MUSIGAJI
JF-Expert Member
- Dec 26, 2014
- 2,187
- 2,462
Wakuu amani iwe kwenu,
Siku ya leo Mh Rais amezungumza na wahariri juu ya mambo mbalimbali yaliyofanyika katika mwaka mmoja huu wa utawala wake. Mtakumbuka kuwa katika kipindi hiki kuna habari ya utumbuaji majipu ambayo kimsingi imemjenga kisiasa Mh katika huu mwaka mmoja kwa watu wa kawaida.
Tumekuwa tukishuhudia watu wakitumbuliwa katika nafasi zao na wengine kufikishwa mahakamani kama kina Masamaki.Hawa watu wengi walifanya makosa/ubadhilifu kabla ya serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani lakini serikali hii imewawajibisha ni jambo jema sana.
Leo katika hotuba ya Mh Rais amezungumza jambo moja ambalo kimsingi limeendelea kunifikirisha sana,suala la ufukuaji makaburi.Mh amesema hayupo kufukua makaburi maana akiyafukua mengine atashindwa kuyafukia hivyo yeye ataanzia hapo tu alipoikutia nchi hataangaika na yale mengine yaliyopita.
Ametoa mfano wa fedha za kiwanda kule Lindi zilivyotafunwa na amekiri kuwa waliozitafuna wapo.
Sasa katika hali hii watu wanapokuwa wakizungumza kuwa wanaotumbuliwa na kupelekwa mahakamani ni vidagaa wale manyangumi tutawezaje kumbishia mtu anayesema hivyo.Mtu akisema hii ni doubles standard si atakuwa sahihi?
Kwa nini hawa watendaji wengine wakurugenzi wawajibishwe kwa mambo yaliyofanyika katika awamu ya nne wakati huohuo waliohusika na ufisadi mkubwa namna hii ambao bila shaka walikuwa/ni wanene wasiguswe kwa kuogopa kufukua makaburi?.