Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,848
- 730,372
Kinachoendelea Zanzibar kinatisha, wale wote walio kinyume na ccm wanatekwa au kukamatwa live kupata mkong'oto kufungiliwa mashtaka mabaya ya kubuni na kutupwa lumande au kutupwa porini ukiwa hoi.....hali hii haitofautiani sana na huku Tanganyika bara japo huku kwa sehemu kubwa wanaofanyiwa hivyo ni viongozi na wabunge wa upinzani (CHADEMA, kule Zanzibar visiwani ni wanachama, wapenzi, wakereketwa wa CUF na viongozi wao
Kuna hii safu mpya inayoendelea kusukwa na Magufuli safu ya viongozi na wakuu wa idara mbalimbali za serikali...wengi kama si wote ni watu wa NDIO MZEE watu wa maguvu bila hekima wastaafu na vijana wenye uchu wa madaraka na matarajio makubwa...hii ni safu hatari kwa mustakabali wa demokrasia na siasa huru
Inaundwa mahakama ya mafisadi ni jambo jema sana, nchi ilifika mahali ikawa zaidi ya shamba la bibi au mzoga wa kiboko kila mnyama mla nyama alikuja akajing'atia pande lake...lakini hii mahakama ni ya muda...ikishamaliza kesi za mafisadi wote mahakimu na majaji watakuwa hawana kazi. Itabidi watafutiwe kazi second phase ya hii mahakama ni viongozi wa upinzani na wanachama wao..kesi za kubambikiwa zinakuja kesi za kuhujumu uchumi kesi za kuhatarisha usalama wa nchi....hizi zinakuja
Magufuli kasema haitaingilia mambo ya Zanzibar lakini atahakikisha usalama wa watu wa Zanzibar (wanaccm?)manake kinachoendelea huko Mungu pekee ndie ajuaye na ndio hicho hicho kitakachotokea Tanganyika bara 2020
Kwasasa tunamuona ni mzuri sana kwa jinsi ya utendaji wake ambao tuliutamani kwa miaka 30 hivi.kwamba hivi ndivyo mambo yalipaswa yawe bado tuko kwenye kiwewe na shangwe za watu kutumbuliwa majipu..lakini tunamuumba Kagame mwingine Museveni mwingine Mugabe mwingine
Kagame baada ya vita ya kimbari ya 1994 kwa miaka kumi ya kwanza akafanya kazi nzuri sana ikaongezeka mitano akapata sifa kubwa kitaifa na kimataifa leo hii Rwanda iko vizuri kiuchumi na mambo mengine lakini sio demokrasia, siasa huru za uwazi usawa na usalama... viongozi wengi wa upinzani wameuawa na wengine wamekimbia nchi
Kinachotokea kwa sasa kwenye ulingo wa siasa hakina dalili njema huko tuendako