Tafakuri ya FaizaFoxy 2: Korosho

Mimi najiuliza swali moja Yale maghala makuu yamejaa korosho zilizokosa mnunuzi, na msimu mwingine unakuja, sijui wataziweka wapi. Ni dhahiri wanunuzi wanaweza wakarudi nyuma msimu ujao kwa hawajui wataingiliwa namna gani. Mkuu anaweza akamuru kama wanataka kununua korosho tz lazima wanunue Kwanza za kwenye maghala. Hapo ndo utakuwa mwisho marketability ya zao la korosho tz. Kaburi li wazi.
 
Thank you. A very good Idea....Mo simuamini sana mana muhindi kwao kulee atatugeuka tu
 
Wana CCM wengi sana ni wafanya biashara. Fatilia utaona. Hata wale wakubwa. Pia wabunge na madiwani wengi wa CCM (Kama si wote) ni wafanya biashara mbali mbali.

Huo ushauri wako hauna maana yoyote kwa CCM. Been there done that.
 
Pamoja na mawazo yangu duni, unafikiri hilo ni wewe wakwanza kushauri?? Ndio maana nikakwambia katika taifa ambalo limeshawahi kupewa kila aina ya ushauri basi tanzania ni namba moja, TUMESHAJIULIZA KWANINI KILA USHAURI MZURI HAUFANYIWI KAZI?? - TAMBUA HII SIO BAHATI MBAYA BALI WANATAMBUA KILA WAFANYALO..

Kila kukicha toka enzi za Nyerere watu walishauri juu ya kuweka nguvu sekta binafsi na kuifanya iwe strong kiasi pia ya kuwekeza kila mahala kuanzia kwenye muhogo mpaka Korosho..Sekta binafsi sio tu kilimo kila mahala hata viwandani, transportation, majini na kwenye elimu nk but who cares??.

Tanzania imebalikiwa kila mahala lakini Tanzania pia ndio yenye shida kila mahala..tunashindwa wapi? Kama tuna nguvu kazi ya watu zaidi ya milioni 50???. Kwanini tusiseme kipo chanzo cha matatizo yote ya Tanzania ambacho ni CCM..
 
Poleni sana...

Kwani mfumo wa zamani wa ukusanyaji na ubanguaji ulikua na kasoro zipi?

Tatizo ujuaji mwingi ndiyo umepelekea haya yote..

Cc: mahondaw
 
Kila zama na kitabu chake.

CCM wanashaurika sana tena sana, ingekuwa hawashauriki usingeona Rais anaitisha mikutano na vikundi tofauti tofauti ili kusikiliza maoni yao.

Ukisoma huelewi basi hata picha huoni?
 
Poleni sana...

Kwani mfumo wa zamani wa ukusanyaji na unanguaji ulikua na kasoro zipi?

Tatizo ujuaji mwingi ndiyo umepelekea haya yote..

Cc: mahondaw
Hakuna kasoro bali biashara ni ubunifu, ushauri umelenga katika kuzidisha thamani ya zao la korosho.
 
Wana CCM wengi sana ni wafanya biashara. Fatilia utaona. Hata wale wakubwa. Pia wabunge na madiwani wengi wa CCM (Kama si wote) ni wafanya biashara mbali mbali.

Huo ushauri wako hauna maana yoyote kwa CCM. Been there done that.

Waache ubunge wajikite kwenye biashara maana huko kwenye siasa ndio wameharibu kwa kutoa rushwa, kufanya ukatili nk ili washinde. Kama unaweza kunisaidia unaweza kuniambia Profesa Kabudi kiwanda chake kiko wapi? Ukiweza nitajie na kiwanda cha Makonda kilipo nikaombe ajira.
 
Naona udini umeweka pembeni kwa muda, hongera
Udini haachagi huyo,ukisoma kiutulivu utagundua udini uliomo kwenye uzi wake huu..msome vizuri
Enzi za alhaj kikwete alikuwa hatoi ushauri,sasa hivi ushauri mwingi implying that things ain't going well wakati jakaya ndo katufikisha hapa
 
Hakuna kasoro bali biashara ni ubunifu, ushauri umelenga katika kuzidisha thamani ya zao la korosho.

Na umetaja serikali ijaribu kukopesha wafanyabiashara wakubwa wenye uzoefu na biashara ili waweze kuboresha zao la korosho...

Hilo linawezekana, ila hao wafanyabishara wanakwepa masharti magumu yaliyopo kwenye hilo zao...

Cc: mahondaw
 
Tafakuri imelenga ku add value, kama hatuja add value ya mazao yetu vipi kipato cha wafanyakazi kitaongezeka?
 
Kila zama na kitabu chake.

CCM wanashaurika sana tena sana, ingekuwa hawashauriki usingeona Rais anaitisha mikutano na vikundi tofauti tofauti ili kusikiliza maoni yao.

Ukisoma huelewi basi hata picha huoni?

Kuna hivi vitu bibi.
preventive maintenance = fix before failure.
Breakdown maintenance = fix after failure.
Kikao =breakdown maintenance..
Tunataka kurekebisha baada ya tatizo wakati watu walishauri kabla ya tatizo na sio hili tu yapo mengi sana..

Athari za kutengeneza baada ya tatizo ni kubwa na wanaozibeba wananchi kila siku na hakuna wakuwafidia na bado tunaendelea kuishi kwa majaribio mwaka wa 50 sasa huku wanaoumia na kuendelea kuwa masikini ni watanzania..

CCM hawakuwahi kushaurika na hawatashaurika maana kwasasa Tanzania ni mali yao na watanzania ni misukule yao hivyo tutaendelea kuishi sana kwa majaribio..
 
Na umetaja serikali ijaribu kukopesha wafanyabiashara wakubwa wenye uzoefu na biashara ili waweze kuboresha zao la korosho...

Hilo linawezekana, ila hao wafanyabishara wanakwepa masharti magumu yaliyopo kwenye hilo zao...

Cc: mahondaw
Masharti siyo misahafu ya Mungu, yanabadilika.
 
Hayo maisha ya kila siku, uamuzi mmoja unaweza ukaharibu lakini kuharibu ndiyo kujifunza. Hutarudia na inabidi utafute njia mbadala.
 
Udini haachagi huyo,ukisoma kiutulivu utagundua udini uliomo kwenye uzi wake huu..msome vizuri
Enzi za alhaj kikwete alikuwa hatoi ushauri,sasa hivi ushauri mwingi implying that things ain't going well wakati jakaya ndo katufikisha hapa
CCM ni ile ileee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…