likitoka utashangaa unapata ujasiri na unaona ni kawaida bali kidonda kila siku kinakuwa kibichi hakikauki hadi siku unaingia kaburini. Si ya kuomba yakupate, kila siku omba kwa mungu usione
 
20160419055125.jpg
 
Likitoka utashangaa unapata ujasiri na unaona ni kawaida bali kidonda kila siku kinakuwa kibichi hakikauki hadi siku unaingia kaburini. Si ya kuomba yakupate, kila siku omba kwa mungu usione
Inshallah nikisikia hivyo naogopa! nilimfumania simtaki tena ivoo............
 
Inshallah nikisikia hivyo naogopa! nilimfumania simtaki tena ivoo............
Hata wengine tulijiapiza hivyo acha mama hiyo haiwork. Kama mna watoto unaangalia future ya watoto na unacool down. Ila kuhakiki ni mtindo mmoja
 
Maana yake usipige tena hadi upigiwe

Ila kama umempigia mupenzi akagoma kupokea litakufurukuta rohoni kana kwamba mtu kafikicha pilipili kwenye kidonda
 
sijaelewa hapo bado kidogo
Ni hivi kwa kawaida kama upo katika kikao mtu akipiga simu unaikata pengine kwa kumtumia sms kuwa upo busy. Ila kama ni mtu wa karibu kama mwenzi ambaye hutaki ajue upo wapi unaacha iite mpaka ikatike. akikuuliza mbona hukupokea unajidai kuwa ulikuwa ofisi ya pili ndo maana hukusikia simu ile na umekuta missed call. Sasa kama upo na mpenzi wako na simu ikaita naye akasema siipokei hii, je inatoa tafasiri ipi? Kama hakuna namna kwa nini asiikate?
 
Ahaaa hapo mkoje inategemea kama mna element za kutoaminiana na michepuko juu ni ishu
 
Back
Top Bottom