Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 262
- 466
Licha ya jitihada mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanyika kuboresha Mahakama Nchini ili kuwezesha mazingira rafiki ya utoaji haki lakini bado kuna changamoto ambayo ni kero kubwa licha ya kutoelezwa mara kwa mara 'uenda ni kutokana na hofu', lakini naamini kupitia jukwaa hili ujumbe utawafikia wahusika.
Baadhi ya Mahakama ambazo nimebatika kufika zilizopo Jijini Dar es salaam, hususani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mahakama Kuu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni (Kituo cha Utoaji Haki) baadhi ya kumbi zake ambapo kesi zimekuwa zikiendeshwa bado azina mifumo rafiki ya sauti ambayo inawafanya wafuatiliaji wa kesi kusikia vizuri mawasilisho yanayofanywa kwenye vyomba vya Mahakama.
Kwa mara kadhaa nimekuwa nikiwaona Mawakili, Waandishi wa habari pamoja na wadau wengine ambao ufika Mahakamani kwa ajili ya kesi wakipata shida kusikilizana hasa kile kinachowasilishwa ndani ya vyumba vya Mahakama.
Lakini kingine ambacho ni hatari zaidi hata kuna wakati unaona Jaji au Hakimu akipata shida kusikiliza Mawakili au mashahidi wakati wakiwasilisha maelezo, changamoto hiyo pia inaonekana wazi kuwapa tabu makalani wa Mahakama ambao utekeleza jukumu muhimu la kutunza kumbukumbu.
Changamoto hii imekuwa ikijitokeza zaidi haswa kwenye kesi zinazoonesha kuwa na mguso zaidi kwa umma (Public interest) ambazo huudhuzuliwa wadau mbalimbali, ikiwemo Wanahabari na wanaharakati.
Kwenye Mahakama nilizotaja baadhi ya kumbi unakuta zipo feni za kawaida, ambapo kulingana na wingi wa watu ambao hufika kufuatilia kesi wahusika wanalazimika kuwasha feni hizo ili kupunguza joto lakini feni hizo zimekuwa pia zikichangia zaidi hali ya kutosikika.
Hali hii uenda ikawa na athari katika mienendo ya kesi au wakati mwingine inaweza ikawapelekea Waandishi wa habari kufanya makosa ya kunukuu vitu ambayo sivyo vya kweli, jambo ambalo badae linaweza kutafsiriwa kama kosa, lakini hali hiyo inaweza kuwaweka wanahabari katika uwezekano wa kuupotosha umma.
Ni muhimu sasa Mamlaka kuhakikisha kumbi za Mahakama hasa ambazo ni kwa ajili ya kesi za wazi zikawekewa mifumo rafiki ya sauti ili kutoa fursa ya kusikilizana vyema. Maboresho hayo yakifanyika yataongeza tija katika mienendo mizima ya usikilizaji wa kesi.