Tafakuri ya FaizaFoxy 3: Njozi. Saikolojia ya Siasa

Tafakuri ya FaizaFoxy 3: Njozi. Saikolojia ya Siasa

Nimekujibu kwa mafumbo hivyo hivyo kuwa huyo mfalme (na wenzake) anatakiwa kulazwa na kupewa na matibabu kwa sababu ana magonjwa ya akili
Mfalme Njozi hatunae tena bali tuna wanasiasa. Unakubaliana au unapingana na swali lililopo kwenye post namba moja?
 
Wanasiasa wanaongoza kwa kutegemea njozi hawanamafanikio ya kimaendeleo, mwisho wao wanaishia kuota njozi za kutoa kafara kwa wafalme wao wanaowaotesha njonzi, hapa ndipo zinapotokea ajali za meli kuzama, ajali za barabarani,raia kutekwa, kuuawa kwa kupigwa risasi.
 
Vipi maamuzi ya Lowassa, hayakuwa ya njozi zake?
 
Dosari ya "Tafakuri" inaanzia na kuishia hapo kwa ndoto za upishi wa maandazi ya nazi na kusahaulisha watu kwamba yapo mambo ya msingi zaidi ya hayo maandazi ya nazi yanayoweza kuwafanya baadhi ya watu wawe na chuki bila ya kujali wali wa nazi au maandazi ya vitunguu saumu.

Njozi yangu ndio hiyo.

Eeenh, na kuhusu hiyo saikolojia..., nawatakia njozi njema kwa hilo!
 
Njozi ni istilahi inayotumika hasa katika maisha ya kiroho kama njia ya mtu kupata taarifa ya mambo yaliyopita, yaliyopo, na yale yajayo.
Ndoto ni mfululizo wa picha, mawazo, mihemko na hisia ambao unatokea akilini, kwa kawaida bila makusudi, katika hatua fulanifulani za usingizi KUTOKA WIKIPEDIA
 
Hapo zamani za kale palitokea mfalme mmoja aliyependwa na wengine na kuchukiwa na wengine kati ya raia zake. Mfalme huyo akiitwa Njozi. Sifahamu kama neno "njozi" linatokana na jina la mfalme huyo au lilikuwepo kabla.

Kupendwa na kuchukiwa kwa mfalme Njozi na raia zake hakukuwa rasmi, hakukuwa kuna kundi lililompemda au kuna kundi lililomchukia daima. Maamuzi ya mfalme Njozi ndiyo yaliyopelekea au kupendwa na baadhi au kuchukiwa na baadhi kwa wakati huo.

Baadhi ya maamuzi ya mfalme Njozi kuna siku yaliwapendeza waliomchukia na kuanza kumpenda ghafla na kuna siku yaliwachukiza waliompenda na kuanza kumchukia ghafla. Maamuzi ya Mfalme njozi yalitokana, kwa asilimia kubwa, na njozi zake. Na kwa asilimia chache sana yalitokana na kufata ushauri wa wasaidizi wake.

Kuna siku Mfalme Njozi akipata Njozi yamepikwa mandazi ya nazi basi siku hiyo ataamrisha nyumba za raia zake wote zipike maandazi ya nazi. Wapenda mandazi ya nazi siku hiyo ikawa ni furaha na neema kubwa kwao na wasiopenda mandazi ya nazi ikawa ni chuki na karaha kubwa kwao, nchi yote ilinukia mandazi ya nazi kwa wayapendao na ilinuka maandazi ya nazi kwa wasioyapenda.

Huo ni mfano mmoja tu wa kuwaelewesha ni vipi Mfalme Njozi alitumia njozi zake kufanya maamuzi.

Bingwa wa saikolijia za siasa Jaap Van Ginneken amewahi kuandika (tafsiri isiyo rasmi) "Ikiwa saikolojia ni sayansi ya uzoefu (experience), tabia, mwingiliano wa mtu na makundi basi saikolijia ya siasa ni sayansi ya uzoefu wa kisiasa, tàbia ya kisiasa, mwingiliano wa kisiasa wa mtu na makundi.

Kwa kisa hicho cha Mfalme Njozi na saikolijia ya kisiasa kama alivyoielezea bingwa wa saikolijia (kwa kuifupisha), tukitazama mwenendo na maamuzi ya wanasiasa wa hapa Tanzania, tokea kabla ya Uhuru mpaka tupate Uhuru mpaka leo hii, jee, wana tofauti na Mfalme Njozi?

Nawatakia njozi njema wote mtakaoshiriki madà hii.

tatizo ni nyumbu wa cdm na ccm
 
Vipi maamuzi ya Lowassa, hayakuwa ya njozi zake?
Ndiomaana hakufanikiwa kwa kuwa zilikuwa ni njozi zake, na tusitegemee kupata mafanikio kwa kuongozwa na wafalme wanaoongoza kwa kutegemea njozi za kuota usingizini, ipo siku watakuja kuota kutukata vichwa.
 
Kwa wenye kufikiri, hii tafakuri inawagusa zaidi raia kuliko wanasiasa au Wafalme.
 
Mfalme Njozi... kweli watu walijua kuandika hapo zamani...
Wakatumia fasihi, nahau, misamiati na tafsida katika simulizi zao tamu...
Mfalme Njozi yeye aliongozwa na utashi wa njozi zake akiamini ndio mfumo sahihi na anawafurahisha raia wake pasi kujua kwamba mandazi yale ya nazi kuna wengi yakiwadhuru na kuwafanyia mzio aidha shida za wengine haikuwa mandazi bali mavazi!!!
Yawezekana Mfalme Njozi alikuwa tofauti sana na Mfalme Juha lakini kwa kuwa wote walikuwa wafalme ni lazima WALISHABIHIANA SANA maana katika ufalme wanaofaidika sana ni VIKARAGOSI wanaomzunguka MFALME huku wakimsifia na na kumhadaa kwamba kila kitu kiko sawa ili waweze KUJAZA MATUMBO YAO!!!
Njozi uzuri wake mtu anaweza miliki utajiri wa dunia nzima kukicha akaenda kukopa mandazi ya shilingi miambili!!!
NI NJOZINI TU MTU AWEZA KUWA SIVYO ALIVYO!!!
 
Yule mfalme aliyetembezwa uchi ndio mfano wa mfalme tuliyenaye.
Magufuli nia yake namba moja ni kumfuta Nyerere kwenye historia ya taifa hili.
Miradi hii inatoibuka kwa kasi ya uyogo, INA gharama kubwa sana kwetu sisi na kizazi kijacho.
Magufuli hana ndoto za kuboresha maisha ya watu wake.
Yeye anataka kuboresha miundombinu huku watu wake wakifa kwa njaa.
Watu gani wamekufa kwa njaa Tz, nyumbu mtapata tabu sana.
 
Mfalme Njozi... kweli watu walijua kuandika hapo zamani...
Wakatumia fasihi, nahau, misamiati na tafsida katika simulizi zao tamu...
Mfalme Njozi yeye aliongozwa na utashi wa njozi zake akiamini ndio mfumo sahihi na anawafurahisha raia wake pasi kujua kwamba mandazi yale ya nazi kuna wengi yakiwadhuru na kuwafanyia mzio aidha shida za wengine haikuwa mandazi bali mavazi!!!
Yawezekana Mfalme Njozi alikuwa tofauti sana na Mfalme Juha lakini kwa kuwa wote walikuwa wafalme ni lazima WALISHABIHIANA SANA maana katika ufalme wanaofaidika sana ni VIKARAGOSI wanaomzunguka MFALME huku wakimsifia na na kumhadaa kwamba kila kitu kiko sawa ili waweze KUJAZA MATUMBO YAO!!!
Njozi uzuri wake mtu anaweza miliki utajiri wa dunia nzima kukicha akaenda kukopa mandazi ya shilingi miambili!!!
NI NJOZINI TU MTU AWEZA KUWA SIVYO ALIVYO!!!
Hakika nimefurahishwa sana na uchambuzi wako wa njozi za Njozi.
 
Back
Top Bottom