Tafakari ya 9 Disemba: Leo ni siku ya Uhuru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tafakari ya 9 Disemba: Leo ni siku ya Uhuru

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mshirazi, Dec 8, 2009.

 1. Mshirazi

  Mshirazi JF-Expert Member

  #1
  Dec 8, 2009
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wanabaraza, kesho ni siku kubwa kwa Taifa hili,,lakini hapa barazani mbona tumeisahau kabisaa...kama vile haina maana kwetu, KULIKONI!!
  Kama sio tarehe 9 December Tanzania Ingekuepo?
   
 2. S

  Sir Leem JF-Expert Member

  #2
  Dec 8, 2009
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 564
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Wengi wa members wamezaliwa baada ya uhuru tena wengi wao wa 70`s na 80`s hawaoni umuhimu wa kujadili au kuisherehekea!!!
   
 3. B

  Bobby JF-Expert Member

  #3
  Dec 8, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  I thought you knew the reason? Sababu ni kuwa hiyo tarehe uliyoitaja hakuna kilichofanyika zaidi ya kubadili rangi ya wakoloni kutoka weupe kwenda weusi. Na kwa taarifa yako ukoloni huu wa sasa unauma kuliko ule wa weupe kwani mtanzania mwenzio kbs wa Bagamoyo anakufanyia mambo ambayo hata mwingereza wa London asingeweza kukufanyia- It is very sad kwa kweli.
   
 4. Y

  Yetu Macho JF-Expert Member

  #4
  Dec 8, 2009
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Watanzania hawanasababu ya kuikumbuka hii tarehe. Hawaoni utawala uliopo umewafanyia nini. Uhuru wa kusiasa hauna maana kama hauleti mapinduzi na uhuru wa kiuchumi.

  Tunapoelekea hiyo tarehe "sitaki kuitaja" watanzania wanaendelea kutonesha vidonda vyao kwa kujiuliza kwanini ilitokea, kwanini tusingebaki mikononi mwa wakoloni weupe ambao matumbo yao yalikua yuanashiba kuliko hawa wa sasa weusi na wenye nyele zakuvutika vutika ambao wanatamani wachukue kila kitu hata ikiwezekana na kile kibanda alichoacha babu pale salamander.

  Wakati wakoloni weupe wakiwepo, ingawa walitulimisha kwenye mashamba ya mkinge kule Tanga na kuchukua kahawa yetu kule Kilimajaro, walituongoza tukajenga reli na barabara kuwasaidia wao na sisi kwa usafiri. Bahati mbaya reli hii imeondoka na wao ingawa tunaihitaji sana

  wakati wakichukua pamba yetu kule mwanza na tumbaku yetu Tabora, reli ya kati ilifanya kazi kuwasaidia wao na sisi. Leo wamepewa wenywe nyele za kuvutika sijui nii semee nini hii reli............

  Haya na mengi etc etc yanafanya watanzania tuumie tunapoisikia hii Tarehe. Ni bora tuikumbuke tar 14 Oct maana maana aliebeba maana ya kweli ya hiyo tarehe aliondoka. Mwalimu ndie pekee aliekua na nia ya dhati na taifa hili ingawa alifanya makosa kidogo ni udhaifu wa kibinaadamu na mungu ailaze roho yake peponi.

  Baada ya hapo walobaki wote wanalibaka taifa hili na rasilimali zake na watanzania hatunasababu kushereheka na wabakaji wa taifa hili. Siku ya kweli ya kusherekea na kukumbuka yaja pale ambapo mapinduzi ya kisiasa kupitia sanduku la kura yatauondoa utawala huu wa kidhalimu na wabakaji hawa wa CCM.
  Hii ndio siku watanzania wataikumbuka daima na wataifurahia na kushangilia. Maana hii ndio siku ya uhuru wa kweli.
   
 5. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #5
  Dec 9, 2009
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Wakati wetu ni huu, tunapoadhimisha miaka 48 ya uhuru. Ni wakati wa kutafakari taifa letu lilipotoka, lilipo na tunapotaka liende. Makala hii inakulenga zaidi wewe uliyezaliwa baada ya uhuru; tunaounda sehemu kubwa ya taifa hili. Ni kwa ajili pia ya watanzania wote wenye kuamini kwamba uhuru wa kweli, si uhuru wa bendera bali ni uhuru dhidi ya umasikini, ujinga, maradhi na ufisadi. Uhuru wa kweli, ni uhuru wenye kuleta maendeleo kisiasa, kijamii na kiuchumi. Uhuru huu utapatikana kupitia mabadiliko ya kweli, yenye kuhimili misukosuko ya ukoloni mamboleo; na kujenga taifa lenye kutumia vizuri rasilimali katika kutoa fursa kwa raia wake.

  Wakati wa uhuru taifa hili lilikuwa na watu chini ya milioni 10; sasa Dar es salaam pekee ina wananchi takribani milioni nne, karibu nusu ya Tanzania ya wakati huo ikiwa Tanganyika. Sasa taifa lina watu takribani milioni 40; hivyo taifa letu watu wake takribani robo tatu ni kizazi cha baada ya uhuru. Maanake katika kila watu kumi tunaopishana nao barabarani, saba ni kizazi cha baada ya uhuru. Hiki ni kizazi chetu, hili ni taifa letu. Huu ni wakati wetu, tusidanganyike kwamba wakati wetu bado. Ujumbe kamili huu hapa: http://mnyika.blogspot.com/2009/12/miaka-48-ya-uhuru-huu-ni-wakati-wetu.html

  Hata hivyo, nchi yetu ni zaidi ya vijana; hivyo, baadaye leo nitapanua zaidi hii tafakari katika hotuba yangu ya ufunguzi wa Kongamano la Siku ya Uhuru lenye ujumbe "Mabadiliko ya Kweli; Uhuru wa Kweli"

  Nawatakieni heri ya sikukuu

  JJ
   
 6. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #6
  Dec 9, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,401
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Ni lini wakati ulikuwa si wako au wa vijana? Please we need change, a big change, not on genda, or age; but on our thinking/mindset. Mie sijaona tofauti ya mindset ya vijana na wazee. Labda ungesema vijana waongoze hizo changes, na ilenge kwenye thinking. Things like Charisma, Civic Education, flow of information, human rights, good governance and a war on corruption (rule of law).
   
 7. p

  pekupeku Member

  #7
  Dec 9, 2009
  Joined: Dec 6, 2009
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  vijana nao wakiwa engaged kwenye ufisadi ndio basi tena
   
 8. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #8
  Dec 9, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  taifa linakaribia takriban miaka 50 sasa! nusu karne...kwa hiyo waache kusema 'taifa letu changa'...maana ndio kisingizio cha maendeleo kudorora siku zote
   
 9. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #9
  Dec 9, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,037
  Likes Received: 23,817
  Trophy Points: 280
  Bado changa sana! Miaka 50? LOL!
   
 10. K

  Kinyikani Member

  #10
  Dec 9, 2009
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 65
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  SASA HUU NI UHURU WA TANGANYIKA AU waTANZANIA??
   
 11. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #11
  Dec 9, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,037
  Likes Received: 23,817
  Trophy Points: 280
  Uhuru Wa Tanzania bara. Tanganyika walishaiua eti. Lakini cha ajabu leo utapigwa wimbo wa Taifa La Tanzania!
   
 12. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #12
  Dec 9, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hakuna nchi inayoitwa Tanzania bara, December 9 ni maadhimisho ya uhuru wa Tanganyika. Unapofanya maadhimisho ya kitu si lazima hicho kitu kiwepo.

  Watu mpaka next year watasheherekea birthday ya Bob Marley, ingawa Bob Marley kafariki miaka mingi tu na harudi tena.

  Zanzibar ilipata uhuru wa bendera December 19 1963 lakini Wazanzibari wengi hawaitambui tarehe hii na wanatambua uhuru ulikuja na mapinduzi January 12 1964. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliounda Tanzania ni April 26, December 9 has everithing to do with Tanganyika and next to nothing with Zanzibar, and by induction, Tanzania.
   
 13. m

  matambo JF-Expert Member

  #13
  Dec 9, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 728
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  kwani tarehe 9 disemba kuna maadhimisho ya nini?nchi iliyopata uhuru kutoka kwa wakoloni tarehe hiyo haipo tena duniani,na nchi inayoadhimisha tarehe hiyo haikuwahi kutawaliwa kabla ya 1961 ila imeanza kutawaliwa tangia 26 april '64 tena wakoloni hawa wamezidi kuwa wabaya kadri miaka inavyozidi kwenda mbele,
  tunahitaji kutafuta uhuru wetu tena
   
 14. m

  mfundishi Member

  #14
  Dec 9, 2009
  Joined: Aug 27, 2008
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Tatizo la msingi linaanzia hapo, tunaposema "uhuru wa taifa letu" tunamaanisha nini? Je Tanganyika ndiyo Tanzania? Historia hapa imepinda. Tunaambiwa kuwa hakuna taifa la Tanganyika, hivyo ki mizania maadhimisho hayo yanakosa maana. Tujitambue!
   
 15. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #15
  Dec 9, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Uhuru hauna maana .....nchi haina mwenyewe wala control.....
   
 16. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #16
  Dec 9, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tanzania haijawahi kuwa huru! Tanganyika ilipata uhuru ukaporwa na Tanzania ambayo nayo pia haiko huru.
   
Loading...