Kiungani
JF-Expert Member
- Feb 2, 2007
- 274
- 71
Uongozi ni ushawishi. Uongozi siyo kutegeana, kutegeshana, kunyemeleana na kufukuzana. Na uongozi siyo vitisho au mikwara. Kiongozi anayeishi kwa vitisho ni kiongozi aliyeshindwa hoja. Hili ni kweli kwa vyama vile vile; chama kinachoishi kwa vitisho kimeshindwa hoja. Tafakari
Natafakari na nazidi kuelewa nini maana ya TANU/AFRO SHIRAZ/CCM kushindwa kwa HOJA kwa kuwatimua Mtemvu, Fundikira, Msangi, Hanga, Maalim Seif, Jumbe, Babu, n.k.
Huko kulikuwa ni kushindwa kwa hoja kwa uongozi wa Mwalimu JKN. Uongozi siyo vitisho wala mikwara.
Vile vile natafakari na kuelewa kukubalika na kutoshindwa kwa hoja kwa Mwenyekiti JMK kwa kutowavua magamba mapacha watatu: Lowassa, Rostam na Chenge na mafisadi kedekede ndani ya CCM, pamoja na wale waliopata nafasi zao kwa rushwa za uchaguzi.
Huu ndiyo uongozi uliokubuhu na usiyo na vitisho wala mikwara. Hakuna mambo kama vile kupeana siku 90 kwa magamba kujivua au wale walioshinda NEC kwa rushwa "kushughulikiwa" ndani ya miezi 6. Uongozi siyo vitisho wala mikwara.
Mwanakajiji, with all due respect, nashindwa kukuelewa na hii tafakuri yako. Is it not the case of what is good for the goose?
Pia kama mwana-CCM nitategemea kuwa chochote CDM, TLP au NCCR inachofanya kujidhoofisha ni baraka kwa CCM kwani kuvuja kwa pakacha.............!!!!
Sijawahi kuona bondia anamuongezea lishe bora mpinzani wake ili pambano liwe zuri.