Tafakuri: Rais Magufuli hakutafakari kuhusu suala la kurudisha machinga katikati ya mji

Kiuhalisia hakujishauri vema na au hakuhitaji ushauri. Nasema hivi kutokana na kauli yake kuwa wamachinga wale wa mwanza ndio waliomchagua kwa kura nyingi. Kwa maneno mengine anawalipa fadhila kwa kuwaacha wao wavunje sheria.
Ushauri wangu kwa hao wateule wa mwanza jiondoeni tu ofisini mje huku kulima nyanya.
Hivi hana wataalamu washauri na waelekezi wa namna ya kuzuia migogoro (conflict managers)? Atuajiri tumsaidie.
 
Ninaamini wewe mleta mada rais angeweka msisitizo kuwa machinga watimuliwe ungesema rais kakosea,
Sasa bora wakati mwingine muwe mnakaa kimya,maana kwenu hakuna zuri wala baya,,
 
Ninaamini wewe mleta mada rais angeweka msisitizo kuwa machinga watimuliwe ungesema rais kakosea,
Sasa bora wakati mwingine muwe mnakaa kimya,maana kwenu hakuna zuri wala baya,,
Machinga ni vijana wanaokimbia maisha magumu vijijini, utawapangia eneo gani mjini waenee? hii ni ishara tosha kuwa kuna tatizo, na CCM ndio mwasisi wa sakata hili.
 
Tatizo hao rais anaowachagua wanakurupuka kujaji.wee utaanzaje kuwafukuza watu bila kuwaandalia sehemu ya kwenda kufanyia kazi au unafikiri wamachinga sio binadamu wenye haki.

Tatizo kubwa la Tanzania atupendi kutibu matatizo tunapenda kuongeza matatizo.
Hao wamachinga waliletwa na serikali? Je mitaji walipewa na serikali? Sula LA kuondoka na kutafuta sehemu rafiki ya kufanya shughuli zako, ni wewe mwenyewe. How and why uisumbue serikali ikutafutie eneo ilhali ulichagua wewe mwenyewe kuwekeza eneo hatarishi? Hapa Rais Wangu kapotea vibaya, mikoa yote INA marching guys kibao nini kitatokea jibu unalo.
 
Hao wamachinga waliletwa na serikali? Je mitaji walipewa na serikali? Sula LA kuondoka na kutafuta sehemu rafiki ya kufanya shughuli zako, ni wewe mwenyewe. How and why uisumbue serikali ikutafutie eneo ilhali ulichagua wewe mwenyewe kuwekeza eneo hatarishi? Hapa Rais Wangu kapotea vibaya, mikoa yote INA marching guys kibao nini kitatokea jibu unalo.
machinga ni bomu linalosubiri kulipuka subiri tu waendelee kuongezeka mjini, maeneo ya kupanga bidhaa zao chini yakiisha watahamia sehemu ya wazi hata kama itapatikana Ikulu.
 
Mwanzoni walisema Magufuli hawezi sababu tatizo ni mfumo.

Baada ya kuanza kuwatumbua mafisadi wenzao wakasema ni nguvu ya soda.

Baada ya mwaka mzima kuisha huku sindano zikiwaingia kwa kasi ile ile na soda haiishi nguvu, sasa wameanza kupongeza!

Safi sana Yericko, natamani ufipa yote ipokee ubatizo wa moto kama uliopokea wewe na hatimaye kuungana na rais bora kabisa duniani kulijenga upya taifa la Tanzania.
 
ameandika Dotto Bulendu

Nikiwa mwanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe,nilisoma somo linaitwa utawala bora(Good governance),niliambiwa dhana hii ya utawala bora ina misingi yake,miongoni mwake ni Rule of law(utawala wa sheria),matumizi sahihi na stahiki ya rasilimali,haki za binadamu,ushirikishwaji,uwajibikaji n.k. Dhana ya uwajibikaji niliambiwa imegawanyika katika mafungu matatu,uwajibikaji wa kisheria(legal accountability),uwajibikaji wa kiutawala(administrative accountability)na uwajihikaji wa kisiasa(political accountability). Dhana zote hizi tatu zinagawanywa katika makundi mawili,uwajibikaji wa pamoja(collective accountability) na uwajibikaji wa mtu mmoja mmoja(individual accountability). Wataalam wa masuala ya uongozi wanasema katika maeneo yote matatu ya uwajibikaji,kitaasisi ama kiserikali kila mnapowajibika inashauriwa kuzingatia dhana ya uwajibikaji wa pamoja(collective accountability),dhana hii inasaidi kuonesha mnaowaongoza kuwa mpo pamoja,mnafanya mambo pamoja,individual accountability ina ukakasi kutokana na kuweka uwezekano wa kuonesha kuwa kila mtu ana lake . Kilichofanyika kwenye sakata la machinga jijini Mwanza,ni kuonesha kuwa serikali haizingatii misingi ya utawala bora hususuni uwajibikaji wa pamoja(collective accountability). Kitendo cha Rais kusubiri wasaidizi wake wawafurushe machinga na yeye aje kuwarudisha huku akitumia lugha ya kuwatisha,kitaalam inaitwa "individual accountability",huu ni mfumo ambao kila mtu anawajibika kivyake,tatizo la mfumo huu mlio chini kila siku mtaonekana hamfai,mkuu anakuwa katika nafasi kubwa ya kujisafisha ili aonekane hana kosa,mlio chini mnabidi muwe makini kwenye kuamua jambo lolote. Athari za individual accountability inaweza onesha kama taasisi ama idara hampo pamoja,hamna dira wala maono,kila mtu anafanya atakavyo. Si mfumo mzuri kiutawala,huu mfumo wa uwajibikaji wa mtu mmoja mmoja ndiyo alioutumia Rais kutatua tatizo la machinga,Rais kawavua nguo wasaidizi wake,sijui wasaidizi wa Rais jijini mwanza wanazificha wapi sura zao? Kama Rais angekuwa anaongoza kwa kuzingatia msingi wa uwajibikaji wa pamoja,katazo hili angelifanya kabla ya siku ya utekelezwaji wa zoezi hilo,na katazo hilo asingelitoa yeye,angemwambia mkuu wa mkoa asitishe na Tangazo hilo lingetolewa na mkuu wa mkoa ili wawe na heshima mbele ya jamii ya watu wanaowaongoza. Mfumo alioutumia Rais umewavua nguo wasaidizi wake,kawapora nguvu zote walizokuwa nazo,sasa si lolote mbele ya jamii ya machinga. Nadhani Rais angebalidi stlye yake ya kuongoza asiongoze kwa dhana ya uwajibikaji wa mtu mmoja mmoja,atumie dhana ya uwajibikaji wa pamoja(collective accountability),madhara ya individual accountability ,inajenga hofu kwa wasaidizi,inaweza sababisha wasaidizi wako wakawa waoga kutenda jambo wakihofia kudhalilika kama ilivyowakuta viongozi mkoani Mwanza. Kama Rais ana nia njema na viongozi wa mkoa wa Mwanza,ni vizuri akawapa uhamisho viongozi hawa,kiutawala Mh Rais ni vizuri akabadilisha style yake.
Nb moderators please iacheni kama ilivo
 
Ktk mambo aliyoniboa JPM ni hili. Amenikera sanaaaa. Amenikera mno. Yaani anashindwa kutumia simple common sense? Real? Hata kama ni kutafuta sifa, hii ni zaidi ya uhun.i. Kwa hiyo viongozi watimize majukumu yao kwa kushikiwa akili? Mkulu waamini wateule wako, acha kuwavunja morale, ogopa kuongoza maroboti, yakikugeuka hakuna wa kukusaidia

Ktk mambo aliyoniboa JPM ni hili. Amenikera sanaaaa. Amenikera mno. Yaani anashindwa kutumia simple common sense? Real? Hata kama ni kutafuta sifa, hii ni zaidi ya uhun.i. Kwa hiyo viongozi watimize majukumu yao kwa kushikiwa akili? Mkulu waamini wateule wako, acha kuwavunja morale, ogopa kuongoza maroboti, yakikugeuka hakuna wa kukusaidia

Inaonekana wewe ni mnyanyasaji, mbinafsi au ni kati ya hao wakuu ambao hawana ubunifu au ni marobots kwani ni busara na utu tu vinahitajika katika swala hili. Wapatie eneo lingine, wajengee vibanda, wawekee maji, vyoo, Umeme halafu kaa nao kikao ili wahame kwa utaratibu. Wanashindwa nini hapo?
 
Ukweli machinga ni shida. Hawa wa mwanza tayari mali zao zimefukiwa kwenye madampo.
Suala lao ni la miaka 30 sasa..na kila mwaka ni same issue. Fukuza , ondoka rudi..tangu enzi za Mwinyi walipo anza , wakati wa mkapa ..ingawa mkapa alikuja na solution ya hapa na pale mfano sunday markets nk ilisaidia lakini rudi fukuza ilikuwepo
Wakati wa kikwete nae alijaribu sana kuwafungulia sehemu mbali mbali ili waondoke barabarani ...alifanikiwa kidogo...machinda waliondoka ..ila kama kawaida siasa zetu za kudanya dangaya..wakaachiwa karibia na uchaguzi, wakajaa kibao kioa mahali.
Awamu hii wakahamishwa na makonda na akaweza kwa kiasi kufanikiwa. Mkuu aliporudi kutoka dodoma baada ya kupewa uenyekiti akihutubia lumumba akawarudisha ...barabara zikafunikwa na wenye maduka wanao lipa kodi wakawa na hali ngumu.
Baadae waziri na wakuu wa mikoa wakaona ile shida nao wakaaka wawatoe.kusagisha miji...watu wafanye biashara kwa amani...mkuu akawarudisha tena na kutoa onyo kuwa wasibughudhiwe yeye ni raia wa wanyonge.
Na sasa wametudi kwa jeuri kubwa zaidi . Katiakoo kwa mfano wamejaa na suala la usafi limekua myihani.
Kuwapo wamachinga upande mmoja ni njia nzuri ya kukwepa kodi...na kuuza bidhaa bila ya risiti.
Mavhinga huchukua bidhaa hizi kwa wauza jumla , na wengi hawachukui tusiti halisi ili wapunguziwe na wapate faida zaidi...na wao pia hawalipi kodi na risiti hawatoi..hivyo zoezi hili ni pigo kwa TRA kwani wanashindwa kukusanya kodi ipasavyo na mwanya wa kukwepa unakua mkubwa na huwezi kuu control
Ukiangalia mavhinga hawauzi bidhaa za kwao au kutengeneza wao bali wanauza bidha za kutoka nje kama nguo viatu mitumba saa miavuli na vitu vya electrinic...hivi wengine ambao wanaaminiwa huchukua kutoka kwa magodown na wakiuza wanarejesha kwa wenye mali.
Upande mwengine wale wenye maduka yenye kuzungukwa na wamachinga basi biashara hupungua sana kutokana na kukosa wateja kwani machinga bei poa yeye halipi kodi , halipi pango halipi mshahara....hivyo retail hii inapungua na EFD mashine zinakua likizo...pigo jengine kwa TRA.
Suala la machinga sio la kuangalia hawa watanipa kura bora niwachie tu...suala hili linatakiwa kungaliwa kwa upana zaidi...kuwapiga matufuku haiwezekani lakini sio suala la kusema hawa masikini kwanini wasifanye biashara mjini ?
Kila kitu kina taratibu zake na principles...sio kila mahala ni pa kufanyia biashara...inatakiwa mipango madhubuti kuwa wezesha hawa vijana kujiajiri . Kujenga maeneo maalum kwa ajili ya wachuuzi yaani wamachinga,..
Kuanzisha sunday markets
Kuwapa uwezo kuanzisha biashara za maana , ufugaji , kilimo nk ili nao walipe kodi...hili la kutembeza chupi barabarani sio kazi na sio utaratibu wa nchi nyingi funiani...rafiki yetu kagame hawaruhusu hawa kukaa nje ya maduka au barabarani....kigali ni safi...kuna principles wamejiwekea sio suala la kura za masikini...au wanyonge
Juzi tulikua na machinga elfu tano, leo tunao laki moja kesho kutwa tutakua na machinga million moja....kwa bara bara gani tulizo nazo ?
Kama suala la mjini badi tuwaruhusu watandaze bidhaa zao masaki , na mikocheni kwa pia huko ni mjini...na wanyonge pia wanataka kuona bahari
 
Katika suala la Machinga mimi binafsi natofautiana naye sana katika uamuzi wake wa juzi.
 
Machinga watengewe maeneo yao bhana, kuwa na machinga katikati ya miji inakua ni usumbufu kwa watu na miji inaonekana haina ustaarabu na mipangilio na muda mwigine kunakuwa na ongezeko la wizi , kuna machinga na waendesha boda boda wote wanatakiwa wawe na sehemu yao maalum, wakuu wa mikoa walikuwa sahihi kabisa kwa kuwapeleka sehemu maalumu ambayo walikuwa wameitenga kwa machinga, Raisi magufuli kwa hili hakuwatendea haki wateule wake,Raisi asiangalie kura tu za machinga/waendesha boda boda akawa anatoa maamuzi ambayo yanakinzana. Kama ana huruma na machinga na ahataki waondolewe katikati ya miji basi aanze kujenga majengo makubwa ya serikali ghorofa kuanzia tatu au tano na kuwaweka ndani hao machinga ili wafanye biashara zao indoor na serikali ikusanye kodi, sio hivi wanavyofanya ,yaani mji unaonekana uko holela tu.
 
Kauli ya CCM kwa wamachinga na mama nitilie wote Tanzania.

Je kwako wewe ambaye hauko kwenye kundi tajwa hapo juu unasemaje?
 
Haya makundi ya wamachinga yamepoozwa tu kwa muda..

Ngoja baada ya muda wataipata Habari yao.

Hii sio Serikali ya kuiamini hata chembe.
 
KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA MKOA NA WILAYA INATOA TAARIFA YA HALI ya USALAMA YA WILAYA NA MKOA KILA SIKU KWA MUDA MAALUMU KWA RAIS,. NAAMINI HATA KABLABYA ZOEZILILE KUFANYIKA, MKUU ALIKUWA NA TAARIFA KUWA ENEO MOJA NDANI YA NCHI YAKE KUNA jambo LINAFANYIKA DHIDI YA RAIA LIKIWASHIRIKISHA ASKARI MGAMBO NA WENGINEO. SO ALIJUA,. KWANINI ASINGESITISHA MARA MOJA KABLA YA MADHARA? INAKUAJE BAADA YA MADHARA NA HASARA ATOE AGIZO HILI?!
NI KWELI MACHINGA KAMA RAIA WENGINE WANA HAKI, LAKINI ISIWE KWA STAHILI HII.
SIJUI IWAPO WATAENDA MAHAKAMANI KUDAI FIDIA ITAKUAJE?! MTAJI WA WANASHERIA HUO.
 
Amekwambia anatoa agizo mara ya pili wewe unasema hakutafakari, acha zareu
 
Back
Top Bottom