FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,506
- 123,819
Hapo zamani za kale palitokea mfalme mmoja aliyependwa na wengine na kuchukiwa na wengine kati ya raia zake. Mfalme huyo akiitwa Njozi. Sifahamu kama neno "njozi" linatokana na jina la mfalme huyo au lilikuwepo kabla.
Kupendwa na kuchukiwa kwa mfalme Njozi na raia zake hakukuwa rasmi, hakukuwa kuna kundi lililompemda au kuna kundi lililomchukia daima. Maamuzi ya mfalme Njozi ndiyo yaliyopelekea au kupendwa na baadhi au kuchukiwa na baadhi kwa wakati huo.
Baadhi ya maamuzi ya mfalme Njozi kuna siku yaliwapendeza waliomchukia na kuanza kumpenda ghafla na kuna siku yaliwachukiza waliompenda na kuanza kumchukia ghafla. Maamuzi ya Mfalme njozi yalitokana, kwa asilimia kubwa, na njozi zake. Na kwa asilimia chache sana yalitokana na kufata ushauri wa wasaidizi wake.
Kuna siku Mfalme Njozi akipata Njozi yamepikwa mandazi ya nazi basi siku hiyo ataamrisha nyumba za raia zake wote zipike maandazi ya nazi. Wapenda mandazi ya nazi siku hiyo ikawa ni furaha na neema kubwa kwao na wasiopenda mandazi ya nazi ikawa ni chuki na karaha kubwa kwao, nchi yote ilinukia mandazi ya nazi kwa wayapendao na ilinuka maandazi ya nazi kwa wasioyapenda.
Huo ni mfano mmoja tu wa kuwaelewesha ni vipi Mfalme Njozi alitumia njozi zake kufanya maamuzi.
Bingwa wa saikolijia za siasa Jaap Van Ginneken amewahi kuandika (tafsiri isiyo rasmi) "Ikiwa saikolojia ni sayansi ya uzoefu (experience), tabia, mwingiliano wa mtu na makundi basi saikolijia ya siasa ni sayansi ya uzoefu wa kisiasa, tàbia ya kisiasa, mwingiliano wa kisiasa wa mtu na makundi.
Kwa kisa hicho cha Mfalme Njozi na saikolijia ya kisiasa kama alivyoielezea bingwa wa saikolijia (kwa kuifupisha), tukitazama mwenendo na maamuzi ya wanasiasa wa hapa Tanzania, tokea kabla ya Uhuru mpaka tupate Uhuru mpaka leo hii, jee, wana tofauti na Mfalme Njozi?
Nawatakia njozi njema wote mtakaoshiriki madà hii.

Mfalme Njozi... kweli watu walijua kuandika hapo zamani...
Wakatumia fasihi, nahau, misamiati na tafsida katika simulizi zao tamu...
Mfalme Njozi yeye aliongozwa na utashi wa njozi zake akiamini ndio mfumo sahihi na anawafurahisha raia wake pasi kujua kwamba mandazi yale ya nazi kuna wengi yakiwadhuru na kuwafanyia mzio aidha shida za wengine haikuwa mandazi bali mavazi!!!
Yawezekana Mfalme Njozi alikuwa tofauti sana na Mfalme Juha lakini kwa kuwa wote walikuwa wafalme ni lazima WALISHABIHIANA SANA maana katika ufalme wanaofaidika sana ni VIKARAGOSI wanaomzunguka MFALME huku wakimsifia na na kumhadaa kwamba kila kitu kiko sawa ili waweze KUJAZA MATUMBO YAO!!!
Njozi uzuri wake mtu anaweza miliki utajiri wa dunia nzima kukicha akaenda kukopa mandazi ya shilingi miambili!!!
NI NJOZINI TU MTU AWEZA KUWA SIVYO ALIVYO!!!